Eti serikali inaagiza cement kutoka nje na viwanda vyetu kukosa wanunuzi

zamlock

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
3,840
657
Kwa habari niliyo pata kutoka pale wazo kiwanda cha cement inasemakana serikali saizi inaagiza cement kutoka nje kwa matunizi yao na kwa ile cement inayobakia wanampatia mhindi mmoja anaitwa Zakaria ambaye naye ufanya biashara kwa kuuzia watu.

Hizo ni taarifa nilizopewa na wafanya biashara niliowakuta pale Wazo wakilalamika kuwa cement imejaa kiwandani na wanunuzi hakuna kwa sababu serikali imejiingiza na swala la kuagiza cement ambapo serikali ilipaswa kuvipa nguvu viwanda vyetu na kutoa fursa kwa vijana kujipatia ajira.

Kwa mtu mwenye uelewa zaidi kuhusu jambo hili, ni vyema tukaliweka hapa na lijadiliwe na watanzania kujua ni kwa nini serikali ichukue jukumu la kuagiza cement wakati tuna viwanda hapa kwetu.
 
Week iliyopita nilikuwa naongea na boss mmoja toka Tanga Cement na nilipata bahati ya kumuuliza kuhusu bei za cement (imported na hii ya kwetu hapa). Tumekuwa tunapata Cement toka Pakistan na kuna tofauti za bei kati ya cement ya ndani na ile iliyotoka nje ya nchi. Imported mara nyingi huwa na bei nafuu na sababu moja ni kodi, lakini kuna kitu kimoja alinigusia, Quality ya cement ya Tanzania na ile ya Pakistan ni tofauti. Mimi sio mtalaam wa cement lakini mara nyingi watanzania tumegeuzwa jalala la vitu toka nje, na kwa hili pamoja na kwamba aliyekuwa ananieleza ni boss wa kampuni ya cement hapa nimeamua kuamini (walau kwa sasa) kuwa cement ya Tanzania ni bora kuliko ya Pakistan.

Kwa sasa hivi natafuta more details kwa watu wenye uelewa wa kitaalam juu ubora, hata hivyo kama kuna mtu mwenye huo ujuzi basi atufanunulie maana tunaweza kuendelea kuwa jalala la bidhaa mbovu.

La mwisho, kwa makampuni kama Tanga cement au Wazo, viwanda ambavyo ndugu zetu wanafanya kazi huko na kama product (cement) inayotengezwa ni good quality basi ni jukumu la kila mtanzania kuwaunga mkono. Made in Tanzania
 
Taabu ya cement ya bongo quality mkuu!haswa hii ya wazo!ukiwa na cement ya nje unapata tofali nyng zaid kwa one bag than kutumia hii ya kwetu!but simba cement is the best!hushangai Konoike wanatumia simba cement from tanga than kutumia cement ya wazo,jiulize
 
Taabu ya cement ya bongo quality mkuu!haswa hii ya wazo!ukiwa na cement ya nje unapata tofali nyng zaid kwa one bag than kutumia hii ya kwetu!but simba cement is the best!hushangai Konoike wanatumia simba cement from tanga than kutumia cement ya wazo,jiulize

Encouraging news mkuu wangu. Boss niliyeongea nae ni wa Tanga cement, na alisema haya unayosema kuwa quality ya cement toka kiwandani kwao (Tanga cement) ni nzuri kuliko imported one. Nadhani ni vizuri habari kama hizi tupeane maana hakuna kitu kinachoodhi kama nyufa.
 
Bora ya NJE ije tuu!ya tanzania haina ubora kama ya nje pia bei rahisi.zakaria mkombozi wa nchi mafuta ya kula,sukari,cement huingiza nchini pindi viwanda vyetu vinapochemsha kama sasa sukari
 
Suala la kuagiza cement toka nje ni miradi ya watu binafsi ila wakitumia mgongo wa serikali!
Suala la ubora Kama lacky cement huwa inatengeneza cracks ukiwa waitumia kujenga hivyo si nzuri
Alafu kwa serikali makini huwezi agiza bidhaa kutoka nje unless capacity ya viwanda vyako iko chini!
Jiulize sukari mara nyingi inakuwaga haba lakini husikii imeagizwa toka nje kisa kwenye ivyo viwanda kuna mikono ya wakubwa tofauti na ivi vya cement!
Ata sielewi waziri wa viwanda na biashara anangoja nini kulivalia njuga hili
Ivi viwanda vya cement over a long run vyaweza stop production na kufanya retrenchment ya watu ambao ndo wapiga kura wa 2015
Ndo maana naungana na mtu aliyesema CCM inajichimbia kaburi lake yenyewe bse retrenched people wataongeza chuki dhidi ya serikali yao!
Na izi imported cement zauzwa cheap bse ya tozo dogo la kodi na zingine hazitozwi kabisa ikiwa ni kama miradi ya baadhi ya watu wenye uchu na uraisi 2015
 
kikwete is calling this economic policy for Tanzania ... tumuulize mkullo na ndulu si unemployment itapungua if you continue importing goods and exporting foreign currency at the same time?

This is incredible! Let's see how many goods kikwete is importing from other middle east and Asian countries. What a shame! sugar, rice, fuel, tea, clothes, cement, water, people from China.
 
Serikali imeenda likizo. Ikirud itatoa tamko lake.
 
Mimi sijui hayo ya quality lakini kama mtu ambaye nimepitia adha ya kujenga nyumba naunga mkono suala la cement kuagizwa toka nje ya nchi. Bezi za cement nchi hii zinabadilika kama homa za vipindi. Hivi viwanda vyetu vimengángánia kulindwa na serikali wakati utendaji wao ni mbovu. Wameunda syndicate na wafanyabiashara na wanapandisha bei za cement kwa kutengeneza artificial shortage kwenye soko. Wao badala ya kuzalisha cement nyingi ili wauze mifuko mingi ya cement kwa bei nafuu na kupata faida based on quantity wamekalia kubana supply ili wauze mifuko michache kwa bei kubwa zaidi. Pu.....................fu zao.
 
hata kwa maelezo ya watu nilozungumza nao pale wazo wanamlalamikia sana zakaria na baadhi ya viongozi serikalini kuwa ni chanzo cha wao kudidimiza biashara ya cement ya hapa kwetu na kwa sasa akuna cement inayonunuliwa kutoka kwenye viwanda vyetu wakanipa mfano kuwa zamani ulkuwa uwezi kwenda wazo na kupakia cement siku hiyo hiyo kwa sababu kulikuwa na biashara na ulikuwa unapanga foleni lakini siku hizi ukifika unapakia na kubembembelezwa kwa sababu mzigo uko kiwandani akuna wanunuzi cement ya nje ndiyo inauzwa, kwa kweli inaisha sana watanzania na wanaumia sana ni swala hili ni serikali na wizara husika kuchukua taadhali mapema sana kwa sababu ukienda pale wazo unakuta vijana wamelala kwenye majani wakisubiria kazi za kufanya pale na huku kituo cha polisi kilichopo jirani kikiathilika na vumbi jembamba linalotoka kiwandani ambalo limekuwa kero kubwa sana kwao na ukifiika pale kituo cha polisi utawaonea huruma san ajinsi walivyo pauka na kujaa vumbi na kibaya zaidi wakitoka pale hata pesa ya kujinunulia maziwa hawana kwa kweli ni hatari sana,
 
Kiwanda kipya cha saruji cha Kisarawe kipo katika hatua za mwisho kuanza kuzalisha saruji
 
Luck cement ni bora sana kwenye utengenezaji wa Tofali kuliko Twiga cement. Hapa naongelea kitu ninachokifahamu, nimeachana na Twiga cement kabisa mpaka nitakapokamilisha idadi ya Tofali zangu
 
1.bora ya nje ije,viwanda vya cement hapa vinatunyonya wananchi kwa bei ya juu sana!inakuaje cement ya nje iwe bei rahisi kuliko yetu wakati materials yote inapatikana hapa hapa?
2.kiwanda cha wazo twigacement wanatumia gesi ya songas katika uzalishaji lakini bei ipo sawa na tanga na mbeya cement wanaotumia heavy fuels oil na makaa ya mawe?
3. kama cement yan nje haipo wafanyabiashara ma agent wa cement kama ilivyo sukari hufanya scarcity ya makusudi ya bidhaa hiyo ili bei ipande mtaani wapate faida kubwa
4.kwa ubora ya nje inatoa tofali mpaka 70,wakati ya bongo inatoa 40
 
Back
Top Bottom