Eti Mwakyusa hana bao 2015

Highlander

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
3,093
1,075
Wana Jukwaa salaam. Nimetoka Tukuyu na habari mbaya. Kaka yetu, rafiki yetu mpendwa DR.Mwakyusa hana bao 2015. Mwanachadema machachari sana Mama Slaa katoa onyo hili juzi akiwa tukuyu. Naweka picha yake hapa, na samahani nimechelewa kuleta picha hii na ujumbe huu mzito kutoka CHADEMA. Eti Rungwe Magharibi itachukuliwa na CHADEMA 2015 bila shaka yoyote. Haya yamesemwa na huyu Mwanachadema machachari sana Mama Slaa. sijui jina lake Josephine Nani vile? Jamani ee, hivi Mwakyusa ana sababu ya kuondolewa bungeni kweli? Mtu mpole vile?

Kilichonifuarahisha zaidi hata hivyo ni utulivu wa wana ccm pale tukuyu wakati wa mkutano huo. Mkutano ulifanyika kwenye uwanja uliopo makao makuu ya CCM wilaya ya Rungwe, lakini ulifanyika kwa amani na utulivu mkubwa sana pamoja na Huyu mwanasiasa hahiri kurusha vijembe vingi kuichoma ccm uwanjani pao, akisema CCM wauaji wakubwa hawatufai kabisa. Haya mada hiyo hapo. Mwakyusa tumng'oe? tumwache. Mi nadiriki kusema siyo mwizi, siyo muuaji. Mama Slaa alimpamba sana mpenzi wake Dr. Slaa kwenye mkutano huu na kuahidi kumleta huyu Mpinzani mkubwa wa Kikwete hapo Tukuyu kabla ya Julai. Dr. Mwakyusa upo? Taarifa nyingine zimesema Chadema na CCM wanaishi kidugu sana pale Tukuyu.

Tukuyu 1.jpg Josephine 2.jpg
 
Mama slaa? ndio nani?

Huo utulivu ni ujumbe na ishara kuwa CCM hawana fujo na wakomavu kisiasa,

We unafikili ingekuwa Kwenye ngome za CDM si matusi, kejeli, fujo vingetawala?

Jifunzeni sasa!
 
Nimemwita Mama Slaa kwa sababu ndio jina alikuwa anaitwa pale Tukuyu. Lakini pia inajulikana huyu mwanasiasa ni mpenzi wa Dr. Slaa Anaitwa Josephine sijui nani...jina lake la pili limenitoka
 
Nafahamu siasa za Tukuyu (Rungwe magharibi), namfahamu sana Prof. Mwakyusa. Kama unakumbuka uchaguzi wa mwaka 2010 ndani ya CCM, Prof alikabwa koo sana na Bw Richard Kasesera, alishinda kwa kura chache sana. Kwa sasa Prof hana mvuto sana kwa wana Rungwe. Ndani ya CCM Richard alionekana kung'ara kuliko Prof. Ila kwa sasa naye Richard Kasesera hana nguvu kabisa. ( Uchaguzi wa Udiwani kata ya Kiwila) ambako ndiyo nyumbani kwa Kasesera, naye alipiga kambi kuhakikisha CCM inashindwa lakini hakufua dafu mbele ya Chadema.
Kwa maoni yangu ni dhahiri CCM mwaka 2015 hawatakuwa na uwezo wa kukabiliana na CDM huko Rungwe magharibi kutokana na mwamko mkubwa wananchi wa Rungwe walionao.
Nawasilisha!!!!!!!!!!!!!!!!
 
We Suzana. Si taarifa tu jamani! Kwani kuna ubaya gani nikikupeni habari wanajukwaa....
 
Nafahamu siasa za Tukuyu (Rungwe magharibi), namfahamu sana Prof. Mwakyusa. Kama unakumbuka uchaguzi wa mwaka 2010 ndani ya CCM, Prof alikabwa koo sana na Bw Richard Kasesera, alishinda kwa kura chache sana. Kwa sasa Prof hana mvuto sana kwa wana Rungwe. Ndani ya CCM Richard alionekana kung'ara kuliko Prof. Ila kwa sasa naye Richard Kasesera hana nguvu kabisa. ( Uchaguzi wa Udiwani kata ya Kiwila) ambako ndiyo nyumbani kwa Kasesera, naye alipiga kambi kuhakikisha CCM inashindwa lakini hakufua dafu mbele ya Chadema.
Kwa maoni yangu ni dhahiri CCM mwaka 2015 hawatakuwa na uwezo wa kukabiliana na CDM huko Rungwe magharibi kutokana na mwamko mkubwa wananchi wa Rungwe walionao.
Nawasilisha!!!!!!!!!!!!!!!!

Nadhani unasema ukweli. Prof Mwakyusa anaonekama kuwa mtu wa dini sana, na kuwa mtu mwadilifu sana. Lakini hilo pia halimsaidii katika medani ya siasa. Kwa hiyo inaelekea anakosa mvuto si kwa sababu ya tuhuma za ufisadi walio nao wenzake, lakini kwa sababu nadhani kutokuwa mwanasiasa. Chadema watachukua Rungwe Magharibi kirahisi sana 2015 nadhani, lakini haitakuwa kura ya chuki kwa mtu, bali kwa kundi analotoka.
 
Mchango wake kwa wananchi wajimbo lake ndio utakao mwacha 2015 kama hamna piga teke kule gamba hili
 
Mama slaa? ndio nani?

Huo utulivu ni ujumbe na ishara kuwa CCM hawana fujo na wakomavu kisiasa,

We unafikili ingekuwa Kwenye ngome za CDM si matusi, kejeli, fujo vingetawala?

Jifunzeni sasa!
:focus:BACK TO TOPIC UNASIFIA NINI CCM BANA TUONE 2015 MCHANGO WAKE KWA WANA RUNGWE NDO ATABAKI AU LA
 
Mama slaa? ndio nani?

Huo utulivu ni ujumbe na ishara kuwa CCM hawana fujo na wakomavu kisiasa,

We unafikili ingekuwa Kwenye ngome za CDM si matusi, kejeli, fujo vingetawala?

Jifunzeni sasa!

Rudi nyuma halafu ndio upost comments zako mkuu, kawaida watu wa Mbeya hasahasa wilayani Rungwe huwa hawana shida na mtu mpaka pale utapowanyanyasa au kutoa kejeli.
 
mleta mada kuna mahali uesema jamaa mwakysa sio mwizi, sio muuaji na mpole......hapo kwenye sio muuaji hapo paangalie sana...huyu jamaa wakati ni dr wa mwl aliwahi kususia kwenda butiama kumtibu mwl hadi akaitwa daktari mwingine kutoka bugando.....we fatilia tu kwa nini familia ilimpiga marufuku kumgusa mwl alipokuwa london..huyu na Ben mkapa wana siri nzito sana juu ya kifo cha mwl...
 
Unapokuwa kwenye mapambano unahakikisha kwamba No stone will be left unturned,so long Prof ni CCM ,he ought to go otherwise hamame mabondeni ahamie CDM.
Wana Jukwaa salaam. Nimetoka Tukuyu na habari mbaya. Kaka yetu, rafiki yetu mpendwa DR.Mwakyusa hana bao 2015. Mwanachadema machachari sana Mama Slaa katoa onyo hili juzi akiwa tukuyu. Naweka picha yake hapa, na samahani nimechelewa kuleta picha hii na ujumbe huu mzito kutoka CHADEMA. Eti Rungwe Magharibi itachukuliwa na CHADEMA 2015 bila shaka yoyote. Haya yamesemwa na huyu Mwanachadema machachari sana Mama Slaa. sijui jina lake Josephine Nani vile? Jamani ee, hivi Mwakyusa ana sababu ya kuondolewa bungeni kweli? Mtu mpole vile?

Kilichonifuarahisha zaidi hata hivyo ni utulivu wa wana ccm pale tukuyu wakati wa mkutano huo. Mkutano ulifanyika kwenye uwanja uliopo makao makuu ya CCM wilaya ya Rungwe, lakini ulifanyika kwa amani na utulivu mkubwa sana pamoja na Huyu mwanasiasa hahiri kurusha vijembe vingi kuichoma ccm uwanjani pao, akisema CCM wauaji wakubwa hawatufai kabisa. Haya mada hiyo hapo. Mwakyusa tumng'oe? tumwache. Mi nadiriki kusema siyo mwizi, siyo muuaji. Mama Slaa alimpamba sana mpenzi wake Dr. Slaa kwenye mkutano huu na kuahidi kumleta huyu Mpinzani mkubwa wa Kikwete hapo Tukuyu kabla ya Julai. Dr. Mwakyusa upo? Taarifa nyingine zimesema Chadema na CCM wanaishi kidugu sana pale Tukuyu.

View attachment 54970View attachment 54971
 
Siyo mama slaa wewe.Hujui mama yake ni yule aliye mzaa na atakuwa na umri mkubwa sana sema huyo sukuma siku wa slaa.Acha kuchafua jina la mama.
 
Nadhani unasema ukweli. Prof Mwakyusa anaonekama kuwa mtu wa dini sana, na kuwa mtu mwadilifu sana. Lakini hilo pia halimsaidii katika medani ya siasa. Kwa hiyo inaelekea anakosa mvuto si kwa sababu ya tuhuma za ufisadi walio nao wenzake, lakini kwa sababu nadhani kutokuwa mwanasiasa. Chadema watachukua Rungwe Magharibi kirahisi sana 2015 nadhani, lakini haitakuwa kura ya chuki kwa mtu, bali kwa kundi analotoka.
Highlander,
Heshima mbele mkuu, Prof Mwakyusa kusema ni mtu wa dini hapo ni kupotosha. Yeye ni msomi mzuri na mpole. Ila siyo mwanasiasa wala mtu wa dini.Pesa chafu ilitumika kumpa ubunge kwa mara ya kwanza mwaka 2000. Na source ya hizo fedha chafu wengine tunafahamu zilipotoka...., mwamko ni mkubwa sana Rungwe nzima hata Prof. Mwandosya kakalia kuti kavu. Ndiyo Mwandosya ana jina kubwa kitaifa, lakini jimboni kwake hakuna cha maana alichokifanya. Ni kweli amesimamia ujenzi wa baadhi ya vishule vya kata ambavyo vingi havina facilities za kutosha. Jimbo zima halina hata Km moja ya barabara ya lami wakati amekuwa Waziri kwa takriban miaka 15?, uchumi umekuwa ukishuka kila mwaka, hakuna ubunifu wa kutosha ili rasilimali zilizopo ziweze kuwasaidia wana Rungwe. Rungwe kuna mlima wa volcano ambao ni wa tatu kwa urefu nchini, kuna gesi- kule mlima kyejo, maziwa, mito mingi na mikubwa, chakula tele, hali ya hewa nzuri. lakini bado wananchi ni fukara wa kutupwa.......
Nyumba nyingi zinazoonekana nzuri za bati huko Rungwe zilijengwa miaka ya 60 na 70, lakini kwa sasa vijana wanaishia kujenga nyumba za nyasi.
Angalizo kwa Chadema, tunawaomba wafanye kazi, wafanye kazi, wafanye kazi... Tuna rasilimali za kutosha kuweza kutuendeleza bila ya kutegemea wafadhili. Zitumike vizuri kwa maendeleo ya Watanzania.

Mungu Ibariki Tanzania, Amen........
 
mleta mada kuna mahali uesema jamaa mwakysa sio mwizi, sio muuaji na mpole......hapo kwenye sio muuaji hapo paangalie sana...huyu jamaa wakati ni dr wa mwl aliwahi kususia kwenda butiama kumtibu mwl hadi akaitwa daktari mwingine kutoka bugando.....we fatilia tu kwa nini familia ilimpiga marufuku kumgusa mwl alipokuwa london..huyu na Ben mkapa wana siri nzito sana juu ya kifo cha mwl...

Ndugu De,

nashindwa kusema mengi hapa kwa sababu maneno haya kuhusu Mwakyusa na Mkapa ni hisia zaidi kuliko ukweli. Nilipata bahati ya kuzungumza na ndugu yake Nyerere ambaye siyo mwanasiasa mwaka jana kabla ya kampeni za Arumeru, na yeye alisema Nyerere alikuwa mgonjwa kwa muda mrefu kidogo. Hoja ya njama za kumuua nyerere zinaonekana kama hisia zaidi kuliko fact. Lakini pia Mwakyusa anaonekana kupendwa sana na familia ya Nyerere kwa kadri ninavyojua mimi. Kwa hiyo kama kuna hisia za njama za kumuua nyerere, labda abaki nazo Mkapa lakini siyo Mwakyusa. Again nadhani ni hisia zaidi kuliko fact.
 
Duh kazi kwelikweli
 
Highlander,
Heshima mbele mkuu, Prof Mwakyusa kusema ni mtu wa dini hapo ni kupotosha. Yeye ni msomi mzuri na mpole. Ila siyo mwanasiasa wala mtu wa dini.Pesa chafu ilitumika kumpa ubunge kwa mara ya kwanza mwaka 2000. Na source ya hizo fedha chafu wengine tunafahamu zilipotoka...., mwamko ni mkubwa sana Rungwe nzima hata Prof. Mwandosya kakalia kuti kavu. Ndiyo Mwandosya ana jina kubwa kitaifa, lakini jimboni kwake hakuna cha maana alichokifanya. Ni kweli amesimamia ujenzi wa baadhi ya vishule vya kata ambavyo vingi havina facilities za kutosha. Jimbo zima halina hata Km moja ya barabara ya lami wakati amekuwa Waziri kwa takriban miaka 15?, uchumi umekuwa ukishuka kila mwaka, hakuna ubunifu wa kutosha ili rasilimali zilizopo ziweze kuwasaidia wana Rungwe. Rungwe kuna mlima wa volcano ambao ni wa tatu kwa urefu nchini, kuna gesi- kule mlima kyejo, maziwa, mito mingi na mikubwa, chakula tele, hali ya hewa nzuri. lakini bado wananchi ni fukara wa kutupwa.......
Nyumba nyingi zinazoonekana nzuri za bati huko Rungwe zilijengwa miaka ya 60 na 70, lakini kwa sasa vijana wanaishia kujenga nyumba za nyasi.
Angalizo kwa Chadema, tunawaomba wafanye kazi, wafanye kazi, wafanye kazi... Tuna rasilimali za kutosha kuweza kutuendeleza bila ya kutegemea wafadhili. Zitumike vizuri kwa maendeleo ya Watanzania.

Mungu Ibariki Tanzania, Amen........

Amina. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Wilaya ya Rungwe. Umesahau kitu kidogo. Mwandosya kafikisha umeme kijiji cha Kisegese ndugu yangu--hata kama umeme huo haujapata watumiaji wa kutosha pale kuleta faida kwa Tanesco. Ila kipengele hiki sina hakika kama ni sahihi sana. lakini kwa sasa vijana wanaishia kujenga nyumba za nyasi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom