eti neno "shushi" lilitoholewa kutoka kichina?

Mbunge wa CCM

JF-Expert Member
Nov 13, 2009
475
22
wapendwa, mi sikukuu hii ya krismass na mwaka mpya nasherehekea pamoja na rafiki yang mmoja mchina. pamoja na mambo mengine huwa ananifundisha kidogokidogo kuongea kichina, sasa juzi tukiwa katikati ya hekaheka za sikukuu, akanifundisha kuwa mapumziko yaani rest kwa kichuna huitwa "xiuxi" ukimsikia anavyotamka, ni sawa na kutamka "shushi" kwa kiswahili. mfano kusema kesho sitaenda kazini, napumzika kwa kichina unasema: "mingtian wo bu qu shang ban wo xiuxi" sasa hili likanirudisha nyuma kidogo enzi nasoma shule ya sekondari.

wakati nikiwa sekondari ya awali katika shule siyo ya bweni, nilikuwa naishi na kaka yangu aliyekuwa askari na tuliishi katika nyumba za askari maarufu kama laini au laini polisi. kama mjuavyo moja ya majukumu ya kila siku ya askari ni ulinzi. sasa kulikuwa na msemo pale laini miongoni mwa askari na wanajamii wengine wa laini kuwa siku ambazo askari hakwenda lindoni, yaani anapumzika, tulisema kuwa "anakula shushi" mfano utasikia"mimi niko shushi hadi jumatatu" akiwa na maana kuwa haende kazini (anapumzika) hadi jumatatu.

sasa waungwana na wakereketwa wote wa lugha yetu adhimu, je nini asili ya hili neno shushi. na je lina uhusiano gani (kama upo) na neno la kichina "xiuxi" linalotamkwa "shushi"?.

ufafanuzi tafadhari
 
swala zima la kichina mmh mi mwenyewe mgeni ngoja waje wenye kujua, ila kama na shushi ilitoka china basi waswahili ni malinguistic
 
Yawezekana kabisa neno "shushi" likawa la kichina kwa sababu ya uhusiano wa kihistoria ambao tumekuwa nao kwa muda mrefu katika nyanza za ulinzi, usafiri, viwanda, nk.
 
shushi ni hiyo hiyo XIUXI. Hilki lilikukuwa neno slang wakati tuko JKT, Wachina walikuwa wanasema hivyo ndiyo vijana wa JKT waaanza kulitumia; sijui kama liko mitaani siku hizi.

Kama liko lilianzia JKT.
 
...sasa waungwana na wakereketwa wote wa lugha yetu adhimu, je nini asili ya hili neno shushi. na je lina uhusiano gani (kama upo) na neno la kichina "xiuxi" linalotamkwa "shushi"?.

ufafanuzi tafadhari
Hilo neno linavyo tumika ni sawa kabisa. xiu xi maana yake ni mapumziko/kupumzika.Kwa kiingereza ni Rest/Relax
 
duuh, asili ya neno 'shushi' yawezekana kabisa ikawa hilo neno la kichina 'xiuxiu'..!! cha ajabu mimi sijakutana au sijabahatika kukutana na mtu akitumia neno 'shushi' katika mazungumzo akimaanisha mapumziko au kupumzika!!

'xiexie' kwa kichina ni sawa na 'ahsante' au 'shukrani' kwa kiswahili... je, neno 'kasheshe' limetoholewa kutoka neno 'xiexie' ....kwani nayo inatamkwa 'sheshe'?!
 
Naomba nitoe mawazo yangu kama mmoja wa watu waliojifunza Kichina kwa muda mrefu na nimekaa China kwa muda mrefu pia familia yangu ni Wachina. Kuna maneno mengi sana ya kichina yanayofanana na kiswahili. Tumeweza kuwa na mahusiano ya muda mrefu na Wachina tangu hezi za Jang He. Mfano, Yesu anaitwa hivyo hivyo kwa Kichina. (John) Yohana anaitwa Yue Han "yuehan". Mila na desturi zetu hazitofautiani sana na wachina ukiondoa kasoro ndogo ndogo zinazovumilika mfano: Wote tunajumuika pamoja wakati wa misiba, tuna extended family etc

Ninaweza kusema kuwa Neno hilo Shushi limetoka China au limetoka Tanzania kwenda China kwani tunamaingiliano ya muda mrefu sana na wachina. Tanzania na Macao (sehemu ya China) wanauhusiano wa damu hivyo kuna mambo mengi tunafanana ... kuigana n.k
 
Mie nafikiri litakuwa limetoka china na si Bongo kwenda china hasa kama na wachina walishirishi kutupa mafunzo jkt kwani hawa watu ni nadra sana kuwa na second language hasa kipindi hicho cha jkt ukichikulia ni muda mfupu uliopita tu ndo wameanza kujichanganya kwa sana.Na kama unavyowajua hawa ndugu zetu mkuu,wakiwa hawajui lugha nyingine yeye atachapa kichina chake bila ya kujali unaelewa au la.
 
Nakubaliana na wachangiaji wanaosema kua neno hili asili yake ni kichina "xiuxi". Ila napenda kuongeza kua neno hili halikutumiwa jkt tu,bali sehem nyingi ambazo wachina walikua wakifanya kazi na wazee wetu enzi hizo walipenda kulitumia sana.
Mimi niliishi ktk kampuni ambayo wachina walikua wengi pale na wazee wetu wakawa wanatumia maneno mengi sana ya kichina (utasikia leo kazi meiyou,shushi shushi! Pia walikua wakituonesha sinema za vita na kung fu. Tukienda kwenye ukumbi wa sinema tunawauliza "rafiki sinema yo?" mchina akisema yo(you) anamaanisha ipo akisema meiyou anamaanisha haipo, etc).
Vijana wa mtaani pale wote tukawa tunatumia neno shushi bila hata kujua kama kwa kichina linaandikwaje. Hivyo naamini sehem nyingi sana ambazo wachina walikuwepo(au wapo hadi sasa) wanatumia pia baadhi ya misamiat yao na jamii. Nafikiri hata wenzetu wanaokaa/kufanya kazi na watu wa nchi nyingine pia wanajua baadhi ya misamiati ya lugha hizo. Mfano wale wanaokaa au wanaofanya kazi na wahindi kuna misamiati ya kihindi mingi wanaijua na mingine imeanza kuwa ya kawaida tu mtaani.
 
Mimi nilikutana nalo RUVU JKT (Oparation Usafi) mwaka 1978 wakati tunalima Mpunga chini ya wataaamu wa Kichina walikuwa wanalitumia sana na sisii tukaiga sana kulitumia badala ya neno kupumzika
 
duuh, asili ya neno 'shushi' yawezekana kabisa ikawa hilo neno la kichina 'xiuxiu'..!! cha ajabu mimi sijakutana au sijabahatika kukutana na mtu akitumia neno 'shushi' katika mazungumzo akimaanisha mapumziko au kupumzika!!

'xiexie' kwa kichina ni sawa na 'ahsante' au 'shukrani' kwa kiswahili... je, neno 'kasheshe' limetoholewa kutoka neno 'xiexie' ....kwani nayo inatamkwa 'sheshe'?!
Ni mandarin hiyo, Nahisi hilo neno nalo tumelitohoa na imekuwa salam ya watoto kwa watu wazima. Chei chei
 
Back
Top Bottom