Eti waungwana kwanini jeykei kabandika mabango ya picha zake nyingi kupita kiasi?

kaka hujakosea ni kweli, Kibaya chajitembeza kizuri chajiuza.
 
ili watu wamjue maana tangu aingie madarakani hana tukio muhimu sana alilolifanya watu wamkumbuke
 
:amen:Kupita kiasi kipi, ndugu. sidhani kama kulikuwa na Idadi ya mabango ya kutundika iliyopangwa na tume. Ila naamini kampeni ni sawa na biashara zingine zozote. Ni lazima uwekeze vya kutosha katika matangazo na utangaze bidhaa yako ili watu waijue na kuinunua. Soda ya coca cola ni maarufu sana duniani lakini inatangazwa utadhani ndio inaaingia sokoni kwa mara ya kwanza. Kampuni zetu za simu zinatangaza kwa ushindani mkubwa kwa kutoa zawadi kedekede kwa lengo la kuvuta wateja. Vivyo hivyo kw wanasiasa, wao kipindi cha kampeni ni sawa na bidhaa iliyoko sokoni ikihitaji mnunuzi na ni kazi ya mwenye bidhaa kuhahakisha inauzika kwa gharama yoyote. sina ugomvi na matumizi ya mabango hata yakiwekwa hadi msalani, ugomvi wangu ni output baada ya bidhaa hiyo kununuliwa na kukalia Ikulu.
 
Hahaaaaa kapiga picha na chege halafu eti imeandikwa mtu wa watu...dash rais kweli tunaye
 
[sina ugomvi na matumizi ya mabango hata yakiwekwa hadi msalani, ugomvi wangu ni output baada ya bidhaa hiyo kununuliwa na kukalia Ikulu. originally posted by jackob ]

Mara nyingi historia inatuonyesha ufisadi mkubwa hapa duniani,uliyofanyika katika serikali mabalimbali duniani, chanzo chake kikubwa ni kufadhili garama kubwa za kampeni za siasa.Na hata ukiangalia hapa hapa nchini kwetu ufisadi wa EPA,ulitokana na heka heka za kugaramia kampeni za CCM za 2005,ili mgombea wa CCM apata ushindi wa kishindo.Sasa ushindi wa kishindo unatakiwa usitokana na kumkandamiza mtanzania masikini,ndiyo maana watu wanalalamikia mabango mengi ya JK,kwa kuwa wanahisi fedha hizo zinaweza kuwa fedha za walipa kodi kinyume na sheria na taratibu za nchi yetu.Naona wewe umelalia zaidi kwenye principle za marketing,sote tunalijua hilo,lakini hofu yetu ni wapi fedha hizo wamezitoa?Hatuongelei ushabiki wa vyama!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
huko huru kujinadi kwa wananchi kwani vyama vingine vimekatazwa kuweka mabango yao....?????

Kwani hakuna anayemjua si aliishawahi kuwa waziri wa mambo ya nje, si amekuwa rais kwa muda wa miaka mitano sasa anajinadi kitu gani ambacho watanzania wasichokijua au anajinadi ufisadi
 
Au ndio ukamilifu wa methali isemayo kibaya chajitangaza...kizuri chajiuza!
Pamoja na hivyo, yafuatayo pia ni sababu kubwa sana;

  1. Hana uchungu na fedha za walalahoi; na ndio maana mabango hayo yameprintiwa Canada, na kulipwa malipo ya kwanza USD 1.5 million kutoka hazina...!
  2. Ufisadi uliokaa damuni hadi hata kiwango cha matumizi yanamshinda...! Sasa utangazaji huo umeshafikia hatua ya "Diminishing Returns".....!
  3. nk.
 
Pamoja na hivyo, yafuatayo pia ni sababu kubwa sana;


  1. Hana uchungu na fedha za walalahoi; na ndio maana mabango hayo yameprintiwa Canada, na kulipwa malipo ya kwanza USD 1.5 million kutoka hazina...!
  2. Ufisadi uliokaa damuni hadi hata kiwango cha matumizi yanamshinda...! Sasa utangazaji huo umeshafikia hatua ya "Diminishing Returns".....!
  3. nk.
Huoni kama yeye ni HANDSOME na anapendeza kwenye mabango!
 
Hahaaaaa kapiga picha na chege halafu eti imeandikwa mtu wa watu...dash rais kweli tunaye

Kweli mtu wa watu, Kwenye red hapo, umesahau kumpa bajaji yule mama mlemavu na kuwapa pipi watoto..,
Hivi Mh JK anawashauri kweli??
 
Kazi kweli kweli, biashara ni matangazo na biashara yenyewe iko Ikulu.
Lakini biashara itawezekana tu indapo watu watampigia kura, tusipompigia kura biasha itakuwa imeharibika.
 
ana maandalizi ya kutosha hajakurupuka kutafuta urais ndio maana (mind you kitu resource kabla hujafanya kitu) hao wengine wanaiga tuu hata ofisi zao zenyewe wamepanga.

Hureeeeeeeeee CCM HOYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE

wana jamii itikieno HOYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE
 
Back
Top Bottom