Eti binti huyu ni mzuri, kwa vigezo gani…………………!?

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
chanel_red.jpg

Kuna msemo kwamba uzuri huwa uko kwenye jicho la mtazamaji, sio kwa yule au kile kinachotazamwa. Bila shaka msemo huo una ukweli kidogo. Kwa nini? Kwa sababu watafiti wengi wa masuala ya saikolojia ya upendo wana ugunduzi tofauti.

Wanasema wamebaini kwamba, kunakuwa na makubaliano, yasiyo rasmi katika jamii kuhusu uso mzuri au mbaya. Ina maana kwamba, pamoja na kuwa, kila mtu ana namna yake ya kupima uzuri wa sura, bado kuna ule uzuri unaopangwa na jamii. Taarifa mbalimbali za utafiti, ukiwemo utafiti uliofanywa na jarida la Experimental Psychology; Human Perception and performance, zinaonesha kwamba, msemo huo wa zamani una nguvu yake, lakini siyo kwa asilimia mia moja.

Ni kama vile una nguvu nusu, na hili la jamii kuwa na vigezo vyake vya uzuri wa uso lina nguvu nusu.
Hii ina maana gani? Kwamba unapoona mtu fulani ni mzuri au mbaya wa sura, ujue hapo kuna maono yako nusu na maono uliyofundishwa na jamii kuhusu uzuri, nayo ni nusu.Ndio maana kwa hali hiyo, unaweza kukuta idadi kubwa ya watu mahali wakasema fulani ni mzuri au mbaya.

Kama ingekuwa uzuri na ubaya uko kwenye macho ya mtazamaji, yaani yeye ndiye anayeamua siyo kile kinachotazamwa, basi kungekuwa hakuna mahali ambapo, watu wengi wangeunga mkono kuhusu uzuri au ubaya wa sura ya fulani.
Kuwepo kwa hali hiyo, kunaonesha kwamba, jamii nayo, bila kuambiana au kufanya vikao, inakuwa tayari ina vigezo vyake kuhusu uzuri. Hiyo ipo kila mahali duniani. Kila unapoenda utakuta watu wanahesabu uzuri au ubaya kwa vigezo fulani.

Mara nyingi utakuta watu wengi wanasema mtu fulani n mzuri au mbaya, lakini utakuta watu wengine wanatofautiana na hao kwa kiasi fulani. Hawa ni wale ambao wanatumia upande ule mwingine wa mtu binafsi katika kuamua uzuri au ubaya………….Sasa mmeelewa eh!
 
Mkuu.
Kwa ninavyoamini mimi kila kitu huwa kinakuwa analyzed kwa kutumia vigezo fulani (criteria, perspectives, standards etc). ..mfano ili useme fulani ni tajiri lazima uwe na vigezo fulani inaweza kuwa pesa, idadi ya ng'ombe, wanawake , majumba n.k..
Halikadhalika linapokuja suala la kusema huyu ni MZURI..tunarudi palepale ..vigezo!!!
Tatizo huwa Je? vigezo unavyotumia wewe na mimi navikubali??..Ukisema Jamii imevikubali..nitakuuliza jamii ni nani na nani??..mtiririko utakuwa mrefu na mwisho wa siku tutarudi palepale tu kuwa jamii ni wewe na mimi..
Ndiyo maana hata akina Lundenga wanapochagua msichana mzuri wa Tanzania (Miss Tanzania) huwa wanakuwa na Majaji..jiulize je wale majaji wanapoweka marks kwa kila kigezo ..huwa wanaongozwa na 'jicho' lipi??..na kwa nini asiwe jaji mmoja badala yake huwa wanakuwa wengi??..Na kwa nini bado huwa tunalalamika kuwa aliyeshinda hakustahili provided vigezo vipo wazi???....Nadhani nakupenda kuko hivihivi...mzuri kwako..kwangu mbaya!!!
 
Nakubaliana na wewe mkuu, lakini jambo moja ambalo hata mimi nimejifunza katika utafiti huu, ni kwamba, mara nyingi jamii imekuwa ikiratibu maamuzi yetu kwa kiasi kikubwa. si huo uzuri au ubaya tu, bali pia hata katika mambo mbalimbali kuhusu maisha yetu, kuna mchango lau kidogo kutoka katika jamii. kila mtu kabla ya kuifayna jambo lazima atajiuliza kwamba jamii itamfikiriaje au jamii itapokeaje maamuzi yake............... yaani kila mtu anafanya maamuzi kwa kuangalia kama maamuzi yake yatapokelewaje na jamii. The Boss aliwahi kuuliza hapa JF wakati fulani kwamba ni yupi mwenye maamuzi ya kiuanamume, kati ya yule anayemuoa mwanamke anayesemekana ni malaya lakini amempenda sana na ana matarajio makubwa katika uhusiano huo au kuoa mwanamke ambaye hajampenda lakini anavyo vigezo vyote vinavyokubalika katika jamii, mzuri, msomi, mtanashati na ana kazi nzuri, lakini moyo wake haupo kwa huyo mwanamke ila jamii inaonekana kushabikia uhusiano huo.........
Nakumbuka maoni yalikuwa ni mengi na sehemu kubwa ya maoni yalionekana dhahiri kumtenga huyo anayesemekana ni malaya.............
 
Nakubaliana na utafiti huu, kuna ukweli mkubwa kuliko inavyofikiriwa
 
Nautafuta huo uzi wa The Boss ulioutaja hapa naomba link tafadhali
 
Last edited by a moderator:
Hivi kila siku ni kujadili tuuuuuuuuuuuu uzuri wa mwanamka eh?

Mbona its so boring jamani.
 
Hivi kila siku ni kujadili tuuuuuuuuuuuu uzuri wa mwanamke eh?

My Dear ayanda, usiboreke mama!!

Anzisha tu thread ya kujadili uzuri wa Muhogo na Nyanya Chungu, pia tutachangia pia na itapata wengi wa kuunga mkono

Kuna wengine thread hii ni very useful kwao so usimkatishe tamaa muanzisha thread wala wachangiaji wengine

Ni mtazamo na maoni yangu tu
 
ah watu daily uzri uzuri ili iweje? wnegine wanakuja humu na mikasfa kibao ya kuwakashifu wanawake! kisa nini?

mi nadhani ni bora tungejadili vitu ambavyo ni owns making, sasa kila kukicha ni kujadili mambo ambayo Mungu ndo mwamuzi na ndiye aliyeumba inasaidia nini? Anyway, mi huwa sipendi kumkosoa Mungu kwa hiyo nyie endeleeni na ujinga wenu.
 
Hebu taka watu radhi dada yangu kwa kutuita wajinga...sio kila usichokipenda kinakupa wewe tiketi ya kuwaita wengine wajinga

Hakuna anaemkosoa Mungu....Mungu huyo huyo unaetaka kusema humkosoa katika maeneo mengi kwenye Biblia (kama wewe Mkristo) anatumia neneo "alikuwa mzuri wa sura....alikuwa mzuri wa Umbo".......(Angalia Mwanzo 29:17 juu ya Habari ya Raheli, Esta 2:7 juu ya Binti Hadasa/Esta, Mwanzo 24:17 juu ya Rebeka binti Mrembo na pia kama wewe ni Mwislam nimesoma hii article inazungumzia pia juu ya uzuri wa mtu Sira- Ukhalifa wa Sayyidna Aliy bin Abi Twaalib).....So I think there is no way you can stop people talking about it

Angalia vizuri original post na mawazo ya wachangiaji utaelewa nini kinaendelea...sio tu kusoma heading na conclusion kufuatia

Kuna mambo mazuri yanayoweza kuwafaa hata hao unaoona wanatoa "mikasfa" kibao
 
sasa niambia nini faida ya kujadili uzuri wa mwanamke? eti sijui demu hana wowowo sijui jeusi kama mkaa! mnataka nini
 
Back
Top Bottom