Eti mi mchoyo

Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
5,649
Huyu mmama ni jirani yangu wa muda mrefu sana,zaidi ya miaka mitano sasa, kwa kipindi chote hicho uhusiano wangu na yeye zaidi ya ujirani umekuwa ni salamu tu. Mwanzoni mwa mwezi huu nyumbani kwa jirani yetu mwingine imefunguliwa glocery hivo imekuwa kawaida yangu kwenda pale ama kupiga fundo la mwisho kabla sijaingia home, au kuuweka kabisa na kutandika castle rites zangu za baridi.

Glocery hii ndio imesababisha mimi na huyu mama kuwa karibu zaidi, sababu mara nyingi tunakutano hapo, karibia kila siku nikienda lazima nimkute anakula bata au yeye atanikuta, na kama kawaida tumekuwa tunasalimiana tu na mpaka sasa haijatokea tukakaa japo meza moja, sasa recently kaanza kunitupia shutma kwamba mimi mchoyo mimi mchoyo, nikafiriki anataka bia, juzi nimemkuta nikamsalimia alipomaliza kuitikia akaniambia lakini nipunguze uchoyo, nikamtupia bia mbili, jana nikamkuta tena akarudia hiyo kauli nikamuambia mi sio mchoyo sema serikali ya jakaya imeharibu uchumi akanambia namsingizia, nikajitoa muhanga nikamuambia basi ye anywe tu bill ntalipa mimi, jana tena nimekutana nae karudia kauli ile ile, as if sijamuonyesha uungwana na utoaji wangu hata mara moja.

Kuna mshikaji niliyekuwa naye nilimueleza hii kitu katika kujustify kumlipia bill yule mama, akacheka na kuniambia kweli nimebadirika. ndo nikafunguka, hivi inawezakana kweli huyu mama akawa anamaanisha namnyima mambo yenu yaleeee.

Kilichojiri
Jana huyu Mama kanipigia simu, alipopata number yangu sijui ananiomba faragha ya maongezi weekend nje kabisa ya wilaya ya kinondoni, na kwamba amenipigia mapema ili niweze kujiandaa na hiyo ratiba bila kukosa. Yaani alikuwa ananieleza as if she is mke wangu bila kuuma uma maneno. Nikamkubalia, najipanga jinsi ya kupangua na hii.
 
wee nae ulishatoa bia nne zinatosha...sasa ni wakati wa huyo mama kuzilipia kwa kukupa wewe utamu
 
sioni sababu ya kuwa unamnunulia nunulia huyo mama bia! eti kisa anakwambia mchoyo :loco:
 
Mfuate umuulize ukituuliza sisi unakosea ndugu..pengine unapika mboga nzuri nyumban,haumkaribishi je..
 
Kesto niniii.., okay en'wei ukiamka asubuh mtafute umulize,kabla hamjanywa wote. Hakika hutakosa jibu.
 
Huyu mmama ni jirani yangu wa muda mrefu sana,zaidi ya miaka mitano sasa, kwa kipindi chote hicho uhusiano wangu na yeye zaidi ya ujirani umekuwa ni salamu tu. Mwanzoni mwa mwezi huu nyumbani kwa jirani yetu mwingine imefunguliwa glocery hivo imekuwa kawaida yangu kwenda pale ama kupiga fundo la mwisho kabla sijaingia home, au kuuweka kabisa na kutandika castle rites zangu za baridi.

Glocery hii ndio imesababisha mimi na huyu mama kuwa karibu zaidi, sababu mara nyingi tunakutano hapo, karibia kila siku nikienda lazima nimkute anakula bata au yeye atanikuta, na kama kawaida tumekuwa tunasalimiana tu na mpaka sasa haijatokea tukakaa japo meza moja, sasa recently kaanza kunitupia shutma kwamba mimi mchoyo mimi mchoyo, nikafiriki anataka bia, juzi nimemkuta nikamsalimia alipomaliza kuitikia akaniambia lakini nipunguze uchoyo, nikamtupia bia mbili, jana nikamkuta tena akarudia hiyo kauli nikamuambia mi sio mchoyo sema serikali ya jakaya imeharibu uchumi akanambia namsingizia, nikajitoa muhanga nikamuambia basi ye anywe tu bill ntalipa mimi, jana tena nimekutana nae karudia kauli ile ile, as if sijamuonyesha uungwana na utoaji wangu hata mara moja.

Kuna mshikaji niliyekuwa naye nilimueleza hii kitu katika kujustify kumlipia bill yule mama, akacheka na kuniambia kweli nimebadirika. ndo nikafunguka, hivi inawezakana kweli huyu mama akawa anamaanisha namnyima mambo yenu yaleeee

Sasa ndugu yangu wewe huyo mama mtu mzima unahangaika naye wa nini? Alishasema wewe mchoyo na umejitahidi kumuonyesha kuwa si mchoyo kwa kumnunulia bia na kulipia bili zake, na still bado haridhiki na jitihada zako, huna shughuli nyingine za kufanya? Jiangalie mdogo wangu asije kuwa ni kweli ana maanisha mambo mengine na kujikuta unajitupia kwa huyo mama na kuharibu mahusiano uliyonayo na mtu umependaye kwa sasa. Wamama wa namna hii wakishakunasa wanakuwaga ving'ang'anizi sana ...
Kama upo single na huna mahusiano na wadada wa umri wako, nakuruhusu, go ahead at your own risk!
 
tayari sangara kikaangoni tayari kwa kukamuliwa ndimu na chumvi tumtafune.

Yaani kakupara magamba kirahisi hivi Sangarara??
 
Last edited by a moderator:
Unatafuta kuhalalishiwa ujinga huna jingine.

Chauro, mi nimeshare hii hapa baada ya mtu kuniuma sikio kwamba likely huyo mama anaelekea wapi, lakini kwa swala la kutaka kuhalalishiwa sio kweli,
 
hahaha! Nimecheka hadi raha... eti mambo yenu yale.. Wewe Sangarara wewe sio yako? au mwenzetu upo ki kanisa zaidi? BTW ndio nini kumbania mama wa watu? hebu acha uchoyo bana! lol

Samahani mimi naomba tu nitume salamu kwa HorsePower, Swts, WiseLady, mzabzab na Chauro nawasalimu with Love...

Sio kikanisa tu, niko married hivyo nilikuwa na refer kwa wale visiting professors? kimsingi kama ni kweli analalamikia hilo atachemsha.
 
ndugu,

ishi vile uwezavyo na si watu watakavyo......

Huyo mama yeye sio mchoyo? Keshakununulia beer?

Mzaha mzaha utaishia kitandani kwa mmama...

Shauriyako........
 
huyo mama anataka nini zaidi? Mkuu sikia kengele tulia na wako maana sijaelewa hata huyo mama mazingira anayoishi kifamilia yako vipo ameolewa au ndio ile mijimama ya mjini?
 
hahaha! Nimecheka hadi raha... eti mambo yenu yale.. Wewe Sangarara wewe sio yako? au mwenzetu upo ki kanisa zaidi? BTW ndio nini kumbania mama wa watu? hebu acha uchoyo bana! lol

Samahani mimi naomba tu nitume salamu kwa HorsePower, Swts, WiseLady, mzabzab na Chauro nawasalimu with Love...

Ashadii, senki yu swit,hakika we si mchoyo "wa salamu", lol!
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom