Eti kwa njia ya internet

KakaJambazi

JF-Expert Member
Jun 5, 2009
18,711
12,067
Mi huwa nakereka sana na TBC mnaposema "........Kama alivyotutumia habari hii kwa njia ya internet/mtandao/satelite".

Nia yenu hasa ni nini? tuogope?? au tujue mmeendelea sana ki-technologia? au picha hazitakua na quality? au mbembwe tu.

Mnawapumbazaga na kuwaokota wa huko vijijini tu, ambao satelite au sijui internet kwao wanaona kama vile mwandishi alienda space kutuma.
Mbona hakuna tv station yeyote duniani wanaotamka ivyo??? au wao hawatumii na wanajua technolojia iyo ishapitwa na wakati na nyie ndo mmevumbua sasa?

Yaani hata citizentv ya watani zetu inawashinda?

Badilikeni jamani, internet sasa ivi haitustui watanzania.
 
mzee mtangazaji muhusima alipo mbali na kituo cha utangazaji huwapelekea tbc makao makuu habari hiyo kwa njia hiyo net

Kwani kunaulazima gani wa kutuambia?? kwani wasipotamka habari haitasikika ? kuna tija gani tunayopata baada ya kutueleza hivyo?
 
Wakisema hivyo waandishi wa vituo vya nje kama CNN, Al Jazeera, BBC n.k. huwa unalalama?
 
Wakuu kama mnasikiliza BBC Radio au TV lazima kabla ya mwandishi kuwaletea newz utasikia anatambulisha kwanza either utasikia report from Video Phone, au email kama ni radio utasikia his fax report au email au podcast ni vitu vya kawaida jamani mimi wakati TV Station Bongo hazijaingia mzee wangu alikuwa anapenda sana kusikiliza redio ujerumani, toka 1982 baba yangu alikuwa msikilizaji mzuri sana wa news toka Ujerumani, baadaye miaka ya 1990 alipenda sana kusikiliza BBC radio ya kiingereza na kiswahili, hapo ndo nilikuwa nasikia mzungu akitema yai a fax report from our BBC correspondent in Siera Leona. Wakati huo Muasi Foday Sanko anatesa huko. So ni vitu vya kawaida kutaja jinsi hiyo ripoti ilivyotumwa.
 
Mi huwa nakereka sana na TBC mnaposema "........Kama alivyotutumia habari hii kwa njia ya internet/mtandao/satelite".

Ni kweli there is NO need bcs tunajua mpo juu na very complicated
mtaje aliyetoa habari Inatosha!
 
kiuandishi au kiupashanaji habari hicho kitu ni muhimu sana, kwa sababu kwanza quality ya picha na sound lazima itakuwa ni tofauti, vile vile wavelegth zinazotumika huwa sio sawa, kwa hiyo kiuandishi ni lazima uambiwe hiyo picha unayoiona ni aina fulani, anyway kama ulivyosema wewe unakereka ni wewe lakini kwa mimi naona ni sawa na nina haki ya kujua ni aina gani ya picha ninayoonyeshwa
 
Tunachohitaji ni hicho chakula (habari) chenyewe na mpishi labda toka sehemu fulani, hatuhitaji kujua kimepikwaje, kimepikwa na jiko la mchina, umeme,kuni, gasi, viungo gani vimetumika, kimekuja kwa ndege, treni, ungo, daladala etc mezani. Hii ni sawa na msanii kuwa na singo iliyomtoa kisha harakahara anataka kujaziajazia ili tu atoe album (ie kukosa chakujazia kwenye muda wa habari mpaka maoni ndani).
Binafsi linanikera sana, ila kakaJ umenikumbusha leo.
Ni maoni tu.
 
Mi huwa nakereka sana na TBC mnaposema "........Kama alivyotutumia habari hii kwa njia ya internet/mtandao/satelite".

Nia yenu hasa ni nini? tuogope?? au tujue mmeendelea sana ki-technologia? au picha hazitakua na quality? au mbembwe tu.

Mnawapumbazaga na kuwaokota wa huko vijijini tu, ambao satelite au sijui internet kwao wanaona kama vile mwandishi alienda space kutuma.
Mbona hakuna tv station yeyote duniani wanaotamka ivyo??? au wao hawatumii na wanajua technolojia iyo ishapitwa na wakati na nyie ndo mmevumbua sasa?

Yaani hata citizentv ya watani zetu inawashinda?

Badilikeni jamani, internet sasa ivi haitustui watanzania.

yaani hiyo issue imenikera hadi nimechoka, HUO NI USHAMBA WA HALI YA JUU, watangazaji hao huwa wanaboa sana, ni kama kujionyesha kuwa internet ni kitu cha ajabu sana, kitu cha hali ya juuuuuuu, ni maendeleo yao ya technologia ya juuuuu, hasa hao kina muhando wadada hao...wanakera sana kuwasikiliza. kwani internet ni kitu cha ajabu sana kwa hawa watangazaji, halafu hata kabla haujaweka hii thread, nilishataka kuja kutoa dukuduku langu hili muda mrefu tu, asante kwa kuiweka leo, nafikiri watasoma hapa na wataacha kutangaza kama wametoka kijijini leo kwasababu hiyo tbc 1 inaangaliwa na watu hata nje ya nchi,inatuwakilisha hivyo waacha kutuaibisha,...alaa
 
kiuandishi au kiupashanaji habari hicho kitu ni muhimu sana, kwa sababu kwanza quality ya picha na sound lazima itakuwa ni tofauti, vile vile wavelegth zinazotumika huwa sio sawa, kwa hiyo kiuandishi ni lazima uambiwe hiyo picha unayoiona ni aina fulani, anyway kama ulivyosema wewe unakereka ni wewe lakini kwa mimi naona ni sawa na nina haki ya kujua ni aina gani ya picha ninayoonyeshwa

ulishawai kuona nchi yeyote ile duniani watangazaji wake wanaongea hivyo, si bongo tbc one tu ndo wanafanya hivyo, kwani itv na wengine huwa hawana habari kwa njia ya internet?, tatizo internet tz imeanza kutumiwa juzi tu hapa, ndo watu wanafunguka majicho, hamna cha uandishi wala nini, ni limbukeni tu hiyo, wanakere banaa aaaaa
 
Sa kama ni ivo kwanini hawatuombi radhi baada ya kutoa hiyo taadhari?
 
ulishawai kuona nchi yeyote ile duniani watangazaji wake wanaongea hivyo, si bongo tbc one tu ndo wanafanya hivyo, kwani itv na wengine huwa hawana habari kwa njia ya internet?, tatizo internet tz imeanza kutumiwa juzi tu hapa, ndo watu wanafunguka majicho, hamna cha uandishi wala nini, ni limbukeni tu hiyo, wanakere banaa aaaaa

Mkuu hawa watu inabidi tuendelee kuwa-shape, isije siku moja wakaripoti "....................msafara wa Waziri mkuu ulifika jana London kwa ndege, ukitokea Dar es salaam"
What a shame!!!
 
yaani hiyo issue imenikera hadi nimechoka, HUO NI USHAMBA WA HALI YA JUU, watangazaji hao huwa wanaboa sana, ni kama kujionyesha kuwa internet ni kitu cha ajabu sana, kitu cha hali ya juuuuuuu, ni maendeleo yao ya technologia ya juuuuu, hasa hao kina muhando wadada hao...wanakera sana kuwasikiliza. kwani internet ni kitu cha ajabu sana kwa hawa watangazaji, halafu hata kabla haujaweka hii thread, nilishataka kuja kutoa dukuduku langu hili muda mrefu tu, asante kwa kuiweka leo, nafikiri watasoma hapa na wataacha kutangaza kama wametoka kijijini leo kwasababu hiyo tbc 1 inaangaliwa na watu hata nje ya nchi,inatuwakilisha hivyo waacha kutuaibisha,...alaa

Kweli mkuu, hawa watu sijui kwanini huwa wanatutaadharisha.
Kwenye channel za movie huwa tunaona tahadhari kama hizi:-
PG, VL16, SVL18 etc Sa kama wao wamevumbua INTERNET, waedisplay kwenye screen basi.
 
kiuandishi au kiupashanaji habari hicho kitu ni muhimu sana, kwa sababu kwanza quality ya picha na sound lazima itakuwa ni tofauti, vile vile wavelegth zinazotumika huwa sio sawa, kwa hiyo kiuandishi ni lazima uambiwe hiyo picha unayoiona ni aina fulani, anyway kama ulivyosema wewe unakereka ni wewe lakini kwa mimi naona ni sawa na nina haki ya kujua ni aina gani ya picha ninayoonyeshwa

Wanatakiwa wawe kimataifa zaidi, sio kuwatishia watanzania wasioelewa,, eti kwa njia ya mtandao wa internet.
 
hiki ni kitu kinachokera sana kusikiliza....hivi wameanza kutumia internet lini? huwa sipendi kusikia, ndo maana watu wanatuita watz washamba ivoivo....
 
Naona kwao internet ni kitu cha ajabu sana, huenda typewrite ndo wameziacha kutumia mwaka huu baada ya wachina kuwaletea computer.

Huwa sioni ulazima wa kui-aknowledge internet kivile actually.
 
Back
Top Bottom