EWURA waridhia kupandisha bei mafuta, bei mpya hizi hapa!

Status
Not open for further replies.
Ukweli ni kwamba wiki hii bei ya mafuta duniani imeshuka.

Lakini stock iliyopo imewasili kwa bei ya zamani duniani.

Kosa lingine kwa EWURA ni ku_calculate kwa kutumia exchange rate ya BOT wakati kampuni zinatumia ya commercial bank.

Rafiki tatizo hapa ni serikali iliyotaka kupata credit kwa kushusha bei ya mafuta haraka bila kujadiliana na waagizaji wa mafuta. Kwenye hili swala la kushusha mafuta tunasikia tu upande mmoja wa EWURA wakitaka makampuni yatekeleze amri ya kushusha mafuta.

Hivi sisi jamani lini tutaacha uvivu wa kusoma? Pamoja na ufafanuzi wooooote ule namna mchakato wa kuhuisha bei ulivyowashirikisha wadau wote toka mwanzo hadi mwisho, leo hii anakuja mtu anabwabwaja EWURA haikujadliana na wadau? Ndiyo nyie kwenye mikutano ya Public Inquiry hamuendi kujadiliana mambo hayo, ila Fiesta mnajazana tu, mambo yakibadilika mnakuwa wa kwanza kulalama hamkushirikishwa...unaowatetea mbona hawalalamiki kuwa hawakushirikishwa? hii JF ya siku hizi imekuwa balaa.

Kuna tetesi kuwa next week bei za petroli na diezel zitapanda! Sasa sijui ni serikali gani imeamua kuanza kudanganya kuaznzia bungeni na wabunge wake wakapitisha bajeti. Sasa sijui watakuja na hadithi gani kutudanganya.( maana kama mtoto wa raisi anafanya biashara hiyo lazima baba ahakikikshe mtoto anapata faida). Mtizamo wangu kama itakua hivyo:
1 ewura ifutwe na watendaji wake wanyongwe
2 serikali ichukue jukumu la kuagiza mafuta kutokana na mahitaji ya wananchi wake, kwani muagizaji anapokua msambazaji anawanyonga walaji, hapa ndio tutaona unafuu wa bei maana serikali haifanyi biashara, na pili ikumbukwe bei elekezi za ewura siku zote ni za juu sana.
3 wabunge na wanasiasa wote wanaofanya biashara ambazo zina interest kwa taifa waachie nyadhifa zao, maana hawa kwa pamoja wanashirikiana kutuletea mambo ambayo yana faida kwao pekee

Umesema kuwa EWURA walidhia kupandisha mafuta wiki ijayo kisha unaandika tofauti na kichwa cha habari
mbona hata hatukuelewi unachoandika humu hakiendani kabisa na kichwa cha habari.!!!!!

mtoa mada unataka kuhuadaa umma wa JF , tena bila shaka kwa makusudi, hivi nyie watu hamuridhiki tu na hiyo super profit mnayopata, ndugu , unaweza ukaifananisha 1 na 2 ila kamwe 1 haiwezi kuwa 2

huu ni usani tusitegemee jipya kutoka EWURA maana inafanya kazi chini elimu zisizofahamika ninamashaka na taaluma zao maana maamzi tu ni aibu kila siku

kama kuna mtu alifujatilia kipindi cha KIPIMA JOTO-ITV,siku ya Ijumaa..mwakilishi wa EWURA...alijaribu kujieleza,na badae akasema kuna uwezekano bei ya nishati ya mafuta inaweza kupanda wiki kesho kutokana na hali halisi.

Rafiki tatizo hapa ni serikali iliyotaka kupata credit kwa kushusha bei ya mafuta haraka bila kujadiliana na waagizaji wa mafuta. Kwenye hili swala la kushusha mafuta tunasikia tu upande mmoja wa EWURA wakitaka makampuni yatekeleze amri ya kushusha mafuta. Haiwezekani makampuni yote yakagoma kushusha bei wote. Kuna tatizo hapa.

Na unavojua kampuni kama BP si kampuni mchezo na wala hawana chembe ya ubabaishaji au kupindisha sheria ndio maana wanaigomea serikali make taratibu zote wanazifuata wakijua hata serikali ikiwashitaki itaumbuka tu. Mwezi wa sita ushuru unashushwa, mwezi wa saba bsi zinatakiwa kushushwa. Mafuta waliyolipia kodi zaidi serikali inakubali kuwarudishia pesa walizotoa kodi?

Hapa kuna tatizo ndio maana makampuni yanagoma. Tena BP. Yangekuwa haya makampuni ya kiswahili Oilcom, Moil, Camel na wababaishaji wengine ningewaelewa lakini BP. Hapa serikali imekurupuka. Ni makosa ya serikali ambayo inataka kuyakwepa kwa kubebesha waagizaji mzigo mbele ya jamii iliyochoka.
Makampuni yana cost model tofauti ndio maana Big Bon aliweza kuuza bidhaa kwa bei ya chini wakati wote. So it is clear kwamba huenda cost model ya BP inaifanya kuwa na uendeshaji ambao ni expensive so ili kupata faida lazima auze bei ghali. So hakuna jipya hapa.

Assume BP ana wafanyakazi expertriate watano na kila mmoja analipwa mshahara sawa na wamatumbi 20-50. Unadhani Big Bon atakuwa na cost kama hizo?

Alafu kama bei ya pipa imeshuka lazima ujiulize na exchange ya shillingi iko je?

Regarding exchange rate ya commercial na BOT. BOT haina exchange rate bali BOT in everage ya exchange rate za commercial bank. Hivyo EWURA haiwezi kutumia exchange rate ya Kasheshe bureau de changez.

Haya, EWURA watuambie TZS 2004 WALIPATAJE NA SASA 2114 WAMEPATAJE. NA KAMA WALIKOSEA, BASI WAWJIBISHWE, WENZETU ULAYA HAWAWEZI KUYUMBISHWA NAMNA HII

Bei Juu kuanzia Jumatatu hahahaha, nahaha kujaza full tank hamna vituo vinavyo uza

mtoa mada unataka kuhuadaa umma wa JF , tena bila shaka kwa makusudi, hivi nyie watu hamuridhiki tu na hiyo super profit mnayopata, ndugu , unaweza ukaifananisha 1 na 2 ila kamwe 1 haiwezi kuwa 2

soma tangazo la EWURA NDIO UTAJUA MIMI NI MKWELI AU MKWELE
MAADA NI KWAMBA EWURA WALIKOSEA FORMULA, NA SASA WAMEREKEBISHA, NINANCHOWAAMBIA WANANCHI WENZANGU NI KWAMBA WAWAJIBISHWE KWA KUTULETEA HASARA WANANCHI NA USUMBUFU MKUBWA, YAANI WEWE NA MIMI

soma tangazo la EWURA NDIO UTAJUA MIMI NI MKWELI AU MKWELE

MAADA NI KWAMBA EWURA WALIKOSEA FORMULA, NA SASA WAMEREKEBISHA, NINANCHOWAAMBIA WANANCHI WENZANGU NI KWAMBA WAWAJIBISHWE KWA KUTULETEA HASARA WANANCHI NA USUMBUFU MKUBWA, YAANI WEWE NA MIMI

Acha kudanganya kabla hata ya mgomo EWURA ilikuwa inatoa bei za kikomo kila week... Please watu sio maamuma.

ewura imetangaza bei mpya kwa mafuta ya taa, petrol na diesel kuanzia kesho-tz zaidi uijuavyo. source-tbc habari

Amini usiamini, kabla hata ya kupita wiki moja tangu serikali itoe mkwara kwa wauza mafuta kupunguza bei, leo ghafla bini vuup kwa kisingizio cha kudorora kwa sarafu yetu. Mkurugenzi wa EWURA ametangaza ongezeko la bei kwa wastani wa 5% . Bei hiyo itaanza kutumika kesho. (channel ten news).

Acha kudanganya kabla hata ya mgomo EWURA ilikuwa inatoa bei za kikomo kila week... Please watu sio maamuma.

Nadhani hujui nini kilitokea mpaka wauza mafuta waligoma, njoo ni kukufafanulie, send your email I will deliver a wrong template made by UWURA

Jamani kituo cha polisi jamani kujenga ni billioni na ushee au umekosea kunukuu!

Bora tukajiandaaa kuliasisha kwani serekali ahipo makini na wananch wake bora tusiwe nayo kabisa

KUMBUKA KWAMBA SABABU ZA KUANDAMANA TUNAZO LENGO TUNALO LA KUBADILISHA SEREKALI NA UWEZO TUNAO NAYO NGUVU KUBWA NAYO NI NGUVU YA UMMA MASIKINI . Amka MTANZANIA

kwa akili ya kawaida, Kutoka Ths 2004 hadi 2114 a difference of 110 TZS kweli tunaenda wapi na hawa EWURA

Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom