Eti mapenzi ya kweli yanakuja na kuondoka kwa nyakati tofauti?

Ngekewa

JF-Expert Member
Jul 8, 2008
7,705
1,288
Jirani yangu alinikabili na kuniuliza!
Ilibidi nimuulize imekuwaje tena?
"Kuna wakati mke wangu ananipenda nami huwa najuwa hasa kama ananipenda lakini wakati mwengine huwa hanithamini hadi hudiriki kutaka kuachana nae", alinijibu "Hivyo kweli ana mapenzi ya kweli huyu?", aliendelea kuniuliza.
Nimjibu nini na hiyo ni ndowa, nilitamka neno moja tu "Mhn" nikaubana.
Nilibaki na mawanzo na kujiuliza eti kweli hii inawezekana na kama inawezekana nini suluhisho?
 
Maudhi yanakuja na kuondoka lkn kwa kuwa kuna mapenzi ndio maana wako pamoja!

Mtoto na mama wanaudhiana ingawa mapenzi yapo; binadamu na Muumba wake 'huudhiana' ingawa mapenzi yapo.

Note:
Maudhi yakizidi huathiri mapenzi!
 
Kuna mambo mengi yanayosababisha ndoa/mahusiano iwe na maudhi lakini haifi.Sidhani kama ni mapenzi,lazima mmoja atakua ana matatizo au wote.Kuna maudhi ambayo ni vigumu sana kuyavumilia,lakini mpaka mtu anapata wazo la kuachana,jua hapo maudhi yapo ya kutosha.Hao hawajitoshi na hawaamini kua bila ndoa kuna maisha.Wanaamini ndoa ndo utu na ndo ukamilifu,ndo maana wanailinda ndoa kwa gharama yoyote ile!
 
Inategemea na dhamira ya mtu kama alimpenda mtu baada ya kusikia sifa zake ama kumtamani kwanza na baadae akahisi kuwa anampenda kumbe siyo
 
Mtu asikudanganye kama yanakuwa same levele from day one. Labda mwanzoni yatakuwa hivyo lakini later ni mazoea na zaidi saa nyingine inaweza kuwa hata libido hakuna mnaishi kama dada na kaka.

Its cycle, which need to be revive every time it hits you.
 
Jirani yangu alinikabili na kuniuliza!
Ilibidi nimuulize imekuwaje tena?
"Kuna wakati mke wangu ananipenda nami huwa najuwa hasa kama ananipenda lakini wakati mwengine huwa hanithamini hadi hudiriki kutaka kuachana nae", alinijibu "Hivyo kweli ana mapenzi ya kweli huyu?", aliendelea kuniuliza.
Nimjibu nini na hiyo ni ndowa, nilitamka neno moja tu "Mhn" nikaubana.
Nilibaki na mawanzo na kujiuliza eti kweli hii inawezekana na kama inawezekana nini suluhisho?

Mapenzi huwa hayaji na kuondoka, yakija yamekuja ila tamaa inaweza kuja na kuondoka, ugomvi huja na kuondoka, hasira vile vile na mengi yafananayo na hayo.

Cha msingi ni kumshauri huyo mwenzio ufanye uchunguzi ktk hizo nyakati wakati mkewe huwa anamuonyesha mapenzi sana na kitu gani huwa anamfanyia mkewe ambacho humuongezea furaha au mazingira gani au tabia gani anapozibadili humuongezea mkewe furaha ili aweza kujua ni kitu gani mwenzie anapenda na kipi huwa kinamkera na kumsababishia ugomvi usio wa lazima.

Akifanikiwa kuyabaini hayo ujue kuwa atakuwa amepiga hatua kubwa ya kuondoka na tatizo la mapenzi kuja na kuondoka, loh!
 
Maudhi yanakuja na kuondoka lkn kwa kuwa kuna mapenzi ndio maana wako pamoja!

Mtoto na mama wanaudhiana ingawa mapenzi yapo; binadamu na Muumba wake 'huudhiana' ingawa mapenzi yapo.

Note:
Maudhi yakizidi huathiri mapenzi!

Ina maana mapenzi hayo ni kama malaria? Huja na kuondoka kulingana na wakati au maradhi ya kansa yanayozimika kwa dawa na dawa ikisha maumivu kuendelea?
 
Kuna mambo mengi yanayosababisha ndoa/mahusiano iwe na maudhi lakini haifi.Sidhani kama ni mapenzi,lazima mmoja atakua ana matatizo au wote.Kuna maudhi ambayo ni vigumu sana kuyavumilia,lakini mpaka mtu anapata wazo la kuachana,jua hapo maudhi yapo ya kutosha.Hao hawajitoshi na hawaamini kua bila ndoa kuna maisha.Wanaamini ndoa ndo utu na ndo ukamilifu,ndo maana wanailinda ndoa kwa gharama yoyote ile!

Sasa labda tusome mume ndie mwenye matatizo yanayomfanya mke apoteze mapenzi baadhi ya wakati?
 
Mtu asikudanganye kama yanakuwa same levele from day one. Labda mwanzoni yatakuwa hivyo lakini later ni mazoea na zaidi saa nyingine inaweza kuwa hata libido hakuna mnaishi kama dada na kaka.

Its cycle, which need to be revive every time it hits you.

MadameX mimi nafikiri kuwa hawa watu wana mapenzi lakini mume anashindwa kujuwa kuwa kuwepo mapenzi hakuna maana kuwa mtu hatokereka na jambo fulani. Hata mtoto wako kipenzi utamfutukia na kumkimbia kwa muda atakapokufanyia maudhi.
 
Back
Top Bottom