eti Utafiti (research)St.AUGUSTINE UNIVERSITY NI LAZIMA KIINGEREZA, KISWAHILI KITAKUA KWELI

Mwl Mkwaya

Member
May 20, 2011
68
7
Wadau naomba tusaidiane, eti nasoma degree ya kwanza, St.Augustine University of Tz( branch ya tabora) sheria ni lazima Utafiti uwe kwa lugha ya kiingereza hata kama unasoma kiswahili. Je inawezekana kufanya utafiki wa lugha kiswahili kwa lugha ya kiingereza! Nisaidieni chururu si ndondondo kwa kidhungu vp??
 
Nadhani hapo wamechanganya mambo (kama ni kweli). Kama unasomea kiswahili, itakuwaje ufanye utafiti wako kwa lugha nyingine? Hiyo ni kama vile kusema unasoma kiingereza halafu ulazimishwe utafiti wako uwe wa kiswahili. Au wale wanaosoma degree ya kifaransa waambiwe utafiti uwe kwa kiingereza, kitu kama hicho hakipo.
 
Mwongo wewe, hamna kitu kama hicho. kwanza sidhani kama wanatoa hata hiyo degree ya kiswahili
 
Mkubwa usichanganye mambo hapo, we unasoma degree ya kiswahili au unafanya utafiti wa kiswahili, kwasababu unaweza ukawa unachukua degree ya kswhl ila unafany utafit wa kitu kingine so u shud uz english ila kama unafany utaft wa kiswahl bas unapaswa utumie lugha ya kswhl.
 
Nadhani inabidi uulizie zaidi kwa supervisor wako pengine hujamwelewa au ni kweli anamaanisha hivyo. Ninavyojua unaweza kuandika 'research proposal' kwa lugha ambayo funder au supervisor anapendelea (sidhani kama idea inabadilika) ILA 'dodoso=qustionnaire' lazima liwe limetafsiriwa kwa lugha ambayo wale 'study subjects' wataielewa ili waweze kujaza.

Ila sasa kama kiswahili ni principal subject kwako, napata ugumu kidogo kwann supervisor alazimishe kiingereza.Nadhani tuache 'copy & paste' tuwe wabunifu kidogo otherwise atakua anatenda tofauti na kile anachohubiri.
 
Kutokana na ID yako naamini unasoma shahda ya kwanza katika elimu (BA Ed au BEd) na masomo yako ya kufundishia ni pamoja na Kiswahili (Niko tayari kusahihishwa). Hivyo si sahihi kusema kuwa unasoma shahada ya Kiswahili.

Somo la "research methods" ambalo ndilo unalolitumia kama nyenzo ya kufanya utafiti wako ni somo la jumla na si kwa kufuata kile unachokifanya kama masomo ya kufundishia.

Onesha hekima yako na ficha upumbavu wako. Sosi: Invii
 
Kutokana na ID yako naamini unasoma shahda ya kwanza katika elimu (BA Ed au BEd) na masomo yako ya kufundishia ni pamoja na Kiswahili (Niko tayari kusahihishwa). Hivyo si sahihi kusema kuwa unasoma shahada ya Kiswahili.

Somo la "research methods" ambalo ndilo unalolitumia kama nyenzo ya kufanya utafiti wako ni somo la jumla na si kwa kufuata kile unachokifanya kama masomo ya kufundishia

Onesha hekima yako na ficha upumbavu wako. Sosi: Invii

Ndugu Gurta, nadhani mleta uzi Mwl. Mkwaya hakustahili matusi ila maelekezo kama ulivyomfanyia hapo palipokozwa rangi. Ni ukweli bayana kwamba mleta hoja amedanganya kutuambia kuwa anasoma shahada ya Kiswahili halafu analazimishwa kuandika Pendekezo la Utafiti au Utafiti wenyewe kwa lugha ya Kiingereza. Alichokisema Gurta ndio ukweli wenyewe kwamba Mwl. Mkwaya amechukua kozi nyingine, labda inaitwa introduction to research methods, na anatakiwa kufanya utafiti ni lazima atatumia lugha ya Kiingereza kwa sababu ndiyo lugha ya kufundishia Elimu ya Juu. Lakini pia inawezekana anasoma Shahada ya Linguistics ambapo somo lake la upendeleo ni Kiswahili bado atalazimika aandike utafiti wake kwa Kiingereza. Lakini ikiwa shahada yake anayosoma ni B.A. (Kiswahili) na amefundishwa kozi iitwayo Mbinu za Utafiti za Sayansi Jamii ila kwenye kuandika Pendekezo la Utafiti na Utafiti wenyewe akalazimishwa kuandika kwa Kiingereza, hata mimi naona hapo pana mushkeli. Ni bora mleta hoja afafanue kindakindaki halafu tubadilishane tajriba.
 
Oky ! Labda nimaelezea vibaya, nasoma BAED(linguistics an Kiswahili) bt utafiti forced kuwa wa kiiengereza.. Je nasoma hivi na favour yangu kubwa ni kubase kwny Kiswahili so ni lazima kuandika hiyo kitu kwa kidhungu, ...But all in all asante wachangiaji kwa strong and harsh words zenu(sio wote) , nahisi ni vema kudadisi zaidi kisha ndo judge; am still learning, kama nimeandika kitu kwa kushindwa kukieleza perfect ni vema kuniweka sawa, kisha kunipa muongozo!! Ningekuwa najua kila kitu nisingetaka ushauri au muonozo !! Am disappointed wth some of your answers Wachaniaji !! Hav a blessed Sunday....

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Gandagumu kivip matunda ya shule za kata???

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Gandagumu kivip matunda ya shule za kata???

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

Yaani wewe ndugu unataka kutuambia kuwa hujui matunda ya shule za Kata? Miongoni mwa watokao kwenye shule hizo ni wale wanaoharakia majawabu bila kujisumbua kufahamu njia za kuyafikia majawabu hayo. Matokeo yake ni kwamba hata wanapopewa dhamana ya kutoa huduma kwa jamii huishia kumkata goti mgonjwa anayehitaji upasuaji wa kichwa. Miongoni mwa hao wamo walalamikaji wakubwa kwa mambo ambayo utakuta ni wajibu wao wa msingi kabisa. Utamkuta mtu anapewa mtihani shuleni lakini anaanza harakati za kuwashawishi wenzake waukatae mtihani huo kwa madai kwamba mtihani sio wenyewe! Hawataki kusoma vitabu ambavyo ndani mwake mna maarifa na elimu badala yake watapenda kupata tahakiki au mapitio ya vitabu hivyo. Wakipewa orodha ya vitabu vya kusoma katika kozi fulani wao watapiga kelele kwamba wana mambo mengi ya kufanya na badala yake watamzonga Mhadhiri awape nukuu za kozi yake na watazirudufisha hizo na kuzifanya kama rejea. Hebu jitazame kama haumo ndani ya kundi hili Mwl. Mkwaya!
 
Vema, asante kwa kunijuza....!! But sijasoma shule ya kata so far!.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Wadau naomba tusaidiane, eti nasoma degree ya kwanza, St.Augustine University of Tz( branch ya tabora) sheria ni lazima Utafiti uwe kwa lugha ya kiingereza hata kama unasoma kiswahili. Je inawezekana kufanya utafiki wa lugha kiswahili kwa lugha ya kiingereza! Nisaidieni chururu si ndondondo kwa kidhungu vp??

Wewe unasoma kiswahili halafu hata hiyo sentensi kwa kiswahili umeikosea! ni "ndondondo si chururu".
 
Habari yako Mwl Mtarajiwa Mkwaya, mimi mwenyewe nimesoma SAUT, Kiswahili/History.Kufanya utafiti katika somo la kiswahili kwa kutumia lugha ya kiingereza inawezekana kabisa. Jaribu kuonana na waalimu wako, watakuelekeza vizuri,kwani nwengi wamefanya hivyo na imewezekana.
 
Back
Top Bottom