Ewe Mtanzania, utamkumbuka JK kwa lipi katika utawala wake?

Kwa kukubali watuhumiwa walioiba fedha za EPA kurudisha na kutowapeleka mahakamani, kwa kuwapatanisha cuf na ccm zenj hadi kuwafungisha ndoa ya mkeka,kwa ku kuku daaah aisee kuna mengi ya kumkumbuka usingizi umenibana ngoja nikakojoe then nilale
 
sitosahau siku ile aliyosema, "Sasa mnataka mimi nikanyeshe mvua mtera, nikanyeshe kidatu.........," sijasikiliza tena hotuba zake. this was the funnest speech i ever heard.
 
Nitamkumbuka kwa net (chandarua) za ft 2.5 za msaada.Pia migomo na maandamano katika taasisi tofauti!
 
...Ari mpya nguvu mpya na kasi mpya
....Maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana
....Amethubutu ameweza na sasa anasonga mbele
 
Sina sababu ya kumsifu rais Kikwete na wala haijawahi kumsifu kwa lolote alilowahi kulifanya. Maana sioni chochote alichojitahidi kufanya kwa ustawi wa taifa letu. Mambo yote aliyowaahidi watanzania ukianzia na maisha bora kwa kila mtanzania, kilimo bora, uchumi unaopaa n.k; ameshindwa kabisa ila tuseme kuwa amefanikiwa kwa kuruhusu ufisadi, maisha duni na mfumuko wa bei unaopaa. Ametudanganya na kauli mbiu ya kujivua gamba kumbe ni kawawa funika kombe mwanaharamu apite.

Kiujumla, rais akiri kuwa suala la uchumi uliodorora, mfumuko wa bei, ufisadi ni sera yake binafsi na chama chake. Lazima wawe waungwana ktk hili kuwa limemshinda na awaeleze wazi wazi Watz bila kumumunya maneno jinsi alivyoshindwa ili Watz tujue tutakabiliana vipi na matatizo yetu.

Watu hutofautiana kwa jinsi walivyojaliwa vipaji mbali mbali. Wengine ni wanamuziki wazuri, waimbaji, omba omba wazuri, wasikivu, majambazi wazuri, mafisadi daraja A n.k. Vivyo hivyo ktk uongozi wa rais Kikwete, usanii wake umejidhihirisha bila kificho na hili kiungwana lazima alikiri. Naamini rais wetu hata kama ana udhaifu wake lazima tukiri kuwa uungwana anao ukilinganisha na wenzake wa CCM.

Niseme tu kuwa uungwana wake unatokana pengine kwa shinikizo kutoka nje au ni jinsi alivyo tu. Nataka tu niamini kuwa ndio hulka yake. Kitendo cha kuonyesha nia ya kuthubutu kukaa meza moja na vyama vya upinzani pamoja na shinikizo ndani ya chama chake ni suala la kheri kwa Watz ktk kujipatia katiba wanayoitaka.

Na kwa hili sinabudi kusema kuwa kazi aliyoianza ni sharti aimalize vizuri kwa amani na mshikamano. Kwa kushirikisha watz wote ili siku ikipatikana katiba waitakayo waseme ni katiba yetu sote na wala si ya CCM wala CHADEMA au CUF. Jambo hili ni chungu sana kwa CCM maana suala la kupatikana katiba ambayo watz watasema ni yetu, itawafanya CCM wasahau zile mbinu zao zilizokuwa zinawasaidia kushinda chaguzi mbali mbali na kuwa chama shindani.

Ukweli ni kuwa CCM kwa sasa si chama shindani maana kuna mambo mengi yanawafanya kisiwe chama shindani ukilinganisha na CHADEMA hasa kwa kuangalia kuwa dola ni ya serikali ya CCM. Katiba mpya kama ikienda sawasawa jinsi tunavyotaka watz ni wazi kuwa na CCM watajisahihisha ktk mienendo yao mbaya.

Rais Kikwete atakapohakikisha na kuisimamia katiba mpya; ikapatikana katiba ambayo kila mtanzania atasema kweli rais ametimiza wajibu wake hakika atakuwa ameiepusha taifa hili ktk hali tunayoiona ya kugawanyika na kuwa kitu kimoja. Wakifanya chaguzi zao na mambo mengine kwa amani ktk hali ya kushirikiana lkn ktk hali zao tofauti za ki-itikadi. Hili rais Kikwete anaweza kulisimamia na akitaka kulisimamia lazima aweke pembeni unazi wake wa ki-ccm na yeye kuwa mwenyekiti wa CCM; abaki ktk hali ya yeye kuwa kiongozi wa Tanzania. Maana akichanganya na unazi wa CCM basi Watz hawatapata kile wanachokihitaji na atalaumiwa vizazi hadi vizazi.

Kesho na kesho kutwa rais Kikwete hatakuwa kiongozi wa Tanzania. Atakuwa wapi wakati huo watz wanachinjana kwa kuruhusu katiba mbovu. Labda awe ameikimbia nchi. Lkn akirudisha ule mshikamano uliokuwepo toka mwanzo kwa kuweka misingi thabiti ktk katiba; ni wazi kuwa Tanzania itakuwa mfano wa kuigwa.

Sisi Tanzania hatuwezi hatuwezi kuota kuwa kama Marekani kiuchumi lkn kuna mambo ambayo tunaweza tukafanya kwa busara kabisa tukawa wa mfano kwa ustawi wa taifa letu.

Rai yangu kwa rais Kikwete na wabunge wa CCM: ni kuwa tuachane na itikadi zetu ktk masuala ya kitaifa; tufanye kazi tuliyotumwa na Watz. Tuwape katiba wanayoitaka. Kama hatutawapa katiba waitakayo wakianza kuchinjana mtawaongoza watanzania gani?

Tujitambanue kwa kauli mbiu isemayo: Utanzania (utaifa) mbele siasa/itikati zetu baadaye.
 
Ulivyoanza sikukuelewa, lakini sasa nimekuelewa. Hilo la kusimamia kabisa JK kama yeye yake hawezi kwa sababu inasadikiwa hana nguvu na ushawishi mkubwa chamani kuliko fisado E. Lowasa.

Kwa hiyo saizi mengi ya yanaonekana hayatatuliwi kimaslahi ya taifa bali kimaslahi binafsi.
 
Back
Top Bottom