European Union na Ufisadi Tanzania

mmakonde

JF-Expert Member
Dec 26, 2009
965
66
Nashangaa mpaka leo European Union haijawafungia mafisadi wa Tanzania kusafiri nje ya nchi,kwa kuwanyima visa.Wakati elites wa Kenya hawasafiri tena, nashangaa EU hawafanyi hivi TANZANIA?aU wanangoja vurugu za kisiasa ndio wafanye hivyo? Naona hii ni hypocricy kubwa.
 
Hivi ujui kuwa hao wa Europeans ndio wanaofaidiaka na ufisadi africa? Makampuni yao ndiyo yanayo bribe viongozi wetu, kwa kiasi kikubwa makampuni ya EU ndiyo yanayo fuel corruption africa.

Wakina Chenge na wenzake. wakipewa bribe bado wana zi-invest hukohuko kwenye EU Banks, Mkuu, nchi zao zinaidi kufaidika na contracts za kifisadi, wananchi wao wanapata kazi n.k

Kumbuka scandal za Rada, Ndege ya Mkapa, Madini n.k, wao wa EU waliusika na huu ufisadi, lakini kila siku ukisikiliza TV na Newspaper zao, wanasema viongozi wetu tu ndio mafisadi wao wanao bribe kwao sio makosa. Tuwe makini na hawa watu Mkuu, tusiwategemee.
 
Chanzo cha ufisadi nchi zinazoendelea ni "Development Incorporated" ikijumuisha taasisi zote za nchi zilizoendelea unazofikiria zinatowa misaada ili nchi zinazoendelea ziendelee! Hata hayo ya Kenya ni danganya toto. Miaka yote hiyo leo ndio waonekane ni wakali. Hebu tafuta kajitabu kanachoitwa "Lords of Poverty" kalichoandikwa na Graham Hancock ujionee madudu ya ulimwengu. Hapo utaelewa ni kwanini mwalim Nyerere alikuwa adui wa IMF na WB. Pia utaelewa kwanini BM alishinikiza kulipa "madeni" na ubinafsishaji usiokuwa na mipango. Pia utajuwa ni kwanini vyama vya upinzani vinapewa misaada vishinde uchaguzi. Unaweza kupata haka kajitabu katika moja ya maduka ya duty free pale JNIA.
 
Hivi ujui kuwa hao wa Europeans ndio wanaofaidiaka na ufisadi africa? Makampuni yao ndiyo yanayo bribe viongozi wetu, kwa kiasi kikubwa makampuni ya EU ndiyo yanayo fuel corruption africa.

Wakina Chenge na wenzake. wakipewa bribe bado wana zi-invest hukohuko kwenye EU Banks, Mkuu, nchi zao zinaidi kufaidika na contracts za kifisadi, wananchi wao wanapata kazi n.k

Kumbuka scandal za Rada, Ndege ya Mkapa, Madini n.k, wao wa EU waliusika na huu ufisadi, lakini kila siku ukisikiliza TV na Newspaper zao, wanasema viongozi wetu tu ndio mafisadi wao wanao bribe kwao sio makosa. Tuwe makini na hawa watu Mkuu, tusiwategemee.

Very well said na we have all the evidence jamaa hawa ni wabaya sana na vipesa vya vya misaada ni kiini macho
 
Back
Top Bottom