Eti tusizaane ili kuepuka uharibifu wa mazingira!!!

vukani

JF-Expert Member
Dec 30, 2009
245
165

Kila sekunde moja wanazaliwa watoto watano hapa duniani, na wakati huo huo watu wawili wanafariki dunia, achilia mbali zile mimba zinazoharibika.

Maana ya tofauti hiyo kati ya vizazi na vifo ni kwamba watu watatu wanaongezeka duniani kila sekunde moja. Ukizidisha idadi hiyo utagundua kwamba kuna ongezeko la watu 11,000 kwa saa na watu 265,000 kwa siku na hii inafanya dunia kuwa ongezeko la watu milioni 100 kwa mwaka.

Hivi sasa dunia ina watu wapatao bilioni 6.7. Mwaka 1750 kulikuwa na watu milioni 800 tu duniani. Kufikia mwaka 1850 idadi iliongeka na kufikia watu bilioni 1.8.
Mwaka 1950 idadi ya watu ikawa bilioni 2.5. Ilichukuwa miaka 50 idadi ya watu kufikia bilioni 6 yaani mwaka 2000. Inakisiwa kwamba mpaka kuikia mwaka 2010 idadi ya watu hapa duniani itafikia watu bilioni 7, ikiwa ni ongezeko la watu bilioni 1 kwa muda wa miaka 10.
Ukiangalia mtiririko wa takwimu hizo utagundua kwamba idadi ya watu imekuwa ikiongezeka kwa kasi hapa duniani kuanzia karne ya 19.

Kwa mfano nchi yetu ya Tanzania iko chini ya kiwango cha ongezeko la watu hapa duniani ukilinganisha na nchi nyingine zilizoko dunia ya tatu.
Tanzania ina ukubwa wa eneo la mraba mita la 342,100, karibu sawa na Misri ambayo ina ukubwa wa mita za mraba 384,300.

Pamoja na kwamba tofauti ya ukubwa kati ya nchi hizi mbili ni ndogo sana lakini Tanzania imezidiwa kwa idadi ya watu karibu mara mbili na Misri. Kwani wakati Tanzania ikiwa na idadi ya watu wapatao milioni 38, Misri ina idadi ya watu wapatao milioni 71.

Ikiwa utaiunganisha Tanzania na nchi ya Benin iliyoko Afrika Magharibi ukubwa wake utalingana na nchi ya Misri, kukiwa na tofauti ndogo sana. Ukijumlisha idadi ya watu wa nchi ya Benin wanaokadiriwa kufikia milioni 7 na idadi ya watu wa Tanzania unapata idadi ya watu wapatao milioni 45, ikiwa bado ni chini ya idadi ya watu wa nchi ya Misri.

Hii inaonesha bado nchi hii ina kiwango kidogo sana cha idadi ya watu ukilinganisha na nchi nyingine zilizo katika dunia ya tatu.
Kwa hiyo sioni sababu ya serikali yetu kupiga kelele sana kuzuia watu wasizaane, Je tunataka hayo mapori yaliyoenea hapa nchini wakae kina nani?

Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, ulikadiria kwamba watoto milioni 1.6 huzaliwa kila mwaka hapa nchini. Na kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa hivi karibuni na wizara ya afya zinaonesha kwamba watoto wanaosajiliwa ni 140.000 kila mwaka ikiwa ni asilimia 10 tu ya watoto wanaozaliwa, hii inaonesha kwamba kuna idadi kubwa ya watoto wanaofia tumboni, na wale wanaofariki baada ya kuzaliwa inakuwa haijachukuliwa na kuingizwa kwenye takwimu za serikali.
Hata hivyo inakadiriwa kwamba watoto wapatao 51,000 hufariki baada ya kuzaliwa hapa nchini, na wakati huo huo 43,000 hufia tumboni kila mwaka.

Kwa mujibu wa takwimu hizo inaonesha kwamba bado tunayo safari ndefu ya kupunguza idadi ya vifo vya watoto wanaozaliwa hapa nchini, kabla hatujaanza kupiga kelele ya watu kuzaa kwa mpango.

Mataifa makubwa yanadai kuwa ongezeko la watu linasababisha uharibifu mkubwa wa mazingira, na hivyo kutishia dunia isiwe salama.

Kwani kumekuwa hakuna udhibiti wa kutosha kiasi kwamba watu wamekuwa wakitawanyika kwa ajili ya kutafuta makazi na hivyo kuvamia maeneo ya misitu ya asili na vyanzo vya maji na kufanya uharibifu mkubwa mkubwa wa mazingira.

Imebainika kwamba iwapo watu hao watasogezewa miundo mbinu kama vile Barabara, shule, hospitali, na huduma mbali mbali za kijamii, ina maana ya kuhalalisha uharibifu wa mazingira.

Pia wataalamu hao wanadai kwamba ongezeko la watu haliendi sambamba na ujenzi wa miundo mbinu ambayo itasaidia kulinda uharibifu wa mazingira.

Hata hivyo ukiangalia upande mwingine wa shilingi, unapata nadharia inayopingana na nadharia ya wataalamu hao.
Kuzungumzia ongezeko la watu, unazungumzia ongezeko la soko, kwa maana ukuaji wa biashara, nguvu kazi, na ongezeko la viwanda, na hivyo ukuaji wa uchumi kuongezeka. Kwani kwa jinsi idadi ya watu inavyozidi kuongezeka na ndivyo uchumi unavyozidi kukua, hebu angalia nchi kama ya China, India, Marekani na iliyokuwa Urusi kabla haijasambaratika, ukuaji wa uchumi katika nchi hizo ulitokana na kuwa na idadi kubwa ya watu.
Ila naomba nitahadharishe kidogo hapa, ninapozungumzia ongezeko la watu na ukuaji wa uchumi nazungumzia nchi kutumia nguvu kazi katika kuzalisha na kuwa na serikali makini inayowawezesha wananchi wake kufikia malengo yao na sio watu kuwa wavivu wakisubiri kila kitu kifanywe na serikali.

Naomba nikiri kwamba aina ya maisha tunayoishi hapa nchini hatuwezi kupiga hatua kimaendeleo hata kama kukiwa na ongezeko la watu. Watanzania tumeshindwa kutumia fursa zilizopo na matokeo yake wageni ndio wanaozichangamkia, huku sisi tukibaki kuwa watazamaji.

Wengi tunapenda njia za mkato katika kujiletea maendeleo na ndio maana vitendo vya rushwa na ufisadi vinaiyumbisha nchi.

Kama tunataka maendeleo ya kweli yatupasa kubadili namna yetu ya kufikiri, la sivyo tutazaana na kujikuta tukibaki kuwa ombaomba ndani ya nchi yetu.

Inabidi kila mtu ajiulize afanye nini ili kujiletea maendeleo na sio kukaa na kulalamika na majungu, haitatusaidia zaidi ya kupoteza muda huku dunia ikiendelea kusonga mbele kwa kasi ikikuacha ukiwa umesimama.
 
Back
Top Bottom