Eti Kikwete acharuka!

usanii mtupu muda wote huo alikuwa wapi? amesafiri mpaka amechoka ndio anaona atuzuge na ziara zake za wizara.... aende zake wananchi wameshamchoka tena sana
 
Kikwete maneno meeeeeeng vitendo hakuna,kila nikimwangalia rais nacheka sana,wakati wa kampeni aliahidi kuwaletea meli watu wa Chunya wakati hata ziwa hawana!
 
RAIS Jakaya Kikwete amemtaka Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja kuwa makini na utatuzi wa suala la matatizo ya umeme ili kuiepusha nchi kuingia katika kashfa kama iliyosababishwa na Mkataba wa Richmond.

Katika hatua nyingine, Rais Kikwete ameagiza kuwekwa pembeni kwa ushabiki wa kisiasa katika utekelezaji wa miradi ya uzalishaji umeme ili kuweza kufikia malengo yaliyowekwa na serikali ya kuzalisha zaidi ya megawati 1,130 za umeme ifikapo mwaka 2013.

Rais Kikwete aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na maofisa wa Idara na Mashirika yaliyo chini ya Wizara ya Nishati na Madini katika ziara yake ya kikazi ya siku moja kwa wizara hiyo jana.

HabariLeo | Kikwete acharuka, amtaka Ngeleja awe makini

Naye aache kulalamika kwa wananchi, achukue hatua kama nchi imemshinda akae pempeni waTZ tuko wengi wa kuongoza hii inchi.

Kila siku anakuja na ahadi ambazo hazina tija kwa wananchi hata kidogo, nani hajui kama aliahidi swala la umeme aliahidi kuisha kabla ya 2010, na leo anasemaa litaisha kabla ya 2013 huu ni uwongo usiokubalika

anasubiri muda wake uishe then atuachie matatizo lukuki.
 
Tanzania haijaanza kukaa kiza kipindi cha JK, nakumbuka alipoingia madarakani alirithi kiza kikubwa kutoka kwa??? Utajaza mwenyewe. At least JMK anafanya jitihada za kweli za kukiondoa kiza. Wa kabla yake, wooooote, walifanya nini?

Alituahidi maisha bora kwa kila Mtanzania kwa Ari mpya Nguvu mpya na Kasi Mpya. ina maana aliona wenzake walisuasua yaani walikuwa wanaenda kwa kasi ya kinyonga sasa yeye akatuahidi kasi ya Duma, anapokwenda kasi ya KOBE ndio maana tunamwambia sio kasi hiyo uliyotu ahidi? Embu tueleze toka 2006 hadi 2010 ktk Gridi ya Taifa wameongeza Megawwat ngapi? maana unasema JK ndie ameonyesha jitihada kubwa kupambana na tatizo la umeme kuliko wale walio mtangulia
 
Mtu anauchapa tena mbele yake ataweza kumwajibisha kweli?

03_11_8cu1nz.jpg
Mbona yuko makini long time au mi naangalia vibaya
 
Kikwete maneno meeeeeeng vitendo hakuna,kila nikimwangalia rais nacheka sana,wakati wa kampeni aliahidi kuwaletea meli watu wa Chunya wakati hata ziwa hawana!

hizi ndo ahadi zile alisema huwa mnaziongeza tuu! hahhaha mkuuu umeongeza hii!
 
[/COLOR]
hizi ndo ahadi zile alisema huwa mnaziongeza tuu! hahhaha mkuuu umeongeza hii!
hajawa adui yangu kiasi hicho!had nimsingizie uongo.
Nampenda kama rais anayenitawala.namchukia kwa kutotimiza alichoahidi
 
hawa jamaa ni marafiki wa karibu,so sijawahi ona rafiki akimkemea rafikie kwa swala la ulaji,ukizingatia urafiki ndio uliofanya Ngereja kuteuliwa hapo alipo
hehehehe,naungana na mwana jf kuwa ni mchezo wa kuigiza tuuuu

Si ajabu baadaye jioni Jk alimpigia simu Ngeleja na kumwambia "...usimind bana si unajua tena tehetehetehe"
 
people are extremely negative dah hii kali..... tulimchagua wenyewe na tusubiri amalize muda wake maana kama ni kuandamana sioni muandamanaji tu. pia kiasilia kila m-tz ni fisadi tu. :A S clock:
 
Hivi Kiwira ilirudishwa lini serikalini? Na kina Mkapa walipewa nini wakakubali Kiwira ichukuliwe? Maana kama waliweza kuichukua Kiwira kutoka kwa mwekezaji aliyeingiza fedha zake na aliyekuwa na mkataba na Tanesco; ni kitu gani kimewafanya washindwe kumnyang'anya mwekezaji majenereta yake na kuyaleta serikalini?
 
Wewe raia wa Tanzania! JK ni JK, Mkapa ni Mkapa, Mwinyi ni Mwinyi, the past is rotten huu ni wakati wa kuface real situation sio wakati wa kufanya comparison, we are suppose to face real problems sio kufanya COMPARISON KAMA MAZUZU. hii ni karne ya 21. we tanzanians need to be REAL and Face Real Situation. POWER RATIONING is a REAL problem to the country. Maraisi waliopita walikuwa wanaongoza in a "condusive environment" where by the number of Interllectuals were counterble but today JK is facing "CHALLENGES" in his Leadership, reason being Today at least we have people who are keen, PEOPLE WHO CAN KEEP THE GOVERNMENT ON ITS TOES. :embarassed2::smash::smash:
 
Tatizo waliyachukulia mambo ya kitaalamu kwa kisiasa na kibiashara zaidi. Kama wataalamu wa TANESCO wangekuwa huru kufanya kazi yao, tusingefika hapa. Sasa wao wamekuwa wakifata maelekezo ya kisiasa na kibiashara kwa maslahi ya watu fulani na siyo Taifa. Napendekeza bodi ya TANESCO ipewe ruksa ya kupanga na kutekeleza mambo yake, pia waachwe huru kuyafanyia kazi zao kwa utaalamu, wakishindwa ndiyo waombe msaada serikalini. Siyo mambo yaendeshwe na wengine halafu yakishindikana ndiyo washirikishwe. Wataalamu wa TANESCO wapo wengi (siyo wale vishoka), ila wafanye nini kwenye sakata hili. Leo tunaihukumu TANESCO kwakushinwa huku tukijua serikali (hasa Zanzibar) ndiyo wadaiwa na wakwamishaji wakubwa wa shirika hili.
 
BIG UP TO CHADEMA, sasa Bwana MKUBWA anajitahidi japo kidogo akaze kamba Kufuatilia mambo CDM endeleeni kuplay part yenu ya KUIWEKA SERIKALI JK on ITS TOES, BIG UP to Kamanda wa Anga Freeman Mbowe na Dr. Slaa, hiyo ndo kazi tuliyo watuma.
 
Tanzania haijaanza kukaa kiza kipindi cha JK, nakumbuka alipoingia madarakani alirithi kiza kikubwa kutoka kwa??? Utajaza mwenyewe. At least JMK anafanya jitihada za kweli za kukiondoa kiza. Wa kabla yake, wooooote, walifanya nini?

1)TAA,(TANU,ASP) CCM,
2)BABA WA TAIFA, MZEE MWINYI,MKAPA,KIKWETE..
3)NGUMBARU, SIASA NI KILIMO,KILIMO CHA KUFA NA KUPONA, UPE, SHULE ZA KATA,KILIMO KWANZA..
4)IPTL,RICHMOND,DOWANS..

Kitu gani cha kujivunia hapo juu, urithi upi ni bora jibu ni fupi CCM should GO
 
Tanzania haijaanza kukaa kiza kipindi cha JK, nakumbuka alipoingia madarakani alirithi kiza kikubwa kutoka kwa??? Utajaza mwenyewe. At least JMK anafanya jitihada za kweli za kukiondoa kiza. Wa kabla yake, wooooote, walifanya nini?

Wewe nafikiri umegoma kutumia Akili yako au umeazimisha, kama zipo unakumbuka MOtto wa JK wakati anaingia Ikulu? NIkukumbushe MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA, JE HAYO UNAWEZA THIBITISHA LEO BAADA YA MIAKA SITA MADARAKANI?
 
We hujui kuwa huyo ni Makamba?
 
Tanzania haijaanza kukaa kiza kipindi cha JK, nakumbuka alipoingia madarakani alirithi kiza kikubwa kutoka kwa??? Utajaza mwenyewe. At least JMK anafanya jitihada za kweli za kukiondoa kiza. Wa kabla yake, wooooote, walifanya nini?

Tatizo la kuwa gizani lilianzia mikononi mwake mwaka 1992 alipokuwa wizara hiyohiyo ya nishati...remember? na limeendelea kuwepo kwa serikali zote alizozitumikia bila kukatishwa...usitetee issue kwa kuatamka kumtakasa kwa lawama iliyo mikononi mwake
 
Back
Top Bottom