EWURA kutangaza bei mpya kesho; tunaenda sawa na soko halisi

BASIASI

JF-Expert Member
Sep 20, 2010
9,735
5,003
[h=2]EWURA kutangaza tena bei mpya kesho[/h]


Na Flora Wingia



14th August 2011


email.png

B-pepe



printer.png

Chapa



comment_bubble.png

Maoni





headline_bullet.jpg
Inaweza kupanda kidogo




Mamlaka ya huduma ya Nishati na Maji (Ewura), imesema inatarajia kutangaza bei mpya ya mafuta kesho (Jumatatu) tofauti na ile mpya iliyotangazwa Agosti 3, mwaka huu.
Hayo yalielezwa juzi wakati wa kipindi cha Kipimajoto kinachorushwa moja kwa moja na kituo cha ITV kila Ijumaa ambapo swali lililokuwa linajadiliwa ni: "Wenye vituo vya mafuta kuishiwa nishati hiyo baada ya kutangazwa bei mpya, je, serikali ichukue jukumu la kuagiza mafuta?"
Mmoja wa wageni waliochangia maoni katika kipindi hicho alikuwa Titus Kaguo, ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano Ewura, aliyetoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali kuhusiana na mgomo wa wauza mafuta nchini.
Kaguo alisema Jumatatu (kesho) Ewura itatangaza bei mpya ya mafuta aina ya petroli, dizeli na mafuta ya taa, tofauti na ile iliyosababisha mgomo na kuleta usumbufu mkubwa kwa wananchi kuhusu nishati hizo.
“Pengine Jumatatu tutatoa bei mpya lakini tulitaka kuwaambia Watanzania kwamba bei zilizokuwepo zilikuwa zinaonyesha dalili ya kushuka na hivyo bei huwa zinabadilika badilika wasije wakashangaa ikionekana ile Jumatatu zimetoka bei ambazo kidogo zina mabadiliko, wasiseme Ewura imeshindwa kufanya kazi, Ewura imenyoosha mkono kwa wafanyabiashara, imewaogopa.
“Tunaenda na hali halisi ya soko inavyofanya na exchange rate (kiwango cha kubadilisha fedha) inavyokwenda. Exchange rate imeshuka sana kutokana na thamani ya shilingi yetu kushuka. Kwa hiyo, matokeo yatakayotoka kwa bei hiyo mpya ambayo inafanyiwa kazi kati ya leo, kesho na Jumapili, Watanzania waipokee bei kama ilivyo wasiseme tumenyoosha mikono kwa wafanyabiashara kama kutakuwa na mabadiliko ya bei pengine kupanda kidogo,” alisema Kaguo.
Meneja wa Biashara ya petoli, Godwin Samwel kutoka Ewura alisema “Ni kweli baada ya mamlaka ya Ewura kutangaza bei mpya hapo tarehe 3.8.2011 tukaona kwamba kuna upungufu katika vituo na wenye vituo walibadilisha bei lakini wengi walikuwa hawauzi mafuta, tuliliona hilo tukaanza kufuatilia kuona kwa nini hali iwe hivyo. Alisema kilichofuatia ilifanyika mikutano kadhaa pamoja wenye vituo na watu mbalimbali wanaohusika na biashara ya mafuta.
Kuhusu chimbuko halisi la mgomo akasema, “mimi siwasemei, wao ni wafanyabiashara lakini ninachojua ni kwamba haukuwepo upungufu wowote. Mchakato tuliofanya tulifanya mchakato ambao ilikuwa ni wa kuangalia vipengele mbalimbali katika bei, katika formula (utaratibu) ya bei. Ni formula ambayo tumekuwa nayo kwa muda mrefu.
“Sasa ikafikia mahala ambapo tunataka kufanya marekebisho fulani, marekebisho ambayo tuliwashirikisha wadau wote na wale wafanyabiashara wa mafuta walishiriki. Ndio maana nasema kwamba hakukuwa na mapungufu yoyote lakini hilo la kwamba kwa nini hawakukiri siwezi kuwasemea kwa sababu liko katika mawazo yao,” alisisitiza.
Kuhusu suala kwamba wafanyabiashara hiyo ya mafuta walikua na uwezo wa kukaidi bei, Kaguo alisema; “Hapana. Hawana nafasi hiyo kwa sababu hatupangi bei kwa matashi yetu, tunapanga bei kwa sababu ni matashi ya sheria.
Na sidhani kama yuko mtu ambaye yuko juu ya sheria katika nchi hii kwa kwa hiyo tunapopanga bei kwa kutumia kanuni ambayo inakuwa katika mchakato ambao hata wao wameshiriki, hii tuna uhakika kwamba ni lazima watii kwa sababu ni sheria wala siyo suala la mtu wala si suala la Ewura ni sheria na kanuni za nchi.
Renatus Mkinga kutoka Action for Development Forward ambaye alishangazwa na masharti aliyotoa mfanyabiashara wa kampuni ya Engen kwa serikali. “Mimi sijapata kuona mfanyabishara katika nchi hii anaweza kuipa serikali ultimatum, kwamba nakupa masaa 24 wewe usiposhusha hii bei basi mimi nitaondoka. Hiyo ni serikali kweli unaweza kuipa ishara ya aina hii?, alishangaa.
Pia alisema kuwa umeme na mafuta ni vitu viwili pacha. Kukosekana kwa mafuta kuna athiri vitu vingi sana wilaya zote zinatumia jenereta ambazo zinaendeshwa kwa mafuta ili kuzalisha umeme, hospitali na mambo mengine yanayohitaji umeme.
“Kitendo chochote cha kucheza na biashara ya mafuta kama kinachotokea sasa ni cha hatari sana. Na hili ni kosa kwa serikali, unapobinafsisha mafuta, reli, miundombinu, umeme, unahatarisha usalama wa nchi”.
Zakaria Hans Pope kutoka Chama cha Wamiliki wa malori Tanzania (Truck Roads Association) alisema “Mimi kidogo nina mtazamo tofauti. Wengi wanatazama matokeo kuliko kiini. Na hata kufanya vile wanaingia jazba wanashindwa kufikiria . Nilikuwa nawasikiliza wabunge wanavyozungumza. Inaonyesha wazi hata wabunge hawajui biashara ya mafuta inafanyika vile.
“Watu wameingia jazba wanazungumzia magazeti wameandika habari ya saa 24 na kupotosha kila mtu na kuonekana kila mtu ana hatia. Lazima tujiulize, kwanini kitokee leo, Ewura wanasema wameshirikisha kila mtu. Kama wameshirikisha hawa watu ni vichaa kweli wao waje wazungumze tu kwamba haiwezekani hii bei inayotolewa sasa haifai? Lazima kuna kitu ambacho hawakuelewana. Mimi ningependa Ewura wangekuwa wazi na wakweli”.



CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
Ewura ni wababishaji wameona wameshindwa na wafanyabiashara hivyo kusalimu amri indirect! Nchi hii sijui inakwendaje?
 
kwa hiyo mzigo tunabebeshwa wananchi! wao wanaendelea kutanua na pesa za mauzo ya UDA, SPM MGOLOLO, DOWANS, MEREMETA, DEEP GREEN! mikataba ya RICHMONDULI, IPTL, AGGRECO, wanaweka full tank wanaingia mtaani kwa shangwe! jamani huu ndo wakati wa kufaidi matunda ya nchi yetu, tuanzishe cha TAHRIR SQUARE!
 
Mkiambiwa Tanzania mna serikali legelege mnakataa serikali gani ambayo haina msimamo inaendeshwa na matajiri afu mnatudanganya haki sawa, haki sawa hikowapi hapa wakati wenye kipato cha chini mnawakandamiza
 
Kuwa raia wa kawaida nchi hii kunataka moyo!
Hizi fluctuations za kila wiki za mafuta zinatoa taswira mbaya ya serikali mbele za wananchi!..Hivi kwa unyeti wa Nishati ya mafuta kwa jamii, serikali haiwezi kufikiria kusubsidise hizo bei zinazopanda ili kulinda heshima yake?...Au tutarudi kwenye kauli za kawaida za 'hazina haina fungu hilo!
Hakyanani ingekuwa Maji na Hewa vinapatikana kwa mfumo HUU wa mafuta, wengi tungesahaulika kwenye uso wa dunia!
 
Ewura wamekuwa kama vyama vya siasa kila kitu maneno tu, sasa kuna maana gani kushusha mafuta bei kwa siku nne halafu siku ya tano unapandisha!
Mnawatesa tu wananchi
 
lakini shilingi imeshuka mno!majuzi ilifika Tsh 1620/usd,binafsi sijui mwaka gani imewahi fika huko! Sasa sijui ni devaluation policy ya BOT or just market forces?
 
Back
Top Bottom