Eti maisha ya seminarini yameniharibu...

mimi nimesoma seminari....olevel na A'level nimesoma kule na nilipomaliza nikaenda malezi mwaka mmoja nikamaliza nikaenda seminari kuu nikakaa miaka 2....baada ya kutafakari wito wangu na kuisikiliza sauti ya Mungu toka ndani ya nafsi nikagundua kuwa kule si mahala pangu....nikarudi kwa baba askofu na kipande cha barua nilichooandika kwa kilatini...sehemu ya barua ile ilisema ..Multi vo calte pauce electe....(waitwao ni wengi wateule ni wachache) askofu akanipa baraka na akanishuru japo alishangaa sana kwa uamzi wangu ule...
nikarudi mtaani na nikaomba chuo nikaenda kupiga shule na nimemaliza na sasa namalizia kadigriii ka pili ....ni kweli maisha ya mtaani ni tofauti sana na haya ya seminari hasa linapokuja swala la hawa jinsi ya kike ila inategemea na malezi na mafundisho kwa ujumla.wale ni watu wa kawaida na hupaswi kuogopa mseminari unaogopa mtoto wa kike?!! kwa nini na kwa vipi?? ....lakini inategemeana na wewe jinsi unavyohandle mambo mdogo wangu....waseminari wengi wanapotea sana kwa njia hii mara warudipo uraiani...wewe una social phobia na agora phobia...jaribu kuachana na tabia hiizi ..kuwa mtu wa kawaida nawe utaishi kwa amani....

mimi kaka yako sasa hivi namtumikia Mungu kwa njia hii niliyo nayo sasa nMungu ananibariki ningejifanya mjanja na mnafiki nikakaa seminarini halafu nikalihilikisha kanisa dhambi ingekuwa kubwa sana.....anyway mungu hufinyanga mtu kadri awezavyo yeye nawe atakufinyanga awezavyo kikubwa usiufanye mgumu moyo wako bwana mdogo
 
We dogo rudi zako ukawe padri tu,haya mambo ya kitaani tuachie sie akina senetor tulioshindikana tangu tukiwa nursery school.
 
dogo mi nakushauri usianze hayo mambo,najua unatamani sana kuyaanza lakini madhara yake ni makubwa,sisi wenzio tumepitia huko seminari na hayo mambo tulikuwa tukiyafanya lakini hayana maana sana zaidi ya kukupeleka kubaya,unaweza ukajiona umempata mtu wa kuwa naye kumbe mwenzio alishashindikana na matokeo yake ukaishia kuukwaa,piga moyo konde soma kwanza.
 
hii itakuwa ni laana.
mkuu wewe hufai kuwa padre na nijuavyo seminary wakigundua tabia yako hii watakufukuza ninyi ndo huwa mnaalibu wake zetu haufai kabisa ni bora uoe mkuu kama nilivyokushauli jiunge hata kwaya ujitwalie wako mkuu umpendaye!
 
Seminarini kwenyewe ni disaster bora uraiani. David Cameron anaelewa vizuri anavyotushinikiza kuhusu mambo yale. Unafiki mtupu.
 
Ambao hata siwafahamu.......:shock:
Dogo,you need to man yourself up!It seems you have no idea of what
you wanna deal with!Tena nahisi hujawahi 'do'!Kama ndio hivyo,usiende kwa pupa,soma kwanza,jifunze taratibu.Huo ni uoga tu kwamba utajibiwa vibaya ukiongea nao.Mbona ukipotea njia sehemu unaweza kuulizia maelekezo bila woga toka kwa female yeyote!?!TATIZO UNAJISHTUKIA,HUTOWEZA KUHUDUMIA KONDOO VIZURI UKIWA FATHER KAMA SASA UNAWAOGOPA!Belivdat
 
Heshima wakuu

Nimeishi miaka saba seminarini tangu nilipoanza pre-form one hadi nilipomaliza form six mwaka juzi. Tangu nimemaliza na kurudi rasmi mtaani nimekuwa na wakati mgumu wa kuzoeana na hawa wenzetu wa jinsia ya kike. Nimekuwa sijiamini ninapokuwa mbele ya mabinti, na nimejaribu kuomba ushauri kwa rafiki zangu ambao wamezoea maisha ya mtaani lakini wanaishia kunisanifu kuwa mambo ya mtaani niwaachie wao kwani siyawezi eti kwa sababu seminari imeniharibu, na kuwa ni bora nikarudi huko.
Naombeni ushauri wa namna ya kuweza kujiamini nami nijichanganye mtaani...

Kaeso,

nakushauri nenda kwa ushauri nasaha. utapata ufumbuzi. ninawasiwasi hapa utapata majibu mengi, yatakuchangaya. kama unamfahamu sociologist anaweza kukusaidia. kwa urahisi ni kuwa maafisa ustawi wa jamii wanajua mambo haya. kama unae Padri unamfahamu anaweza kukushauri, ninaamini wanajua mambo haya.

tatizo lako kwa mtu mwingine kulitsikia anaweza kusema siyo kubwa, lakini kwako linaonekana ni kubwa. ni kama tu lingekuwa kwangu wewe ungeona dogo, ila mimi mwenyewe ningeona kubwa , ndo maana nasema hapa utapata majibu mengi , kwakuwa watu wanajua ugonjwa ni ule mtu anaumwa na hata analala. kitandania
 
Ushatamani ya kidunia wewe, bado mdogo soma kwanza utazoea tu polepolae ucwe na haraka.
 
Inavyoonyesha bado upo shule. Umri wako bado ni mdogo.

Kipi kinakushawishi utamani kujichanganya na hawa viumbe wa ke!. Kama lengo lako ni kwaajili ya ku-socialise nakutakia kila la kheri, ila kama ni kwa ajili ya kujionyesha kuwa na we ni kudume, nakusihi ufute hayo mawazo.

Mshukuru mungu kwa kukuweka huo upande. Usijaribu kutamani kuhamia upande wa shetani. Huko ni kubaya kutakufanya umsahau mungu, utajiweka karibu na mabalaa.

Mshukuru mungu amekukinga na hili janga la mapenzi. Usitamani kujitwisha mizigo isiyo na faida.

Hicho kitu chako kipo, na kitaendelea kuwepo. We soma kwanza. Kuna ambaye yupo kwa ajili yako. Muda ukifika utampata. Nawe utafurahia.

Futa dhana ya kuharibiwa na seminari. Bali imekujenga.
 
Hilo tatizo ni lako, nina marafiki wengi waseminari na hata walioacha seminari, hawana tatizo hilo, tena ni mahodari sana wa kupenda hao wasichana na kuongea nao, tatizo lao kubwa labda ni katika kutafuta mzichana ambaye ni "Perfect" kuwa na mawivu sana na kuogopa sana kudanganywa, lakini kuwaogopa halipo, wana tabia ya kujiamini sana.
 
Back
Top Bottom