Amoeba
JF-Expert Member
- Aug 20, 2009
- 3,289
- 781
Hii kitu mi nadhani ni kweli kabisaa, Binafsi nilikuwa mbishi sana kuhusiana na hili, Wife alivojifungua aliambiwa na mama yake tusiguse hii kitu mpaka angalau "miezi sita!", mtoto alizaliwa na afya nzuri sana, na kila mwezi aliongezeka kilo 2 au 1.5! grafu ilikuwa inaenda juu tu, mwezi wa tatu toka kuzaliwa nikaingiza mambo yangu ya shule na vitabu kibao vya refference! nikampiga somo la biology wife mpaka akaona ni kweli, tena tukaridhishana kabisaa kwamba hizi myth za kizamani hazina issue! Mama akapata dawa za uzazi wa mpango, tukacheza gemu siku moja usiku......! Kesho yake mtoto akanyonya kama kawaida, tukashinda na kulala bila noma, next day asbh ndy balaa tuliliona! Mtoto anakunya mavi yasiyoeleweka (yana vitu kama maziwa na harufu isiyo ya kawaida!), Ndani ya siku nne mtoto akawa amepungua uzito balaa! Kumpeleka kwenye vipimo vinasoma negative kila kitu, Wife akaenda kwa maza, akampa stori-maza akamtafutia dawa ya kienyeji!!!!! Mtoto amekunya ile dawa siku mbili tu na kurudia Afya yake ya Kawaida, sasa hivi tumekoma tunasubiria miezi sita ndy Tuanze mambo yetu.
Kifupi ni kwamba baadhi ya mambo na imani za kienyeji si za kubeza! Ukitaka UNAWEZA KUJARIBU. BINAFSI NIMEKOMA KUFANYIA MAJARIBIO KWA MWANANGU MPENZI.
Kifupi ni kwamba baadhi ya mambo na imani za kienyeji si za kubeza! Ukitaka UNAWEZA KUJARIBU. BINAFSI NIMEKOMA KUFANYIA MAJARIBIO KWA MWANANGU MPENZI.