Eti bei ya mafuta ya taa iwe sawa na petrol

akili mu kichwa watanzania wenzangu,badala ya kudhibiti mwizi tunamfunga aliyeibiwa ili asiibiwe tena.kichekesho kiko hapa.anaye chakachua atplani mpango mwingine baada ya mafuta ya taa kupanda.mfano akianza kuchanganya na maji itabidi ewura wawaambie dawasa wapandishe maji yalingane na petrol,je tutadhibiti vipi mto ruvu na mingine mingi na visima vilivyojazana nchi nzima au tutaongeza polisi wa kulinda maji?ewura wajibikeni acheni mambo ya ajabu.naomba mungu mgombea binafsi aruhusiwe muone.
 
Ukimkuta kiongozi anashauri njia ya mkato namna hii ya kumaliza tatizo la mafuta machafu ujue ana matatizo ya akili na ni dalili tosha kwamba yeye pamoja na vyombo husika wameshindwa kazi. Sijui waTZ tunataka ushahidi gani kujua kwamba serikali iliyo madarakani imeshindwa KAZI na inatakiwa ipewe mapumziko ya milele.
 
Naungana na wote ambao wanawaona hawa EWURA kama watu wasiokuwa na akili timamu kwa kitendo cha kutoa wazo la kuongeza kodi.

Ilikuwa inatakiwa hawa EWURA wote waondolewe madarakani kwani kazi yao ni kupanga bei ya mafuta na kutoa mapendekezo ya kipuuzi huku magari ya watu yakizidi kuharibika na mazingira yakichafuliwa na mchanganyiko wa diseal vs kerosene na petrol.

Kwa upande mwingine hawa TBS nao wanasemaje kuhusu hili maana wanakalia kuvamia madukani mitaani lakini wachachuaji wameachiwa tu wakipata faida kubwa huku magari ya watu yakiharibika.TBS wazee wa viwango ingilieni kati ili kuliokoa taifa.

Na Nyie EWURA mkithubutu kupandisha bei ya mafuta ya taa mjue sisi walala hoi ndio tutaumia zaidi sio wachachuaji.
 
Ukimkuta kiongozi anashauri njia ya mkato namna hii ya kumaliza tatizo la mafuta machafu ujue ana matatizo ya akili na ni dalili tosha kwamba yeye pamoja na vyombo husika wameshindwa kazi. Sijui waTZ tunataka ushahidi gani kujua kwamba serikali iliyo madarakani imeshindwa KAZI na inatakiwa ipewe mapumziko ya milele.

Mkuu Ulisemalo si kwamba ntakupinga saaaana hapa na bali sio kuwa anamatatizo ya hakili unajua inafika sehemu serikali ina wa lazimisha baadi ya viongozi kuongea njia zingine za mkato kama hizo kwa nini n ni kuwa Serikali yetu ina desturi ya kutosikiliza ushahuri wa kielimu kwa faida ya wananchi wake na matokeo yake inashindwa hata kusimamia MUSTAKABARI WA NCHI katika nyanja zote za kiuchumi, sheria zatungwa utekerezaji ni mbovu usipime yani mambo wanayapeleka kihohehae ilimradi twaenda na watu wanakula basi hatuoni hizo sera zao zikileta maendeleo na kitu kinacho wasumbua wananchi ni kila budget ipitapo hai leti faida wala haisomewi mapungufu yake kabla ya budget nyingine ya mwaka ipitishwe tena

Sasa kama hao wadhibiti wa mafuta nishati na vinginevyo kweli wananguvu kisheria na kikatiba katika utekelezaji wa kazi zao isije ikawa wanafanya tuuu kazi kwa matakwa ya watu fulani na kufuata orders, na hili ni tatizo kubwa sana kama EULA nadhani ndivyo waitwavyo kwa kifupi kama nimekosea mtanirekebisha hapo walipaswa wawe very serious na kitengo hicho si kwa Dar tu hata mikoani na ndiko huko wanchi wengi nao wako na uchumi wao ni mdogo sana, tusi implement hizo sheria kwa watu wa dar tu jamani ati ndiko kuonekane kuna control na ndivyo hivyo tuichukulie kama mfano kuwa ndivyo itendekavyo mikoani that's nonsense,

Lazima hizi taasisi zije na mikakati bora kwa wananchi na kulitekeleza kero za wananchi kwa kusimamia sheri na katiba zao wazitungazo na kuwajibika ipasavyo.

Leo upandisha bei ya mafuta iwe sawa na Petrol ili ku equalize mambo na ili kuwazuia watu wasi chakachue mafuta????? huu ni uzembe wa viongozi wasimamizi tokea mafuta yaingiapo na yapitako kwenywe vituo vinavyo hakiki mafuta huko njiani na pale yaingiapo mkoa husika yapelekwako kama hawasimamii basi hilo jambo la kuchakachua halitokwisha kaaeni mkijua hivyo.

Pia kuwepo na ile biashara huria mwiitayo kila mtu anajifikishia mafuta kwake jamani hii bila kuwa na chombo kimmoja tu chakusafirisha hayo mafuta imekula kwetu mazimaaa hatuna ustaarabu hata kama tuweke mikakati vipi sijui ije itokeee watu wachache wazalendo na kuifanya hiyo kazi iatawezekana,


 
Kwa hiyo wameona kuwa kwa vile magari ya rais yamegoma kuwaka kisa mafuta ndio wananchi waingie gharama kwa mgongo wake?

Hii si mara ya kwanza kwa taifa hili kuchukua hatua ambazo ni reactive baada ya maafa kutokea tena yakimhusu mkuu wa nchi. Huku ni kukosa kuwajibika. Suala la kusema eti wafanyabiashara wa mafuta wanachanganya mafuta pia ndio iwe kigezo cha kuyapandisha bei?

Hawana takwimu ni idadi gani ya watanzania wanaotumia haya mafuta kwa shughuli za nyumbani? Hawawezi kuoanisha haya mawii - idadi ya watanzania wanaotumia mafuta na hasara inayopatikana katika kuchanganya mafuta na kuja na mbinu ya kukabiliana na hilo? Watuambie kuwa wanataka kuitangaza gesi na si vingine.

Sina maneno ya kutosha kuzungumzia hili...
 
Ni uzembe tu wa idara za serikali zinazohusika. ugoigoi wa EWURA, wizara unafanya wafanyabiashara watumie nafasi hiyo.

Waziri angekuwa Magufuli, Mrema au anayefanana nao, tatizo hilo lingekuwa history.

Serikali imeshindwa jukumu lake la msingi la kudhibiti wezi, mafisadi, wahujumu uchumi nk. ikimaanisha labda wahusika wanashirikiana na watendaji wa serikali.

Maelezo mengine kama kupandisha kodi ya mafuta ya taa hayaingii kwenye akili ya mtu wa kawaida.

Tujiulize swali moja rahisi, kuna tofauti gani kati ya kuwepo au kutokuwepo kwa EWURA?
EWURA inapaswa isiwe mzigo kwa wananchi bali kuwasaidia.
 
Ewura wamesalimu amri kwa wafanya biashara wa mafuta, especially moshi na arusha ambako inaaminika zaidi ya asilimia 50 ya vituo huuza mafuta yaliyochanganywa. Sasa hapo ni kutafuta njia nyingine mbadala.
 
Ni muda sasa watanzania waamke kwani serikali iliyomadarakani kwa kweli imeshindwa kazi rais wetu jk for sure uwezo wake ni mdogo sana ame loss control ila c laumu sana kwani yeye ni mtu wa pwani na watu wa pwani kazi wao hawajui ni kukaa tu barazani na kunywa kahawa maswala ya pesa hawajui ni muda sasa umewadi kumpiga chini kwani hawezi uongozi rais gani hana kauli ya command kila leo vitu vinapanda bei anacheka 2 alipochaguliwa sukari kilo ilikuwa 600 leo hii imekuwa mara 2 zaidi ni muda sasa watz tufanye mapinduzi ya kweli tuache unafiki
Naungana na wote ambao wanawaona hawa EWURA kama watu wasiokuwa na akili timamu kwa kitendo cha kutoa wazo la kuongeza kodi.

Ilikuwa inatakiwa hawa EWURA wote waondolewe madarakani kwani kazi yao ni kupanga bei ya mafuta na kutoa mapendekezo ya kipuuzi huku magari ya watu yakizidi kuharibika na mazingira yakichafuliwa na mchanganyiko wa diseal vs kerosene na petrol.

Kwa upande mwingine hawa TBS nao wanasemaje kuhusu hili maana wanakalia kuvamia madukani mitaani lakini wachachuaji wameachiwa tu wakipata faida kubwa huku magari ya watu yakiharibika.TBS wazee wa viwango ingilieni kati ili kuliokoa taifa.

Na Nyie EWURA mkithubutu kupandisha bei ya mafuta ya taa mjue sisi walala hoi ndio tutaumia zaidi sio wachachuaji.
 
Watz wengi wnaumia sana kwa hali halisi ya kiuchumi kwenye nchi yetu but wengi wao ni wanafiki na hawana umoja, kwa kuongea watz tupo sana lakini vitendo hamna angalia mfano mzuri kwenye soka watz wanajua sana mpira kwa maneno mtu anaweza kukupangia timu ya manu kikosi kizima, but kwa vitendo hamna kitu hiyo kikubwa kinachotugharimu hata kwenye siasa kitu ambacho kwa nchi za wenzetu kama kenya wako real tz wengi wetu kwa sasa ni wa somi ila msomi wakitanzania na ambaye hajasoma ni same upeo ni mdogo sana.

Tuamke watz tuache ushabiki na tuwe na umoja na maamuzi CCM si chama cha kurudi madarakani tena
 
kwa hali hii wengie tutahamia kwenye mishumaa ,,kuna hatari ya mishumaa nayo kupanda bei ..Tanzania jamani..EWURA ...
 
na hao UWURA wababaishaji eti na wao wanasapoti unajua wenzetu hawana shida watu hawajatembea nchi hii unaweza ukaenda mahali siku mbili hakuna umeme,kuna vijij watu wake hawajui hata umeme maana yake ni nini?leo uwapandishie kodi kisa uchakachuaji.Wanaochakachua si wanajulikana kwa nn wasikamatwe au ndio walewaleeeeeeeeeeeeeeee! kuweka kodi sio suluhisho suluhisho ni kutafuta chanzo cha tatizo.
 
Mambo mengi yanakwenda kombo katika nchi ambayo hakuna utawala adilifu, na uliopo ni ule unaowabeba na kuwasujudia wachache, ambao mara zote ni wenye uwezo wa kiuchumi.

Kama taasisi iliyopewa mandate ya kusimamia sekta ya nishati ndiyo inapendekeza hilo, wakati huu ambapo wananchi wanalazimika kumaliza misitu kwa ajili ya kupata nishati mbadala kwa kushindwa kumudu kununua mafuta ya taa, gesi ama kukosa huduma ya umeme...ni ujuha! na ni jambo la kuchukiza sana.
 
Hapo ndy mtajua jinsi watendaji wenu walivyo WAPUMBAVU na wafinyu wa fikra!!
wanashindwa kukdhibiti wizi kisha kwa kuogopa magari yao yasiharibike basi wanapandisha bei ya mafuta ya
taa bila kujali kuwa watoto wa wapiga kura wao wanategemea mafuta ya taa kujisomea!!
 
na haya makampuni yanajulikana, kwa nini wasifutiwe leseni? napata shaka kuwa kuna WAZEE wamo kwenye hii dili, au huwa wanakula pesa.
 
MAMLAKA ya Udhibiti wa Matumizi ya Nishati na Maji (EWURA), imeunga mkono, mapendekezo ya baadhi ya wadau kutaka kupandishwa kodi mafuta ya taa kuwa sawa na ya diseli na petroli. Akizungumza na Tanzania Daima, Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, Haruna Masebu, alisema endapo kodi hizo zitakuwa sawa na zingine hatua hiyo itakuwa suluhisho kuondoa tatizo la uchachushaji mafuta.
Nadhani usugu wa tatizo hili mpaka kufikia hatua ya magari ya ikulu kuwekewa chakachua ni uthibitisho kwamba EWURA wameshindwa kutimiza majukumu yao. EWURA imepewa jukumu la kusimamia masuala ya umeme na maji.

Kama kuna mapungufu ya sheria ya sasa kwa kuweka adhabu ndogo kwa watu wanaouza mafuta yasiyo
na viwango ni tatizo hili lingeweza kutatuliwa kwa kuwa na sheria kali. Ni ukosefu wa busara kuwabebesha walalahoi wa Tanzania mzigo huu kwa kuongeza kodi ya mafuta ya taa.

Ikumbukwe 35.7% ya watanzania wanaishi chini ya kiwango cha kitaifa cha umaskini. Na kwa kiwango cha kimataifa, 57.8% ya watanzania wanaishi kwa chini ya dola 1 ya kimarekani kwa siku.

Watanzania hawawezi kumudu gharama za afya, elimu, hawana maji na sasa tunataka washindwe hata kuwasha vibatari/koroboi majumbani mwao?? Tunahitaji kuangalia madhara kwa jamii kabla ya kuja na measures kama hii inayoungwa mkono na EWURA.
 
...nikamuuliza umenunua lita 4,000 za mafuta ya taa umeyapeleka wapi...hakuwa na jibu akataka tuongee...nikaondoka
...akataka muongee, ukaondoka...basi end of story. So why telling us all this iwapo unaonekana you did nothing? Pathetic!!
 
kwa lugha nyingine unamaanisha uzembe wa ewura kuthibiti hili tatizo ubebwe na mlalahoi ili wao ewura kazi yao iwe ni kukaa tu ofisini na kupandisha bei. hivi umewafikiria watu wanao ishi vijijini kuwa mafuta ya taa ni nishati muhimu kwao, naamini huyo Mungu unaye mzungumzia sio huyu MUNGU wa upendo tunae mjua
Hujamuelewa mkuu, ameongea kifalsafa zaidi. Ni kwamba wananchi ndio wameiweka serikali hii dhalimu ilhali wakijua haiwasaidii, sasa ili waweze kujifunza na kufunguka akili ni lazima haya yatokee wakione cha moto ili wajifunze next time wasichague manyang'au hawa!
 
sasa ili waweze kujifunza na kufunguka akili ni lazima haya yatokee wakione cha moto ili wajifunze next time wasichague manyang'au hawa!

Wananchi hawastahili kubeba mzigo huu, sidhani kama wanapowachagua manyang'au walijua kuwa hii ndio itakuwa fadhila ya manyan'gau kwao. walienda na ahadi nyingi nzuri zikisema maisha bora kwa kila mtanzania yanawezekana. Walipewa Tshirt, vitenge, kanga na wale wajuaji zaidi waliambilia baiskeli..
 
Back
Top Bottom