eti 'HAKUNAGA'..

Tanzania ya leo ni upuuzi mtupu. Mtu anaweza kuimba chochote kwa kuharibu lugha na hata kutukana na wimbo ukashika chati . mambo hayaishii hapo wacheza senema ndio usiombe wao wanaweza kucheza picha ya ajabu nayo ikauzwa sana na hakuna wa kuuliza. zamani kulikuwa na taasisi za kudhibiti picha zinazostahili kuonyeshwa." Fiilm Tanzania" Wenzetu wa rate picha zao sisi kila kitu uza au onyesha. tujitazame.....
 
Moja ya mambo yatayochelewesha ukuaji wa kiswahili ndio hili la kujifanya "polisi". Kiingereza kimekuwa na kuwa na msamiati unaojitosheleza ni pamoja na kuondoa "polisi" wanaotafuta "most correct -- grammatical, semantical, word formation etc. English, na kwa hilo imekuwa ya kimataifa zaidi.

Pia ili neno litumike inategemea makubaliano baina ya watumizi wa lugha hiyo.

Hakuna kiSwahili kilichokuwa sahihi zaidi.
 
hakunaga....huu wimbo una hit na unaharibu lugha sana....na utashangaa anapewa award he he he he tanzagiza ndo hii
 
Moja ya mambo yatayochelewesha ukuaji wa kiswahili ndio hili la kujifanya "polisi". Kiingereza kimekuwa na kuwa na msamiati unaojitosheleza ni pamoja na kuondoa "polisi" wanaotafuta "most correct -- grammatical, semantical, word formation etc. English, na kwa hilo imekuwa ya kimataifa zaidi.

Pia ili neno litumike inategemea makubaliano baina ya watumizi wa lugha hiyo.

Hakuna kiSwahili kilichokuwa sahihi zaidi.
Kwani kiswahili wakifahamu?

Ona mfano kidogo hapa:
-Alichukua / alichukuliwa.
-Alizawa/ alizaliwa.
Je ipi sahihi hapo?
Usichokoze lugha za wenyewe!
 
Kwa mtazamo wangu suma lee hapaswi kulaumiwa.Hii ni kwasababu mtunzi wa nyimbo anapewa uhuru wa kuvunja taratibu za lugha
ya kawaida katika kutengeneza rhyming (poetic license).Hivyo alichofanya yeye ni kutumia tu poetic license yake.Vilevile imefika wakati
Baraza la Kiswahili Tanzania lihalalishe uongezaji wa kitamkwa ga katika vitenzi ili kuonyesha hali ya mazoea.Na mwisho ametumia lugha inayoreflect jamii yake,ambaye hajawa kuongeza kitamkwa ga katika kitenzi hebu anyooshe kidole tumwone.Tusilaumu tu wadau tuangalie hata nchi za nje jinsi mambo yalivyo,baada ya kulaumu tupressure mabadiliko katika kuhalalisha hili
 
Nchi kama Congo, Rwanda na Burundi ambapo kiswahili kinazungumzwa pia zime halalisha msemo huo ila kwa kua ruhusa ya kuongeza au kuponguza neno kwa kiswahili (hata cha kwao) hawana, kuongeza "ga" mwisho kutaendelea kuitwa "makosa".
Chakufanya ni kujaribu kuelewa ni waati gni neno linabadilishwa hivo, kupata rules na ku-publicise in an accademic journal. kama hakuna chalenger, basi itakua halali.
 
naunga mkono hoja

inakera sana, halafu kibaya zaidi dogo ni mtoto wa kitanga
 
Moja ya mambo yatayochelewesha ukuaji wa kiswahili ndio hili la kujifanya "polisi". Kiingereza kimekuwa na kuwa na msamiati unaojitosheleza ni pamoja na kuondoa "polisi" wanaotafuta "most correct -- grammatical, semantical, word formation etc. English, na kwa hilo imekuwa ya kimataifa zaidi.

Pia ili neno litumike inategemea makubaliano baina ya watumizi wa lugha hiyo.

Hakuna kiSwahili kilichokuwa sahihi zaidi.

Hakuna uiongezee "ga" inaongeza au ku[unguza nini zaidi ya kuchefuwa lugha? Unanshangaza"ga".
 
watu gani watahalibika?au hakunaga ina haribu vipi hiyo lugha?tuseme huo wimbo unaweza ukakubadilisha ukaanza kuongeza ga mwisho wa neno?
tuache watu watumie ubunifu kutoka kuliko kutumia lugha za matusi
 
Wacheni kuharibu lugha yetu adhimu. Wengine hatuna nyengine ila hiyo nyinyi munaotoka mikoani ndiyo munaoharibu.

Mpunze, 'nyimbo' ni neno sawa la kiswahili hii 'wimbo' ni ya juzi tu.
 
watu gani watahalibika?au hakunaga ina haribu vipi hiyo lugha?tuseme huo wimbo unaweza ukakubadilisha ukaanza kuongeza ga mwisho wa neno?tuache watu watumie ubunifu kutoka kuliko kutumia lugha za matusi
apo sasa!! mbona sisi huku iringa na mwanza twatumia tu jamani! wakitumia ''GA'' wabaya ila wakiimba matusi ndo poa eeh!
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom