Eti ccm imeteua mafisadi kufadhili jk 2010!

Kyachakiche

JF-Expert Member
Feb 16, 2009
983
207
Katika gazeti la Mwana Halisi toleo la leo no 163, lina kichwa cha habari kuwa akina, Rostam, Karamagi, Somaiya, na wengineo wamechaguliwa na Sekretariate ya CCM iliyo chini ya Uenyekiti wa Makamba. CC inasubiriwa ku-approve. Hii, imekaaje jamani. Mafisadi wanaweza kutenganishwa na hiki chama? Na je, kunadhamira ya dhati ya CCM kupambana na Ufisadi?
 
Sikio la kufa halisikii dawa. Hivi kama CCM ikifa kutatokea nini? Mbona KANU huko Kenya, UPC huko Uganda na UNIP huko Zambia haziko madarakani na nchi zinasonga mbele? Bila CCM kuondoka madarakani Tanzania itabaki hivi hivi. Hakuna jipya CCM.
 
Mimi sielewi kama sisi Watanzania tuna matatizo ya kusahau au tunadharau. Wote waliotuzunguka wamebadili vyama tawala, kwanini sisi tunang'ang'ania?????
 
Katika gazeti la Mwana Halisi toleo la leo no 163, lina kichwa cha habari kuwa akina, Rostam, Karamagi, Somaiya, na wengineo wamechaguliwa na Sekretariate ya CCM iliyo chini ya Uenyekiti wa Makamba. CC inasubiriwa ku-approve. Hii, imekaaje jamani. Mafisadi wanaweza kutenganishwa na hiki chama? Na je, kunadhamira ya dhati ya CCM kupambana na Ufisadi?

wewe ndo unawaona mafisadi wenzio wanawaona lulu kweli hao..ndo maana mnamuudhi kweli mkuu wa kaya mnapowataja taja..hahaaaa yale yale ya kelele za mwenye nyumba hazimnyimi usingizi mwenye nyumba
 
sioni cha ajabu muulize kibunango .....
sasa kama hao ndio waliomwingiza madarakani kwa nini wasimsaidie 2010
kila la kheri
 
Katika gazeti la Mwana Halisi toleo la leo no 163, lina kichwa cha habari kuwa akina, Rostam, Karamagi, Somaiya, na wengineo wamechaguliwa na Sekretariate ya CCM iliyo chini ya Uenyekiti wa Makamba. CC inasubiriwa ku-approve. Hii, imekaaje jamani. Mafisadi wanaweza kutenganishwa na hiki chama? Na je, kunadhamira ya dhati ya CCM kupambana na Ufisadi?

Mkuu, heshima mbele, hebu tuwekee habari kamili, maana sisi wengine tuko mashambani kulipata gazeti hilo mpaka baada ya wiki.
 
jamani hawa watu awashikiki
kama mkulu mwenyewe anawaalika kwenye hafla muhimu;unafikiri wameenda kumuangalia MO IBRA??kila jambo na wakati wake nahisi CCM wameanza kusoma nyakati wajiandae mapema...kibu tupo pamoja???vile vyeo vitamu ukivipata jamani asalaleeeeeeeeeeeiiiiiiiiiii
 
mkuu, heshima mbele, hebu tuwekee habari kamili, maana sisi wengine tuko mashambani kulipata gazeti hilo mpaka baada ya wiki.

ushawahi kusikia ccm inaprove kwenye magazeti...subirini vitendo ndipo mtawajua wakoje....hapo no comments no prove
 
sioni cha ajabu muulize kibunango .....
sasa kama hao ndio waliomwingiza madarakani kwa nini wasimsaidie 2010
kila la kheri

Kama ni kweli basi hicho ndio kielelezo cha Jakaya kuhusu upande anaounga mkono katika vita hii dhidi ya Rushwa na ufisadi nchini!! Haingii akilini kuwateua hawa wezi kukutafutia eti fedha za kuingia IKULU 2010; wakakutafutie wapi, wakatuibie pesa yetu toka BOT tena? Au safari hii watatuibia pesa yetu toka TIB kwa NONI? CCM acheni kuwatukana wadanganyika!
 
Mdogo wangu nnape jamani wamemsahau???hapa akitaka draw lazima amix
 
hao mbona ndo wanachama Imara wa CCM!!! Apewe nani kazi hiyoo muhimu kwa chama??

Labda wamwongeze na Mengi aliyejulikana majuzi kuwa Mwanachama wao...
 
Kazi kweli kweli...mi nahisi soln ya hapo ni sisi kujipanga
kama wana rostam na sisi tutafute wakina mwanakijiji,mpwa masa,invis,firstlady 1,na wengineo tukomae nao hao
 
Pilipili husiyoila yakuwashia nini?Nyinyi mpo upinzani sasa kama ccm wamechagua hapo mapapa kukampenia watu wao tatizo nini/Nanyi chagueni manyangumi wa kukampeni wagombea wenu!
 
Kama ni kweli basi hicho ndio kielelezo cha Jakaya kuhusu upande anaounga mkono katika vita hii dhidi ya Rushwa na ufisadi nchini!! Haingii akilini kuwateua hawa wezi kukutafutia eti fedha za kuingia IKULU 2010; wakakutafutie wapi, wakatuibie pesa yetu toka BOT tena? Au safari hii watatuibia pesa yetu toka TIB kwa NONI? CCM acheni kuwatukana wadanganyika!

Pesa ya wadanganyika iliyozuiliwa DECI inawatosha CCM kufanyia kampeni.
 
Katika gazeti la Mwana Halisi toleo la leo no 163, lina kichwa cha habari kuwa akina, Rostam, Karamagi, Somaiya, na wengineo wamechaguliwa na Sekretariate ya CCM iliyo chini ya Uenyekiti wa Makamba. CC inasubiriwa ku-approve. Hii, imekaaje jamani. Mafisadi wanaweza kutenganishwa na hiki chama? Na je, kunadhamira ya dhati ya CCM kupambana na Ufisadi?
Ni aina nyingine ya Udaku.....
 
hahaha ila kibunango ana siri kubwa ya Chukua chako Mapema ...anafaidika hapo maana kasema yeye ni CCM damu
lakini tukirudi kwenye mada mbona hiki chama kina mambo ya viini macho sana ???????????
 
Kazi kweli kweli...mi nahisi soln ya hapo ni sisi kujipanga
kama wana rostam na sisi tutafute wakina mwanakijiji,mpwa masa,invis,firstlady 1,na wengineo tukomae nao hao

teteteteh pdidy ndoto za kuelekea kwenye uchaguzi
 
Back
Top Bottom