Eti mtoto hapumui tumboni

Z kama Z

Member
Jul 6, 2011
60
10
Wana JF hivi inawezekana kweli kuwa mtoto hapumui akiwa tumboni na mama yuko normal tu, au sometime manesi wanakuwa wamechoka kupima tu,
Hii inakuwaje embu nipeni mawazo yenu.
 
Hamishia jukwaa la JF Doctor...utapata majibu sawia kwani kule kuna madaktari pia.
 
Wana JF hivi inawezekana kweli kuwa mtoto hapumui akiwa tumboni na mama yuko normal tu, au sometime manesi wanakuwa wamechoka kupima tu,
Hii inakuwaje embu nipeni mawazo yenu.

Mtoto huwa hapumui akiwa tumboni mwa mama yake...mimba inapotunga katika maendeleo ya mwanzoni kabisa ni kutengeneza chupa ya uzazi au 'amniotic sac' (ile kwa kawaida inapasukaga wakati wa kuzaa halafu maji yanamwagika), ambayo ni kama mfuko fulani hivi ambamo ndani kunakuwa na majimaji (amniotic fluid)...mtoto anakuwa ndani ya maji hayo, hivyo hawezi kupumua kama ambavyo mtu mzima hawezi kupumua akiwa ndani ya bahari au swimming pool!

Mtoto anakuwa anapata kila atakacho kutoka kwa mama yake kupitia placenta na kitovu (umbilical cord). Kitu ambacho wahudumu wa afya wanapima kwa kusikiliza na kila chombo kama pia hivi kinaitwa 'fetoscope' ni mapigo ya moyo ya mtoto, na vile mtoto kucheza (fetal quickening). Kama mtoto hachezi na mapigo ya moyo hayasikiki, then hiyo ni emergency inayohitaji hatua za haraka kujua kama mtoto yu hai au la.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom