Eti anataka tusahau yaliyopita..........

sema na moyo wako kwani uzito na umuhimu wake wewe ndo waujua .. na naamini utakuwa na maamuzi mazito na mazuri kulingana na hisia zako na si tamaa maana inaonyesha ulikuwa mvumilivu japo sijajua uvumilivu huo unatokana na nnii..

yawezekana ni darasa kwake kwa ajili ya yale yaliyotokea kwa vile hukuwa unamtimizia alichotaka kimwili , kaa nae ongea nae na msikilizane naamini mtakuwa na mwafaka mzuri zaidi ya huo ambao tutakueleza japo sie tutasaidia tu katika kupanua upeo wa kufikiri
 
Maamuzi unayo mwenyewe. Lakini tafakari kuwa alikusaliti hapo awali..... Je hatafanya hivyo tena? Huwezi kuoa mwanamke ajili ati unamwonea huruma. Kwani wewe ni BABA HURUMA. Kaa ukitafakari na umpe ulicho shuriwa iwe kama inatoka kichwani mwako. Maamuzi unayo mwenyewe.

hata baba huruma wapo mkuu,usifikiri ni wanawake tu. Na jua kuwa hata wanawake wanatakiwa kuhurumiwa pia kama wanavyotuhurumia sisi wanapogundua unanyumba ndogo nje au umezalisha nje tena baada ya ndoa.
 
mi nipo sijapotea,ni kuna wakati tu napoteza hamu na hili jukwaa, hivyo napita zaidi jukwaa la matangazo,mchanganyiko na siasa.sometimes nakuwa bored na mmu kwani kuna post nyingine zinaweza kukusababisha hata ukatenda dhambi kwa kuandika mambo ambayo siyo, hata kwa kuchangia tu.maana post nyingine kuzisoma tu ni najisi ukizichangia ndio kabisaa unajitia unajisi.
Hahaha!

Pole, uwe unapita chit chat kujifurahisha. MMU siku hizi inachuja manake watu wanapost vitu vingi havina maana mbaya zaidi vya kutunga! Mie naiona haina tofauti na chit chat, nakuwepo kujifurahisha ila sichukui serious!
 
sema na moyo wako kwani uzito na umuhimu wake wewe ndo waujua .. na naamini utakuwa na maamuzi mazito na mazuri kulingana na hisia zako na si tamaa maana inaonyesha ulikuwa mvumilivu japo sijajua uvumilivu huo unatokana na nnii..

yawezekana ni darasa kwake kwa ajili ya yale yaliyotokea kwa vile hukuwa unamtimizia alichotaka kimwili , kaa nae ongea nae na msikilizane naamini mtakuwa na mwafaka mzuri zaidi ya huo ambao tutakueleza japo sie tutasaidia tu katika kupanua upeo wa kufikiri

bahati mbaya natumia cm ningekugonea like
 
Wewe unaonekana bado unampenda!! BAYA ZAIDI HUNA MSIMAMO. Mpaka mkapata muda wa kuongea na mke wa mtu aliyechika inaonekana ni kwa jinsi gani bado ulikuwa unamuintatain. JUBU LA SWALA HILI LIPO MIKONONI MWAKO NA HAKUNA ANAYEWEZA KUKUSHAURI. HAPA UMELETA KUGIRINI WATU!!
 
Umesema vema Mr. Rocky, huyu sidhani kama amejiuliza hayo maswali manake kama angejiuliza asingekuja na huu uzi... Mwenzie katemwa ndio mana anamwona wa maana kwa sasa.

Unajua kuna mambo mengine mtu unajiuliza hivi huyu hajajiuliz amaswali haya yote kabla ya kufikia kuuliza ushauri
Maana mambo mengine yko wazi kabisa na wala hayahitaji kuangaliwa kwa darubini
 
Hahaha!

Pole, uwe unapita chit chat kujifurahisha. MMU siku hizi inachuja manake watu wanapost vitu vingi havina maana mbaya zaidi vya kutunga! Mie naiona haina tofauti na chit chat, nakuwepo kujifurahisha ila sichukui serious!

nakuunga mkono na mguu kwa asilimia mia mbili. Kuna watoto wa secondari za kata wameingilia jukwaa. Chiti chat ni kuzuri?
 
Huyo hana mapenzi ya kweli ila anataka kujificha tu kukwepa aibu na inaonesha akipata mwingine atafanya hivyo hivyo.
 
njoo chichat
kule ni stress free zone
unalipuka na jibu la kwanza linalokuja kichwani bila kuchuja

nakuunga mkono na mguu kwa asilimia mia mbili. Kuna watoto wa secondari za kata wameingilia jukwaa. Chiti chat ni kuzuri?
 
Hapa nataka niongee na wasichana na wadada.
Wasichana walio wengi(kwa mtazamo wangu bila tafiti) hupata matatizo ya kimapenzi kutokana na wao KUJIONGOPEA na KUJIPA HALI YA IMANI KUWA AT ANY TIME WATAPENDWA NA MWINGINE ni kutokana na 1.Umri wao mdogo 2.Uzuri wao wa kimwonekano 3.Elimu ya juu(atleast 1st degree).Kwa wachache wenye bahati ya kupata pesa ktk umri wa usichana na udada huathirika na hii factor ya 4.Pesa zinazomtosheleza.
Haya ni maeneo ambayo kimsingi msichana ambaye unatazamia kuwa na mume HUPASWI KUJIDAI NA HAYO MAMBO NDANI YA MAHUSIANO. Unapompata mwanamme thabiti ambaye anahitaji kutengeneza familia yenye heshma na kuskilizana na ukamletea hayo mambo ma4 HAKIKA ATAKUWEKA KANDO HATA KAMA UWEJE.
Mwishowe wasichana wengi wenye tabia kama hizi au moja wapo huwa WACHAGUZI SANA WA MPENZI na hupelekea kutopata chaguo sahihi la mme ambaye anaouwezo wa kuishi nae kwa muda mrefu.
Huyo dada ameathirika na moja au mbili ya hizo factor.
Ushauri wangu huku uki note kuwa kashakuacha twice.
1.Jiulize na ujiridhishe nafsini kuwa AMEBADILIKA?
2.Jiulize na ujilidhishe moyoni unaouwezo wa kumpenda tena.
Mapenz ni magumu ndugu si rahisi,inavyoonekana wewe ni dhahifu kwa huyo dada kwa hiyo umakini unahitajika kuamua hilo usikurupuke.
 
Unajua kuna mambo mengine mtu unajiuliza hivi huyu hajajiuliz amaswali haya yote kabla ya kufikia kuuliza ushauri Maana mambo mengine yko wazi kabisa na wala hayahitaji kuangaliwa kwa darubini

huyu bwana nadhani kajiuliza maswali na kajifanya maamuzi lakini inaonyesha hajiamini kwa kile alichoamua kwa hiyo anajaribu kuona jamii itamchukuliaje??
 
Unajua kuna mambo mengine mtu unajiuliza hivi huyu hajajiuliz amaswali haya yote kabla ya kufikia kuuliza ushauri
Maana mambo mengine yko wazi kabisa na wala hayahitaji kuangaliwa kwa darubini
Kuna watu wana roho nyepesi sana, hawawezi kufanya maamuzi magumu! Huyo mdada hakuona thamani ya mwenzie kipindi chote, anaiona sasahivi vile yamemfika! Ila ndio kama hivyo binadamu tunatofautiana sana!
 
huyu bwana nadhani kajiuliza maswali na kajifanya maamuzi lakini inaonyesha hajiamini kwa kile alichoamua kwa hiyo anajaribu kuona jamii itamchukuliaje??

True kabisa hapo na naona ndicho alichofanya
Still mapenzi kwa yule dada yapo na ndo maana ana guts za kuja kuuliza ushauri
 
Kuna watu wana roho nyepesi sana, hawawezi kufanya maamuzi magumu! Huyo mdada hakuona thamani ya mwenzie kipindi chote, anaiona sasahivi vile yamemfika! Ila ndio kama hivyo binadamu tunatofautiana sana!

Kweli kabisa wengine hatuna roho nyepesi kiasi hicho kusahau na kuona kwamba kila kitu kiko sawa
Na then unafukia mashimo unaweka lami mpya ukipita hapo kesho yake unasahau kabisa kwamba pale palikuwa na shimo
Hiyo roho wengine hatuna
Kupewa mimba na mwanaume mwingine wakati bado penzi langu na yeye halijawa na msimamo unaoeleweka licha ya yale yote niliyomfanyia na then ameenda huko ameona maisha hayaendi anarudi kuja kula matapishi yake hiyo ni ticket kuwa hakuwa na mapenzi na mimi
Na je alitegemea wakati huo wote akiwa ameolewa huyu jamaa hakuwahi kuwa na mpenzi mwingine
 
Haya mapenzi eeh ni kitu gani eeeh! (diamond sound)
Mapenzi kizungu,mapenzi kizunguzungu! (saida karoli)
Mapenzi yanarun duniaaax3 (aly kiba)
Wameimba weeeengi kuonyesha jinzi gani mapenzi hayaelezeki. Tumwachie tu kijana afenye maamuzi yake
 
njoo chichat
kule ni stress free zone
unalipuka na jibu la kwanza linalokuja kichwani bila kuchuja

nitakuja mwana,kama hata wewe mtu wa kublast upo lazima nije,libeneke la hapa mmu sometimes linanishinda mwanamalundi wangu. Wabheja khulumba!
 
Kuna watu wana roho nyepesi sana, hawawezi kufanya maamuzi magumu! Huyo mdada hakuona thamani ya mwenzie kipindi chote, anaiona sasahivi vile yamemfika! Ila ndio kama hivyo binadamu tunatofautiana sana!

huyu dada si kwamba hakuona umuhimu au thaman ya jamaa ila alikuwa amehadaika na amekuja kushtuka akiwa tayari kanasa na alifanya ustaarabu kumkwepa jamaa ili isilete mgogoro zaidi
 
Back
Top Bottom