Eti...eti..mwenge haukufika kileleni ml. K'njaro..kisa.

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
Kutoelewana kati ya serikali na JWTZ kutokana na serikali kuvunja makubaliano ya awali kuwa jeshi la wananchi ndilo lishughulikie mipango yote ya kupandisha na kuzima mwenge miaka 50 ya uhuru. TBC nao (walisusa?). Tukio la mwenge kufikishwa katika kilele cha mlima Kilimanjaro lilipaswa kurushwa LIVE lakini hata hilo halikufanyika sababu wanazotoa zilitokana na kamera za kituo hicho kushindwa kufanya kazi vizuri katika miinuko ya juu. Hata hivyo, mmoja wa watangazaji wa TBC Sostehes Amas, alionekana kupitia kituo hicho akiripoti kutoka katika kilele cha Mlima Kilimanjaro. Hadi leo hakujatolewa hata picha moja ya mwenge ukiwa kileleni.

Source: Mwananchi
 
Mazingaombwe yaendelea kama kawaida ya serikali yetu na viongozi kwenye inshu za kizalendo. Kama hawataki kuonyesha vitu vinavyoelezea nchi yetu! kwa nini wanang'ang'ania kufanya vitu nusu nusu?. Hivi ni vitu ambavyo viko kwenye uwezo wet hatuhitaji misaada, lakini ndo kwanza ufanisi zerooooooooooooo. Viongozi wakiwa waharifu wa mali za umma, hata wananchi hawawezi kujitolea kufanya kile kinachohitajika.
 
Back
Top Bottom