Eti watu 10 wamekamatwa Mwanza kwa kumzomea Pinda Mwanza?

Habari wakuu,

Kuna taarifa nimezipata kutoka kwa mmoja wa makada wa CCM Mkoani Mwanza kuwa watu 10 wamekamatwa kwa kitendo cha kumzomea Waziri Mkuu Pinda pale uwanja wa Sahara Jijini Mwanza. Kada huyo ya CCM ameonyeshwa kusikitishwa na kitendo hicho akisema kuwa kitendo hicho ni uhuni na kwamba kuzomewa kwa Pinda ni ujumbe unaotakiwa kufanyiwa kazi na CCM na serikali yake na si kukamata watu.

Nimejaribu kuzungumza na baadhi ya askari polisi jijini Mwanza juu ya taarifa hizi, wamekiri kwamba juzi watu sita walikuwa wamekamatwa na polisi kitengo cha intelijensia kwa mahojiano kuhusiana na Pinda kuzomewa hata hivyo wamesema hawajui kama waliendelea kushikiliwa au waliachiwa. Aidha nimezungumza na mmoja wa askari wa kitengo hicho yeye amekanusha vikali habari hizi.

Tufuatilie ili tujue ukweli kisha tujadiri kama ni halali kumkamata mtu eti kisa kamzomea kiongozi wa serikali kwa kusema hatuitaki CCM!

Ni kama mtu mwenye mke kiruka njia,na kila akimfumania anapiga mwanamume huku akimbembeleza mamaa na kumwomba samahani.Huyu mwanamke hatoacha jiachia kwa kila mwanamume amtamaniye popote.Ipo siku mamaa anachukuwa mbabe na kumuaminisha kuwa hana mume kwani walishaachana, na huyu mume akija na kisirani chake cha kupiga watu bila jieleza vyema ataambulia kichapo.

Kwa ujumla uozo wa CCM hauna tofauti sana na changudoa au uozo,watapiga na kuua kila mtu ila kila waendapo kuguu lazima wavutike.
 
Back
Top Bottom