Eti Mwakyusa hana bao 2015

Highlander,
Heshima mbele mkuu, Prof Mwakyusa kusema ni mtu wa dini hapo ni kupotosha. Yeye ni msomi mzuri na mpole. Ila siyo mwanasiasa wala mtu wa dini.Pesa chafu ilitumika kumpa ubunge kwa mara ya kwanza mwaka 2000. Na source ya hizo fedha chafu wengine tunafahamu zilipotoka...., mwamko ni mkubwa sana Rungwe nzima hata Prof. Mwandosya kakalia kuti kavu. Ndiyo Mwandosya ana jina kubwa kitaifa, lakini jimboni kwake hakuna cha maana alichokifanya. Ni kweli amesimamia ujenzi wa baadhi ya vishule vya kata ambavyo vingi havina facilities za kutosha. Jimbo zima halina hata Km moja ya barabara ya lami wakati amekuwa Waziri kwa takriban miaka 15?, uchumi umekuwa ukishuka kila mwaka, hakuna ubunifu wa kutosha ili rasilimali zilizopo ziweze kuwasaidia wana Rungwe. Rungwe kuna mlima wa volcano ambao ni wa tatu kwa urefu nchini, kuna gesi- kule mlima kyejo, maziwa, mito mingi na mikubwa, chakula tele, hali ya hewa nzuri. lakini bado wananchi ni fukara wa kutupwa.......
Nyumba nyingi zinazoonekana nzuri za bati huko Rungwe zilijengwa miaka ya 60 na 70, lakini kwa sasa vijana wanaishia kujenga nyumba za nyasi.
Angalizo kwa Chadema, tunawaomba wafanye kazi, wafanye kazi, wafanye kazi... Tuna rasilimali za kutosha kuweza kutuendeleza bila ya kutegemea wafadhili. Zitumike vizuri kwa maendeleo ya Watanzania.

Mungu Ibariki Tanzania, Amen........
Uliona mbali mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom