Eti… kuna sumu ya mapenzi…!?

Agika nitapita mtaani kula ftari natumai ni ile ya 'open' kwa kila mtu.

Natanguliza shukrani.

On a separate note, WoS karibu tena kweli tulikumiss kwenye hili jamvi, all for a good course. Karibu sana.
 
Sumu ya mapenzi jamani ni…

1. Ni maudhi…
Uliza watakwambia, hakuna kitu kinachoporomosha penda kama maudhi ya kila kukicha, na hii inakuwa sababu kuu ya kwanza kuliko zote ambazo nitazitaja hapo chini. Kila kukicha kuna hiki, mara kile mara hiki.

Mwisho wa siku Pendo huota mbawa bibi upo hapo. Basi kama kuna cha kuepuka cha kwanza hiki hapa. Epuka kugeuka kuwa kero.

2. Sumu ya mapenzi ni Ufitini…
Anayekuja kukwambia mumeo hivi jua kakubebea kichupa cha sumu amekuja nacho ukimalize. Najua hii wengi mtachukulia tofauti, lakini ukweli unabaki pale pale, fitina siku zote hana jema katika mapenzi yenu, tena mkishamjua mchemshieni maji ya moto mmumwagie (Natania).

Tukiweka utani mbali mambo ambayo huua mapenzi ya watu ni watu ambao hawapendi kuiona meli yenu ya mapenzi baharini. Chukua hiyo.

3. Sumu ya mapenzi ni usaliti…
Hiki ni kidonda shosti, tenda donda sugu katika mapenzi, na hata kikipona basi kovu lake huwa kubwa pengine kuliko hata kovu la jeraha la panga. Hakuna anayejua maumivu ya usaliti isipikuwa yule uliyemfika.

Na katika mapenzi imani ikipotea basi kuirejesha itakugharimu zaidi ya mapenzi. Nauliza chai ikiingia chumvi itaitwa chai au itageuka kuwa supu. Nadhani mpaka hapa ushajua kuwa hii nayo ni sumu kali zaidi ya chatu.

4. Sumu ya mapenzi ni Gubu…
Mwanamke mwenye gubu kwa maana nyingine hujulikana kama mwanamke mwenye nongwa, mwanamke dizaini hii kuwa kwake la kheri nongwa la shari nongwa.

Nazungumzia hulka ile ya kuwa msununu kwako jema halijulikani wala baya halijulikani. Mwanamke huyu ni Yule aliyetaja katika bibilia kuwa huvunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe.

5. Sumu ya mapenzi ni Uchafu na Uvivu wako… Hivi vitu viwili ni baba moja na mama mmoja. Ukiwa mvivu bila shaka utakuwa mchafu, na ukiwa umchafu unasababu nyingine ya kwanini unakiwambiwa. Mwanamke usafi bibi asikudanganye mtu. Kifupi na hayo tu.
By Asma
Aksante babu, leo naona angalao akili zimekukaa sawa mpaka ukatengeneza mada ya maana...lakini mbona inawalenga wanawake tuu mbona sasa hayo uliyosema wengine yapo kwa ma Mr. zetu! Ehe na hapa utatushauri nini sasa.
 
Ama kweli u care my sistah!
.
asante dada WoS, si unajua tena wanawake tumeumbiwa kuwa na upendo na kujali kwasababu Mwenyezimungu alishatupa ile kazi ya kuongeza idadi ya watu duniani ,akatutunikia huruma na upendo tele ili tutunze familia zetu kutumia upendo huohuo.
Wanaume mwezi mtukufu mnawapa special treat wake zenu kwa kuwajali au? Haya ndio mapenzi ya dhati eti asikudanganye mtu.

ila for the record dada when you do it do it because you feel it en do not expect the same from them otherwise you will be frustrated. akikufanyia unamshukuru Mungu asipokufanyia atleast hukufanya ili akufanyie.
 
Agika nitapita mtaani kula ftari natumai ni ile ya 'open' kwa kila mtu.

Natanguliza shukrani.

On a separate note, WoS karibu tena kweli tulikumiss kwenye hili jamvi, all for a good course. Karibu sana.
Karibu sana Kaizer tena mie na wewe yakhee tuko karibu mnooo.............usisahau kuvaaa barakashia tuuuu hahhahah
 
Sumu ya mapenzi jamani ni…

4. Sumu ya mapenzi ni Gubu…
Mwanamke mwenye gubu kwa maana nyingine hujulikana kama mwanamke mwenye nongwa, mwanamke dizaini hii kuwa kwake la kheri nongwa la shari nongwa.

Nazungumzia hulka ile ya kuwa msununu kwako jema halijulikani wala baya halijulikani. Mwanamke huyu ni Yule aliyetaja katika bibilia kuwa huvunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe. by Asma


Jamani naombeni tafsiri ya neno Gubu haswa maana yake ni nini? Na huyo mwenye gubu (nogwa) ndio mtu wa aina gani?
 
Back
Top Bottom