Ewe Mtanzania, utamkumbuka JK kwa lipi katika utawala wake?

Kwa kuasisi maisha magumu Tanzania ( in fact zeroooooooooo!!!!).
 
1. Kuongoza serikali ambayo yeye na mawaziri wake kila moja na lwake
2. Kuwa Rais wa kwanza Afrika kushikana mkono na Obama
3. Kutofungamana na kundi lolote ndani ya sisiyemu


hiyo ya kuwa rais wa kwanza kuonana na obama, marobist walikula $500000 za kodi yetu. kweli rais tunae anahongo kuonana na rais mwenzake..... credibility=o%
 
Maendeleo ya nchi yanapimwa kwa wingi ya magari barabarani. Mchumi mahiri sanaa!!!
 
Kuipatia haki yake Zanzibar na kuwatengenezea serikali ya umoja( na hili limechukiwa na wengi akiwemo katili Mkapa na Pinda na ndio maana mawaziri wake wanamchafua JK kwa kumharibia reputation yake)
 
Maswali hayo muulize mhidini michuzi kwani amekariri ile ya rais 'nimetoa hapa nakuwafikifisha hap'.
 
a. Kwa kujenga barabara kwa kiwango cha lami kupita marais wote Tanzania

b. Kuongeza university students enrollments kupita awamu zote za urais Tanzania

c. Kupeleka pesa nyingi sana maendeleo wilayani kupita rais yeyote Tanzania

d. Kuanzisha mchakato wa katiba mpya na hatimaye katiba mpya by 2015 (major achievement; marai wote walikataa zoezi hili)

d. Kuweka na kusimamia utulivu Zanzibar (major achievement hakuna rais aliweza hii kitu wengine hadi waliomba kuzamisha kisiwa)

e. Kupanua uwigo wa vyombo vya habari na uhuru wa vyombo vya habari..watu wanajiachia hadi wanaboa..(new culture imaged)

BEST PRESIDENT EVER IN TANZANIA; bisha sasa kwa hoja tukusikie..
 
  1. Kuanzisha mchakato wa Katiba
  2. Ni Raisi aliyehudhuria misiba mingi
  3. Kuanguka Jangwani na kwingineko
  4. Rais wa Kwanza kuwa na msafara wenye Ambulance
  5. Kuteua wakuu wengi wa Wilaya (jinsike) kama kulipa fadhila
  6. Kujenga Kaikulu kadogo pale Msoga
  7. Kumrudia mke mwenye kamvuto Salma baada ya kuukwaa Urais
  8. Rais mwenye wake na watoto wengi tofautitofauti
  9. Kukataa kura za Wafanyakazi
  10. Kusafiri hadi kuchoka
  11. Kufikisha mfumuko wa bei hadi 20% bila hata kushtuka
  12. ................................................nitaurdi baadae kidogo
 
a. Kwa kujenga barabara kwa kiwango cha lami kupita marais wote tanzania

b. Kuongeza university students enrollments kupita awamu zote za urais tanzania

c. Kupeleka pesa nyingi sana maendeleo wilayani kupita rais yeyote tanzania

d. Kuanzisha mchakato wa katiba mpya na hatimaye katiba mpya by 2015 (major achievement; marai wote walikataa zoezi hili)

d. Kuweka na kusimamia utulivu zanzibar (major achievement hakuna rais aliweza hii kitu wengine hadi waliomba kuzamisha kisiwa)

e. Kupanua uwigo wa vyombo vya habari na uhuru wa vyombo vya habari..watu wanajiachia hadi wanaboa..(new culture imaged)

best president ever in tanzania; bisha sasa kwa hoja tukusikie..

those are contructive,destructive je?

1. Kapanua wigo wa udini kwa kugawa vyeo kufuata dini yake
2. Katumia pesa mingi sana kwa safari zake nyingi za nje
3. Omba omba mkubwa kuliko marais woote waliokwisha pita
4. Mtaalamu wa kuwaacha wenzake waumie kataika siasa zake
5. Familia yake ni tajiri kuliko familia za marais walopita
6. Katengeneza makundi makubwa hatarishi kwa usalama wa nchi yetu bila kujua mwe3nyewe
 
Kiukweli kama kuna watu wanatakiwa kupimwa ubongo ni wafuasi wanamponda magufuli na kumsifia kikwete.

Kikwete ni Rais aliyepalilia na kurithi ufisadi kutoka kwa mwasisi wa ufisadi nchi hii.

Kikwete alishindwa kabisa kupambana na ufisadi mafisadi wakawa wanapanda mageti ya ikulu,Tulifikia hadi mahali watu wakatapeliwa kwa kuaidiwa kupewa kazi ikulu mpaka mkurugenzi wa mawasiliano kipindi hicho alifikia kutoa tangazo la kuwepo matapeli wanaowaleta watu ikulu na kuwaacha gatini leo hii watu wamesahau haya?

Yaani ikulu iligeuzwa pango la walanguzi kila kijana kujifanya usalama wa taifa mtaani.

Mimi mwenyewe ni muanga wa ikulu ya kikwete niliadiwa kupewa ukuu wa wilaya na afisa mmoja wa Serikali ya kikwete (jina nimelitunza) alikuwa akifanya kazi ikulu magogoni kipindi hicho nilitakiwa kutoa milioni 10 kashi ili aniunganishe kwa mkuu baada ya kugundua nazunguka na maafisa wa takukuru akaacha kupokea simu yangu dakika ya mwisho.

Ukweli lazima usemwe watu walitumia jina la kikwete kutapeli na kujipatia kipato

Wengine wengi walitumia jina la Ridhiwani kikwete kutapeli hawa ndio wengi zaidi taasi ya Urais ilikuwa imeingiliwa na kila aina ya ushenzi!!

Swala la uchumi ndilo watu wanalalamikia zaidi lakini ukweli ni kwamba uchumi wetu ulianza kufa baada ya kuua viwanda ndani ya utawala wa Mkapa ingawa Mkapa alijitahidi ku control inflation na shillings yetu ilikuwa na thamani sana kipindi hicho. Lakini ukweli unabaki kuwa bila na kuwa na viwanda vya kutosha ili Ku export bidhaa hakuna kutakachofanyika.

Kikwete alipoingia inflation ikawa continues mpaka anatoka madarakani aliacha inflation ikiwa katika kiwango cha juu mno !!

Shiling ilikuwa ikipromoka kwa kiwango cha juu mno mfano mwaka 2005 dola moja ilikuwa ikinunuliwa kwa 1200 lakini mwaka 2015 ilikuwa 2200 ongezeko la karibu 100%

Kikwete aliua uchumi sana ila anachokifanya magufuli ni kuzika uchumi wetu kabisa!!

Sasa hivi anasema mfumuko wa bei umeshuka sio kweli Sukari elfu 3000 mafuta pamoja na kushuka kwenye soko la dunia lakini bado sisi tumeshindwa kuyashusha alafu tunakenua eti mfumuko umepungua mfumko upi wa vyakula hivi watanzania mumesahau kwamba bado tupo kwenye kipindi cha msimu? labda kama umepunguza mfumuko wa bei wa nyanya ambazo na zenyewe ni za msimu kufika December tutazitafuta kwa tochi.

Kwa hiyo anayemsifia kikwete na kumponda magufuli bado wote wana matatizo mmoja aliua uchumi mwingine anazika uchumi.
 
Acha chuki zako za ki ngese, fanya kazi, asubuhi asubihi unaacha kutafuta hela umemuamkia mzee wa watu hebu mwache apumzike, ovyoooo!
 
Back
Top Bottom