Eti, nani analeta Madawa ya kulevya Zanzibar?

Kwa ufupi, tusitafute mchawi ni sisi wenyewe.
Mchawi ni lazima atafutwe kwa sababu si 'sisi' sote ni wachawi. Ni baadhi miongoni mwa 'sisi' ndio wachacwi, kama ulivyoonyesha mwenyewe makundi yanayojihusisha na biashara-vyombo vya usalama, wafanyabiashara na viongozi (wa kisiasa?). Hivyo ni lazima tutafute miongoni mwetu ni nani anahusika. Tukiachia kusema mchawi ni 'sisi' tutakuwa hatujitendei haki kwa sababu si 'sisi' wote tunahusika na biashara hiyo
 
Kwani ili tatizo liko Zanzibar tu? Mbona bara ndio zaidi na mwuungwana alikabidhiwa majina ya vigogo wanaojihusisha na hayo madawa lakini amekaa kimya mpaka leo? Sijui aliambiwa asiwachukulie hatua kwa kuwa walifund kampeni za uchaguzi zilizomwingiza ikulu?

Vita dhidi ya drug trafikkers haiwezi kufanikiwa kama vyombo vya usalama na watawala hawatakuwa tayari kutoa ushirikiano unaostahili.

Tiba
 
duh!
tatizo la madawa ya kulevya ni kubwa kuliko watu wanavyofikiri aisee, loh!
si ajabu uongozi wa juu unagombewa kwa gharama yeyote makanisani na misikitini.
 
we raia ukitaka kuwataja basi wanakuuwa....wanajulikana ila hao waondoaji wa uovu huu nao wanapewa donge nono ili biashara iendelee....hili janga sio la zanzibar pekee .....ni tz yote
tuwe makini......
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom