Eti taifa stars walishindwa kuifunga zimbabwe kwasababu ya rangi za jezi zao!

Haika

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,348
559
Eti ni kwamba, wachezaji wengi wa Taifa Stars wanatoka Yanga, jezi za Wazimbabwe ni kama za Yanga...., kwanini wasione ni kama yanga B! Ya kweli haya ndugu wadau? Na kama ni hivyo, huko Ivory cost itakuwaje wakikutana!
 
Mimi nimesikia kuwa ni kwa sababu wachezaji wetu hawakuvuta bangi! Ukweli ni kuwa siku hiyo wachezaji wetu walikuwa na viwango vya chini mno.
 
Heh! makubwa. Kwani kama walikuwa wamevuta angalau two weeks back isingewasaidia. Maana nasikia huwainakaa mwilini kama wiki mbili vile!
 
Tangu tumpate kocha wa timu ya taifa(Taifa stars)mbrazil Marcio Maximo;kuna baadhi ya mambo katika utendaji wa timu amejitahidi kurekebisha.Lakini tatizo kubwa na ambalo la mara kwa mara kujitokeza katika timu yetu,ni safu nzima ya ushambuliaji ambayo ndiyo butu sana.Hatuna strikers wa ku-net(kutupia mpira katika nyavu),kwa mfano katika mechi hiyo ya Zimbabwe Vs Tanzania middle fields players ndiyo haohao strikers.Kilichoonekana hakuna strikers,hivyo basi ni suala la kutafuta magoli kwa kubahatisha tu.
Hiyo ndiyo sababu kubwa iliyowekwa hadharani na wadau wasoka.
 
Ni kweli kabisa mkuu Ibrah,sababu ya kucheza chini ya kiwango inasadikika eti ni kuzuiwa kuvuta bangi nadhan itawaaffect sana hata huko Ivory coast maana naambiwa hawawezi kucheza bila kupuliza wakiongozwa na kijana Haruna Moshi Boban.
 
Nimesikia karibu first eleven yote stars wanavuta bangi
 
Mimi naona wapewe bangi wavute......watanzania tunataka ushindi no matter what.....ila wasiwape cha arusha watazima uwanjani.....
 
Back
Top Bottom