LD
JF-Expert Member
- Aug 19, 2010
- 3,014
- 574
bado...
Orait Seto, kama wengine walivotangulia kusema hili ni swala la kiimani zaidi, kutegemeana na jinsi wewe unavyoamini na unavyomwamini Mungu wako. Haijalishi watu fulani wanafundisha nini si kazi yetu kohoji hilo, haijalishi wanasema uombe kwa jinsi ipi hio ni imani yao
Swala hapa wewe unataka mke wa jinsi gani na unaamini nini katika hilo, Je unaamini Mungu anaweza kukupa hitaji la moyo wako??
Kutoka na mimi ninavyoamini, Mungu anakupa mume/mke mwema kwa wakati sahihi. Na sio lazima ukutane nae kanisani au msikitini. Unaweza ukakutana nae baa, anaweza kuwa changudoa, anaweza kuwa jambazi, anaweza kuwa ktk mazingira mabaya sana lakini wakati wa Mungu ukifika anamtoa huko, anamleta kwako.
Mke mwema/mume mwema ni yule ambaye utaishi nae kwa furaha na amani. Mnaweza kuchukuliana madhaifu yenu, kushirikiana nae na nafsi yako ina uhuru nae.