Eti hatujui... kipimo gani kinatumika?

Tukubali kuenenda kama ilivyo desturi yetu
Kuiga kila kitu kunatugarimu mno
Mapenzi ya kizungu si hadhi yetu

Mi naona vile vizuri tuige, zamani waafrika wengi walikuwa hawaonji real love, moyo uridhike pia, ilikuwa kulazimishana tu, fulani analima sana, muoe, fulani ana mifugo mingi, sijui Chifu, uwaolewa naye, now watu waishi kwa kudecide wenyewen na wanawake waenjoy vya kutosha mahusiano, sio wanaume tu, sio unakuwa na mtu au unaolewa na mtu ili kujishow kwa watu, au kwasababu rafiki zako umeona wako kwenye relation pia, wakati we hauko happy, huenjoy na huyo mpenzi wako ni bora uendelee kuwa single, usubiri, ili umpate huyo anayekufaa, unayeendana naye kiasi kitabia na kikubwa anayekujali na kukuheshimu.
 
wadada wanataka uzungu
wakaka wanataka uafrika
kazi kwelikweli

Pia nadhani katika hili suala la mahaba nadhani wanaume hawajielewi..Wamebaki kuelea hewani..

Nashukuru Mungu nilishamaliza ngwe yangu ya hayo mambo....Sijui kama ningeambulia kitu!
 
Pia nadhani katika hili suala la mahaba nadhani wanaume hawajielewi..Wamebaki kuelea hewani..

Nashukuru Mungu nilishamaliza ngwe yangu ya hayo mambo....Sijui kama ningeambulia kitu!

Hivi kwani mume hatakiwi kuonyesha mahaba nyumbani?
 
Hilo suala la is it fair kuvaa diamond ring wakati kuna watu wanashida duniani linaweza kuanzisha mjadala mrefu lakini kwangu ni fair sana tu. I worked hard for that money ( or the man did), why shouldn't I use it as I see fit?

Unaweza kumlipia karo shem wako na ukamsuuza mwanadani wako sana tu, ila kama mwandani wako hana shem anaehitaji kulipiwa karo jee? Tusikimbie reality tukataka kufanya Watanzania wote wana shida hizo, wengine hawana mkuu, hawa haki yao ya kuonyeshwa mahaba ndo ipotee?

Samahani naomba msaada,

Hivi kuna Mtanzania yeyote ambaye tayari keshajikomboa na kujiondoa kwenye mnyororo wa extended families???

Au wanaficha vichwa vyao kwenye mchanga kama mbuni ili wafurahie mahaba bila kuwafikiria ndugu na jamaa zao wanaosota kwenye tope la umasikini??!!
 
Hivi kwani mume hatakiwi kuonyesha mahaba nyumbani?

Sina jibu kwa sababu wanaopokea ndio wanaweza kujibu...Mimi nilidhani kwama hayo tunayowafanyia wenzi wetu ndiyo mahaba tosha!

Sasa kama wana kipimio chao cha Uzungu na Roma basi tutakuwa tumeuvaa mkenge!
 
uzungu usiwe mwingi sana
hivi kina bibi na babu waliishije katika kuromanciana????

Ingekuwa vizuri kama tungeweza kupata jibu la hilo swali.

Nadhani kipimo cha hao bibi zetu kilishatupwa mtoni na kuingizwa kipya...Ndio maana tuna-float hewani!!
 
Samahani naomba msaada,

Hivi kuna Mtanzania yeyote ambaye tayari keshajikomboa na kujiondoa kwenye mnyororo wa extended families???

Au wanaficha vichwa vyao kwenye mchanga kama mbuni ili wafurahie mahaba bila kuwafikiria ndugu na jamaa zao wanaosota kwenye tope la umasikini??!!

Wapo watu hawana matatizo hayo ya extended family kwa sababu wao extended family mwisho wake ni cousins (mama, baba, na watoto watokanao na ndugu wa baba na mama pekee). Na ikiwa familia ni ya kitajiri tokea babu yao, basi hakuna matatizo mengi yanayohusu familia.
Sasa ukitaka kulipa karo ya mtoto wa familia hiyo ujue kuwa ni milioni kadhaa kwa mwaka. Si bora umpe perfume tu :]]

Note: DC inaonyesha wewe ni wa zamani sana, lakini tayari kuna familia ambazo ni matajiri tangu babu zao.
 
Mi naona vile vizuri tuige, zamani waafrika wengi walikuwa hawaonji real love, moyo uridhike pia, ilikuwa kulazimishana tu, fulani analima sana, muoe, fulani ana mifugo mingi, sijui Chifu, uwaolewa naye, now watu waishi kwa kudecide wenyewen na wanawake waenjoy vya kutosha mahusiano, sio wanaume tu, sio unakuwa na mtu au unaolewa na mtu ili kujishow kwa watu, au kwasababu rafiki zako umeona wako kwenye relation pia, wakati we hauko happy, huenjoy na huyo mpenzi wako ni bora uendelee kuwa single, usubiri, ili umpate huyo anayekufaa, unayeendana naye kiasi kitabia na kikubwa anayekujali na kukuheshimu.

Nat,

Inawezekana baadhi ya wanawake waliishi kwa mateso maisha yao yote kutoka na mila ambazo ziliwanyima nafasi ya kujichagulia wachumba. Hata hivyo nashindwa kuelewa kwa nini mfumo huo ulidumu miaka mingi bila kupingwa wazi wazi na wanawake....Hapa nitaomba wataalamu wanisaidie!

Hata hivyo, pamoja na mabadiliko bado kuna vitu vimegoma kubalidilishwa au muda wake bado..Mfano, wasichana wengi wa Kiafrika bado wanasubiri kutongozwa badala ya kujichukulia sheria mkononi na kusaka kile wanachokipenda!!
 
Jana nimesoma makala ya Freddy Macha kwenye gazeti la Mwananchi iliyokuwa inaongelea mijadala inayoendelea kwenye mitandao mbali mbali ikieleza kuwa wanaume wa Kitanzania (na labda Waafrika wote) hatujui mahaba (romance)!

Nimeguswa sana na makala hiyo. Si kwa sababu napingana na hoja za hao wanaosema hivyo, bali nina wasi wasi kwamba vigezo vinavyotumiwa vinaweza kuwa siyo sahihi.

Inawezekana hii mada ilishajadiliwa hapa pia, ila naomba tu kupata maoni ya wadau wa jukwaa letu hili tukukufu kuhusiana na issue hii.

1. Ni kweli wanaume wa Kitanzania hawajui mahaba??

2. Kama hawajui, ni kosa lao peke yao au na wenzi wao (wanawake)???

3. Na vigezo gani vinatumiwa ku-judge kama mtu anajua mahaba au la?

Naomba maoni yenu!!

Babu DC
Mkuu waambie hao jamaa watuombe razi, wametukosea heshima sana espesheli mimi.

Dah! yaani samtaimu waifu nampigisha msuwaki mwenyewe halaf wananiambia sjui mapenzi . Khaaa! Mungu atatulipia aisee
 
Wapo watu hawana matatizo hayo ya extended family kwa sababu wao extended family mwisho wake ni cousins (mama, baba, na watoto watokanao na ndugu wa baba na mama pekee). Na ikiwa familia ni ya kitajiri tokea babu yao, basi hakuna matatizo mengi yanayohusu familia.
Sasa ukitaka kulipa karo ya mtoto wa familia hiyo ujue kuwa ni milioni kadhaa kwa mwaka. Si bora umpe perfume tu :]]

Note: DC inaonyesha wewe ni wa zamani sana, lakini tayari kuna familia ambazo ni matajiri tangu babu zao.

Hizo familia ziko hapa Tanzania kweli....Kwa sababu watu walio wengi utajiri wao umeanza juzi juzi baada ya kuanza mfumo wa kifisadi.

Pia huo ukomo wa ndugu nao unanitisha kidogo...Labda kama hao watu walishaachana na vijiji vyao!
 
Mkuu waambie hao jamaa watuombe razi, wametukosea heshima sana espesheli mimi.

Dah! yaani samtaimu waifu nampigisha msuwaki mwenyewe halaf wananiambia sjui mapenzi . Khaaa! Mungu atatulipia aisee

Pole sana Brother,

Hivi ulimuuliza shem kama suala la kumpigisha mswaki limo kwenye kamusi yake ya romance na romantic items/issues?

Hebu mtendee haki ili usije kukimbiwa!!
 
Hizo familia ziko hapa Tanzania kweli....Kwa sababu watu walio wengi utajiri wao umeanza juzi juzi baada ya kuanza mfumo wa kifisadi.

Pia huo ukomo wa ndugu nao unanitisha kidogo...Labda kama hao watu walishaachana na vijiji vyao!

Hivi watoto wa siku hizi bado wanaelewa kuhusu jamaa wa vijijini kweli? Mtoto kazaliwa town, kasoma boarding school maisha yake yote na likizo anarudi town unadhani atakuwa na mapenzi na ndugu wake jamaa wa mbali wa vijijini?

Inaweza kuwa hawakuwa matajiri kwa mali nyingi, lakini wote wamesomeshwa (ndugu wa mama na baba) kiasi cha kuwa kuwapatia elimu watoto wao hawashindwi.

Mbona hiyo definition ya extended family ni ya kawaida sana kwa kizazi hichi! Hivi mtoto wa mjomba Wa mama nalazimika kumsaidia kweli?
 
Pia si lazima kama kumpa zawadi girl wako, ili kumshow how much unamcare iwe ya gharama kubwa, unaweza ukamnunulia pipi chache, ua au chocolate, unaweza ukanunua pia chocolate mkashare, na kama ameifungua hiyo chocolate mbele yako na hakukulisha, ujue hakupendi au ulimuudhi, si ajabu kwa makusudi na hukuomba msamaha, ndio maana kukujali kwake kunapungua.

Msamaha ni muhimu sana, na mazungumzo ya mara kwa mara naye ili ujue na yeye akueleze makosa na maudhi madogo madogo uliyotenda na wewe umuleze, ajue makosa madogo madogo aliyokukosea, ili muombane msamaha na kuweka mambo sawa na kuendeleza upendo na kujaliana katika uhusiano wenu, kupeana zawadi siyo mpaka sikukuu na birthday, inakosesha raha, zawadi za kushtukiza mara kwa mara zinaleta furaha kwenye uhusiano na ndoa, kutoka na kutoana out pamoja au na watoto pia, pia kusisahaulike.

Mnaweza kwenda Beach au sehemu tofauti kuenjoy na kurelax, hapo mtaboresha mahusiano na ndoa yenu kwa kiwango kikubwa hata watoto wenu watakuwa na furaha ya kutosha, watoto nao wasisahaulike pia kwenye kupewa zawadi, wapewe zawadi pia mara kwa mara vilevile wafundishwe kuwapenda wengine, kuwajali, kuwa makini,kujilinda, kusali, kujidefend,kuwork hard, Kujipenda, kujijali, kusamehe na kuomba msamaha wanapokosa.

Na sisi waafrika tujifunze kuwaomba msamaha watoto wetu na watu wengine, hata housegirl tunapowakosea, ili kuwaondolea hasira, chuki, maumivu na kupoza majeraha kwenye mioyo yao ili waweze kuwa na furaha, kutupenda na kutujali tena. Mtu anaweza kuudhiwa na watu 3, akajisikia vizuri na kupoa kwa kiasi kikubwa moyoni kwa kuombwa msamaha na wawili tu kati ya hao watatu, na hivyo kumfanya asiwe na hasira, awe na furaha na amani na watu wanaomzunguka na wale anaokutana nao na kufanya maisha yake yawe ya furaha kwa kiasi kikubwa.
 
Jana nimesoma makala ya Freddy Macha kwenye gazeti la Mwananchi iliyokuwa inaongelea mijadala inayoendelea kwenye mitandao mbali mbali ikieleza kuwa wanaume wa Kitanzania (na labda Waafrika wote) hatujui mahaba (romance)!

Nimeguswa sana na makala hiyo. Si kwa sababu napingana na hoja za hao wanaosema hivyo, bali nina wasi wasi kwamba vigezo vinavyotumiwa vinaweza kuwa siyo sahihi.

Inawezekana hii mada ilishajadiliwa hapa pia, ila naomba tu kupata maoni ya wadau wa jukwaa letu hili tukukufu kuhusiana na issue hii.

1. Ni kweli wanaume wa Kitanzania hawajui mahaba??

2. Kama hawajui, ni kosa lao peke yao au na wenzi wao (wanawake)???

3. Na vigezo gani vinatumiwa ku-judge kama mtu anajua mahaba au la?

Naomba maoni yenu!!

Babu DC

Wanaposema mahaba wana maana gani?
 
Klorokwini, shemeji yangu nionee huruma na hizi mbavu zangu! utanunua kesi we shemeji yangu lol.
Kweli bwana we uko very romantic dah, sie tu haturidhiki.

Hii mada naisoma kwanza dah!

Mkuu waambie hao jamaa watuombe razi, wametukosea heshima sana espesheli mimi.

Dah! yaani samtaimu waifu nampigisha msuwaki mwenyewe halaf wananiambia sjui mapenzi . Khaaa! Mungu atatulipia aisee
 
Hivi watoto wa siku hizi bado wanaelewa kuhusu jamaa wa vijijini kweli? Mtoto kazaliwa town, kasoma boarding school maisha yake yote na likizo anarudi town unadhani atakuwa na mapenzi na ndugu wake jamaa wa mbali wa vijijini?

Inaweza kuwa hawakuwa matajiri kwa mali nyingi, lakini wote wamesomeshwa (ndugu wa mama na baba) kiasi cha kuwa kuwapatia elimu watoto wao hawashindwi.

Mbona hiyo definition ya extended family ni ya kawaida sana kwa kizazi hichi! Hivi mtoto wa mjomba Wa mama nalazimika kumsaidia kweli?

Mimi nilidhani nikiijali family ya my wife wangu hadi wajomba na mama wadogo nakuwa nimepita mtihani wa kuwa na mahaba...kumbe chali..

Ningeweza kurudisha mshale wa saa nyuma ingebidi nirudi darasani kwanza!!
 
Pia si lazima kama kumpa zawadi girl wako, ili kumshow how much unamcare iwe ya gharama kubwa, unaweza ukamnunulia pipi chache, ua au chocolate, unaweza ukanunua pia chocolate mkashare, na kama ameifungua hiyo chocolate mbele yako na hakukulisha, ujue hakupendi au ulimuudhi, si ajabu kwa makusudi na hukuomba msamaha, ndio maana kukujali kwake kunapungua, msamaha ni muhimu sana, na mazungumzo ya mara kwa mara naye ili ujue na yeye akueleze makosa na maudhi madogo madogo uliyotenda na wewe umuleze, ajue makosa madogo madogo aliyokukosea, ili muombane msamaha na kuweka mambo sawa na kuendeleza upendo na kujaliana katika uhusiano wenu.

Kupeana zawadi siyo mpaka sikukuu na birthday, inakosesha raha, zawadi za kushtukiza mara kwa mara zinaleta furaha kwenye uhusiano na ndoa, kutoka na kutoana out pamoja au na watoto pia, pia kusisahaulike, mnaweza kwenda Beach au sehemu tofauti kuenjoy na kurelax, hapo mtaboresha mahusiano na ndoa yenu kwa kiwango kikubwa hata watoto wenu watakuwa na furaha ya kutosha.

Watoto nao wasisahaulike pia kwenye kupewa zawadi, wapewe zawadi pia mara kwa mara vilevile wafundishwe kuwapenda wengine, kuwajali, kuwa makini,kujilinda, kusali, kujidefend,kuwork hard, Kujipenda, kujijali, kusamehe na kuomba msamaha wanapokosa na sisi waafrika tujifunze kuwaomba msamaha watoto wetu na watu wengine.

Hata housegirl tunapowakosea, ili kuwaondolea hasira, chuki, maumivu na kupoza majeraha kwenye mioyo yao ili waweze kuwa na furaha, kutupenda na kutujali tena, mtu anaweza kuudhiwa na watu 3, akajisikia vizuri na kupoa kwa kiasi kikubwa moyoni kwa kuombwa msamaha na wawili tu kati ya hao watatu.

Na hivyo kumfanya asiwe na hasira, awe na furaha na amani na watu wanaomzunguka na wale anaokutana nao na kufanya maisha yake yawe ya furaha kwa kiasi kikubwa.

Hivi hizo zawadi lazima ziwe za kizungu ili watoto wa siku hizi watuone kwamba tu watu wa mahaba? Nikibeba pakiti ya miwa, ubuyu, korosho, karanga au matunda damu ya Lushoto nakuwa nimepotea maboya?
 
Limo mkuu, infakti ni moja kati vianzio vianzio vyetu vya ile kitu roho inapenda

Kama kumpiga mswaki laazizi wako limo katika package ya mahaba (kwa mtazamo wako), mbona sasa unashitakiwa kuwa una below (umeshindwa mtihani) kwenye mambo ya mahaba??

Klorokwini, shemeji yangu nionee huruma na hizi mbavu zangu! utanunua kesi we shemeji yangu lol.
Kweli bwana we uko very romantic dah, sie tu haturidhiki.

Hii mada naisoma kwanza dah!

MJ1 sasa unaleta topic nyingine....Ni kwamba hamridhiki au sisi hatujue kuwapa full dose??
 
Back
Top Bottom