Eti Dada Akikataa Kwa MbofuMbofu, Atakubali tu

LINCOLINMTZA

JF-Expert Member
Mar 15, 2011
1,639
516
Katika pilika zetu wanaume, huwa tunajaribu bahati zetu kwa wa dada mbalimbali.
Wengi kama siyo wote hukataa siku ya kwanza unapoingiza gia yako.
Baadhi katika kukataa hutoa majibu ya upole na hekima kama vile ana mtu wake.
Baadhi hujibu kwamba hawataki na kupiga kimya.
Baadhi hukataa na kufuatiwa na maneno mengi sana, kama wewe una nini, Jiangalie kama unahadhi yangu, n.k.

Watu wengi husema kwamba, anayekataa kwa maneno mengi sana huwa anaonyesha kwamba yeye siyo Maharage ya Mbeya, ili aonekama wa thamani. Kwa hiyo ukimfukuzia kwa muda, huwa wanakubali kiraisi tu na ukimwacha anaweza kuja kuuliza kama ulikuwa unamtania tu, na hukasirika sana.


Je, kuna ukweli hapo?

Nawakirisha WanaJF
 
Haya wanaume waje kutuletea vituko vyao wale walokua wazoefu na mambo hayo uwanja wenu......
 
Hiyo ilikuwa zamani, sikuizi ukinusisha pua lako tu umenasa, idume vimekua adimu, hasa ukilenga wanawake wenye age flani ambao wanaona 'jua linazama' na bado hawajapata mtu
 
Nani anatongoza siku hizi?unaomba no. ya simu jioni unampigia akija tu huyo tayari,VODACOM KAZI NI KWAKO.
 
Wakati ana kataa anajichanganya na ka udini lakini baada ya muda akah!
 
Nani anatongoza siku hizi?unaomba no. ya simu jioni unampigia akija tu huyo tayari,VODACOM KAZI NI KWAKO.
Kwani mtu akikupa namba ya simu na akaitikiwa mwaliko wako ndio kakukubali?
Nijaribu mimi uone balaa langu,nakutia hasara ya ukweli mpaka utajuta kunifahamu na hupati kitu vile vile,nyie mnaotuchukulia poa ndio nawatakeni sana nyie.
 
Ninachoamini mimi,km mtu amekupenda hakuna longo longo mnakubaliana mambo mengine yanaendelea,na kwa mwanaume muelewa wala hatakuwa na mda wakufikiria habari za mambo ya maharage ya mbeya wala nini,Tatizo liko kwenye fikra mbovu za watu wanatafsiri vibaya,na nyie wanaume mnapenda mzungushwe kwa mlolongo mrefu kumbe mnaibiwa tu ili mnase vizuri,polen sana.
 
Kukataana mpaka longo longo?Ya kazi gani?
Ni mwendo wa sihitaji, sitaki, au siko interested na wewe. Maelezo ya kwanini akatafute kwingine.
 
Kwani mtu akikupa namba ya simu na akaitikiwa mwaliko wako ndio kakukubali?
Nijaribu mimi uone balaa langu,nakutia hasara ya ukweli mpaka utajuta kunifahamu na hupati kitu vile vile,nyie mnaotuchukulia poa ndio nawatakeni sana nyie.

Utamu extra wee unaonesha upo ngangari tena kinoma.HEBU FUNGUA KA NGO ka kuwaelimisha wenzio maana huku mtaani wananasa kiulaini haswa wakifika geto tu "KWISHA HABARI YAKE" na hivi Bongo shida zimeongezeka
 
Siku hizi ni maharage ya mbeya, Maji mara moja! FaceBook na mitandao ya kijamii inatumika kurahisisha haya mawasiliano
 
Back
Top Bottom