Eti ccm imeteua mafisadi kufadhili jk 2010!

Pilipili husiyoila yakuwashia nini?Nyinyi mpo upinzani sasa kama ccm wamechagua hapo mapapa kukampenia watu wao tatizo nini/Nanyi chagueni manyangumi wa kukampeni wagombea wenu!

loh utawajua tu watu wasio na uchungu na nchii hii
 
Katika gazeti la Mwana Halisi toleo la leo no 163, lina kichwa cha habari kuwa akina, Rostam, Karamagi, Somaiya, na wengineo wamechaguliwa na Sekretariate ya CCM iliyo chini ya Uenyekiti wa Makamba. CC inasubiriwa ku-approve. Hii, imekaaje jamani. Mafisadi wanaweza kutenganishwa na hiki chama? Na je, kunadhamira ya dhati ya CCM kupambana na Ufisadi?

Mimi ningeshangaa kama wasingeteuliwa au kuwepo kwenye hizo kamati zao muhimu... kwani wao ndio mhimili wa hicho chama ..wee unashangaa wao kuwemo kwani uliposikia wana mtandao wa JK uliomsaidia kumuingiza madarakani... ulifikiri ni makabwela wa kupiga domo... nani asiyejua kuwa akina karamagi na wenzie rostam ndio waliofadhili kampeni chafu za ccm..... unaam biwa jimboni kwake karamagi alitumia zaidi ya milioni 800 kwa ajlii ya kampeni hizo za uraisi.....kwa hiyo CCM kuwaacha hao ni sawasawa ni kuweka rehani utawala wao.. ..

tatizo hakuna chama pinzani hapa tanzania kuna vyama vya ulalamishi na nivaitwa upinzani kwa mujibu wa sheria tu lakini kimantiki hakuna...

+++++++++++++++++++++++
There is Big Differeence btwn Weakness and Kindness.. i guess we are wGeeak and a little bit Kind... Let say we are suffering from HOMPHOBIA
 
Je mlikuwa mnataka achanguliwe nani ambaye si fisadi? maana kuna watu wanajifanya wasafi na wanaongoza hivyo vita vya kupambana na ufisadi lakini nyuma ya pazia ni mafisadi no.1.

yeh! sina maana kuwa walio pendekezwa ni wasafi!
 
Kwa maneno mengine kwenye chama chao hakuna aliyemsafi?!
 
Pilipili husiyoila yakuwashia nini?Nyinyi mpo upinzani sasa kama ccm wamechagua hapo mapapa kukampenia watu wao tatizo nini/Nanyi chagueni manyangumi wa kukampeni wagombea wenu!

Kama wewe haikuwashi wengine inatuwasha. Keki ya Taifa igawanywe kwa wachache tena wale wale, wewe unabakia na misemo ya kukata tamaa na isiyo na tija! Nani kakuambia tunajadili mambo ya upinzani hapa, soma mada na mtririko wa wanaojadiliwa ndipo utajua kuwa hiyo pilipili tayari imekwisha kukuwasha ingali shambani!
 
Mie naona waliochaguliwa ndio wanaostahili kuhakiksha kuwa JK anarejea madarakani. Hawa ndio walishiriki ipasavyo kumwingiza madarakani, na wasiposhirikishwa kuhakikisha kuwa anabakia madarakani, basi watamuondoa madarakani!

KIPI BORA?
 
bado hamuamini uswahiba wa jk na hawa ndugu? yaani mnategemea siku moja jk awatose? ''TUNADANAGNYIKA''
 
muda wote tumesema sisi ccm tuacheni jamani.....kama mnaona tunafaidi subirini zamu yenu.....tutawadanganya hivi hivi tutajifanya tumepeleka watuhumiwa mahakamani lakini hatuwafanyi chochote na huu ni mpango wetu tutahakikisha wanashinda kesi watadai fidia tutawalipa tutagawana..mtatufanya nini......dua la kuku halimpati mwewe.....na aliyeko juu mngoje chini uone kama atashuka...
 
Hatuwaachi, tutaendelea kukomaa nanyi mpaka kieleweke. Huoni Visiwani mambo yanaanza kueleweka!
 
Mimi naamini kuwa jmk aliteuliwa ili kuwe na mabadiliko nayo yapo njiani yanakuja, atakabidhi madaraka kwa mtu mwingine baada ya kukubali kwa hiari kuwa kashindwa kwenye uchaguzi Mungu tuokoe hapo ifikapo uchaguzi 2010, wape uelewa watu wako wanaoteseka, tunajua hutatutupa twakuomba mwenye mamlaka kuliko vyote
 
mimi naamini kuwa jmk aliteuliwa ili kuwe na mabadiliko nayo yapo njiani yanakuja, atakabidhi madaraka kwa mtu mwingine baada ya kukubali kwa hiari kuwa kashindwa kwenye uchaguzi mungu tuokoe hapo ifikapo uchaguzi 2010, wape uelewa watu wako wanaoteseka, tunajua hutatutupa twakuomba mwenye mamlaka kuliko vyote

ombea kwanza wasimamizi mungu awapige upofu waachane na kufanya uhuni wao dhidi ya ccm
 
NILIANDIKA ASUBUHI CCM MTAWATAMBUA KWA VITENDO...SASA KAZI IMEANZA

RAIS Jakaya Kikwete amerudia kuvionya vyombo vya habari nchini visitumie uhuru wao kuvuruga amani na kuvunja umoja wa kitaifa.

Rais Kikwete amesema, endapo vitafanya hivyo Serikali haiwezi kuviacha,vitashughilikiwa.

Sanjari na onyo hilo, Rais Kikwete amesema, Serikali itaendelea kulea na kudumisha uhuru wa vyombo vya habari.

Lakini Rais Kikwete amesema,vyombo vya habari lazima vijirekebishe,vitimize wajibu ambao ni sehemu muhimu ya uhuru huo wa habari.

“Kama nilivyowaambia pale Musoma majuzi wakati wa kuadhimisha miaka 10 ya kifo cha Mwalimu Nyerere, huu hauwezi kuwa uhuru wa kuvunja taifa, uhuru wa kugawa watu, uhuru wa kuchochea maasi na ugomvi kati ya dini mbalimbali, kati ya makabila, kati ya watu wenye rangi mbalimbali”

Alisema “Baadhi ya vyombo vyetu havina wajibu kabisa. Vinachochea maasi ya kuvunja nchi na kuleta mfarakano kati ya watu wetu. Vinajaribu kugawa watu wetu, kugawa mataifa yetu na kusababisha maafa makubwa. Hatuwezi kuvumilia vyombo vya habari vya namna hiyo vinavyotumia uhuru kuleta balaa kwa watu.”
 
ombea kwanza wasimamizi mungu awapige upofu waachane na kufanya uhuni wao dhidi ya ccm

Hao wasimamizi si wameteuliwa pia na hao CCM? Mabadiliko yanakuja, tena hayako mbali ni swala la muda tu! Tuombe uzima ili tuyaone.
 
Back
Top Bottom