Zawadi Ngoda
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 3,792
- 1,844
Huwezi kuamini kuwa baada ya Watazania kushindwa kutafuta makosa ya kuilaumu serikali ya Kikwete, wamekimbilia sababu zisizoshikika wala kukubalika. Tabasam lake ndio imekuwa nongwa na silaha ya wsiompenda kuelekea uchaguzi wa 2010. Aidha dhambi zake nyingine ni pamoja na kusaidia wanyonge na kuruhusu uhuru wa kusema kwa kila Mtanzania.
Tony Blair na Bill Clinton ndio viongozi wanaoongoza kwa kuwa na tabasam la kila wakati. Wakati huo huo wao ndio viongozi waliofanikisha sana katika kukuza uchumi wa nchi zao. Na hata baada ya kutoka madarakani bado wanasufa kem kem. Joseph Starlin na Mabuto Seseseko ni viongozi waliosifika sana kwa kuwa na tabasam la nadra sana, na walipotoka madarakani majina yao yalikuwa mwiba kwa walimwengu. Sasa vipi tumhukumu Raisi kutokana na tabasam lake? Sioni mantiki katika hili!
Sababu ya pili ninayoisikia sana ni ile ya kudhani kuwa serikali ya Kikwete ni dhaifu. Ukifanya uchunguzi, utakuta kuwa lawama hizo zinatokana na serikali kuwa na utamaduni wa kusikiliza wadau wote na hasa wanyonge. Aidha kutoifanya Tanzania kuwa Polisi State na kuwaswaga wanyonge ni dhambi waionayo wasiompenda. Wengi walizoea Tanzania kuwa Polis state kama ilivyokuwa wakati wa Mkapa, na kudhani kuwa hiyo ndio tafsiri ya serikali strong.
Kutoona mabomu yakishuka Pemba na Mwenbechai, haikuwafurahisha wengi. Ninashindwa kufahamu ni vipi binaadam akafurahia utawala wa mabavu kama ule wa chama kimoja, tulioupiga vita kwa miaka mingi? Tusiwe Egoist kwa dhana kwamba, la msingi ni kutimiziwa mahitaji yangu tu. Hii ni dhana potovu, na haitatufikisha mbali. Ni muhimu kwa watanzania wote kusikilizwa, hoja zao, matatizo yao na ushauri wao. Vinginevyo ni kukubali kuwa Demokrasia imeshindwa au hatuitaki, na pengine turudi kwenye Auktocrat au udikteta.
Suala la tatu la udhaifu wake, eti ni uhuru wa kujieleza. Watanzania hatukuwahi kupata nafasi kama hii kwa kipindi cha miaka 40. Leo hii baada ya kupata nafasi hiyo, tunashindwa kuitumia vizuri, si watu binafsi hata vyombo vya habari. Hata kuna baadhi ya watu wamediriki kusema kuwa, kwanini Rais hajalifungia gazeti hili au lile. Hii yote ni kuonyesha uchanga wa demokrasia yetu na jinsi tunavyoshindwa kutumia mianya iliyopo kwa ajili ya maendeleo. Hivi kweli ni dhambi ya Kikwete kutoa uhuru wa kujieleza kwa mimi na wewe? Hatukumbuki jinsi Mkapa aalivyopata taabu na vyombo vya habari. Kwanini tusimsifu na kufurahia hilo?
Kama kweli wapinzani wanajiandaa kutumia hizo sababu tatu kama ndio kampeni kuelekea uchaguzi 2010, basi waelewe kuwa CCM itashinda kirahisi kuliko chaguzi nyingine zote. Wakati ni huu kwa wapinzani na wapiga debe wao kubadili stesheni na kuja na sababu madhubuti zaidi, ambazo wananchi watawaelewa. Tunapenda CCM iondoke madarakani, lakini lazima tujue ni chama gani bora kitaingia madarakani. Tunahitaji chama bora, na si bora chama. Jipangeni vizuri ili msiumbuke, wakati ni huu.