Esther Bulaya VS Esther Wassira

Nani utampa kura yako ubunge Bunda kati ya Steven Wasira (CCM) na Esther Wasira (Chadema) ?


  • Total voters
    112
Status
Not open for further replies.
Mkuu kwenye political platform, mvuto wa sura una umuhimu sana kuwavutia watu wakufahamu au wakupende. Umesahau ya JK 2005?

Leo nilikuwa kama nimenuna mwenye hasirahasira bila sababu.Mungu ibariki JF maana nimecheka mpaka sasa nakaribia kuumwa
 
*Esther Bulaya ni mbunge wa kike, kijana kwa tiketi ya CCM viti maalum, watu wengi wamepata kumzungumzia uwezo wake wa kisiasa humu JF mara kadhaa. Ameonekana Bungeni na mara kadhaa kwenye majukwaa ya kisiasa akijenga hoja.

*Esther Wassira alionekana kwa mara ya kwanza kwenye ulingo wa kisiasa siku akichukua kadi ya CHADEMA, watu wengi walitaka kumfahamu uwezo wake wa kisiasa(kujenga hoja na kuamsha ushawishi), na kupitia hotuba aliyoitoa kwenye kongamano la kumbukumbu ya mwalimu Nyerere pale Nkurumah kila mtu sasa anaweza kumzungumzia.

*Sababu za kutaka kuwalinganisha kisiasa.
1/Mfanano wao (Wote ni wanasiasa, vijana, wanawake, wanatoka Bunda, wameshawahi kuwa na mzozo wa kisiasa na Steven Wassira, wote wanaitwa Esther!!)

2/Wanatoka vyama viwili vinavyopinzana.

3/Watu wengi wanataka kuona mmoja wao akirithi kiti cha ubunge wa Steven Wassira kule Bunda 2015.

***Wadau wa JF mnaweza kuchangia kwa kujenga hoja za ulinganifu wao kisiasa.

Wassira Ester kitu ingine kabisa mimi nilikuwa simfahamu jana nikawasha itv kusikiliza kongamano la kumkumbuka Kambarage, asalaaale binti nouma sijawahi kuona nilikuwa na kikao cha harusi nikaomba udhuru
 
Esther Wassira kwa kweli sio mzuri wa kujenga hoja tu ila hata sura anayo. Sikuwepo kwenye jukwaa la mwalimu lakini na nilimwona kwenye TV jana akanivutia sana sana learned counsel, nadhani kama vile natamani kumfahamu zaidi
hatuchagui sura tunachagua mtu mwenye uwezo wa kutunasua kwenye matatizo tuliyo nayo!
 
Esther wasira ni next level, bulaya anaachwa mbali sana. Ilikuwa mara ya kwanza kumwona esther wasira lakini nilimkubali sana. Yamkini akiwa bungeni atakuwa kama au zaidi ya halima mdee,
 
Bulaya nimemfahamu akiwa igunga kwny uchaguzi mdogo alishirikiana na Aeshi kutekeleza siasa chafu dhidi ya cdm
 
ester wassira ni mkali sana. akikuzwa vizuri ndani ya chama atakuja kuwa mwanasiasa mahiri sana. anajua kujenga hoja na anajiamini.
 
Naomba thread isomeke CDM Vs CCM nani zaidi, maana hapa ishabiki wa kochama hautaleta ukweli maana, huyo Wasira ameonekana jana tu tayari amemzidi mtu ambaye yupo ktk siasa kwa zaidi yake.
 
dada yetu yuko juu yaani jana nilimsikiliza alikuwa anajenga hoja na anajiamini kwa kile anachotoa kikubwa ni ukombozi wala si mbwembwe
 
Esther Bulaya ni mkali kwani ndani ya chama kinachoonekana kushindikana yeye anapambana na anao uwezo wa kufanya siasa ambazo ni za juu ya Itikadi ya vyama. Bulaya ni Rafiki wa Halima Mdee na kwenye baadhi ya mambo wanakubaliana lakni kwenye mambo mengine wanashindana kabisa.

Siasa za Bulaya zimepevuka sana bali wengi wetu tumenasa kwenye ule mtego kwamba "ndani ya CCM hakuna Msafi hata mmoja" na ndiyo maana mara nyingi huwa tunawahimiza watu tunaoamini kwamba ni safi watoke CCM waje CHADEMA na huu pia ni mtego wa CCM dhidi ya CHADEMA.

Huwezi kusema jambo hili liko hivi kwa kutoke mara moja tu!! Sayansi inalazimisha kwamba ili jawabu liwe sahihi ni lazima majaribio mengi yafanywe. Bulaya tumemuona mara ngapi na Wasira tumemuona mara ngapi?
 
Kwa nilivyo msikia jana tean muda wenyewe aliopewa? Hapa tuwe wawazi, hata kama mtu huwa haipendi CDM utajikuta unaipenda tu, ukweli CDM pale wamelamba Dume, dada ni mzima, anajenga hoja, ana present hoja, hana hofu na anaweza ku-join dots, Bulaya kama ana ndoto za kugombea pamoja na huyu nafikiri atakua anapoteza muda, ataabika, asipeleke timu pale, labda something to caution, kama huyo baba yake naye ataonehs interest za kugombea jimbo moja, nina hofu suala la kifamilia hapo ninaweza kumuathiri huyu binti, atakapo anza kuporomosha madongo ninahakika Steven Wassira atakosa wasikilizaji, kamati ya nyumbani then inaweza kukaa, hebu hapa Esther pamoja na CDM walifikirie hili mapema, ninahakika huyu Binti humu jamvini lazima ni member tu, sio lazima achangie but heb afikiri hili then abadiri hata jimbo, sheria zinaruhusu then pale Bunda CDM wapepeleke mtu mwingine asie na conflict of interest!
mkuu acha uoga aingie humohumo kwenye jimbo la baba yake.
 
Hata ukiwalinganisha kielimu, Esther Wassira ni jembe kwa mbali sana ukimlinganisha na Esther Bulaya. Hebu angalia ka cv ka Bulaya ni mzaha as compared to that of Wassira!
Nawasilisha!
 
Huyu Esther Wassira ndiye yule mwanabongoflava aliyewika miaka ya mwanzoni mwa 2000 au majina tu yamefanana?(Wengine hatukuuona huo mdahalo)

Umenikumbusha kitu mkuu. Nilikuwa najaribu ku-recall hiyo sura na speaking style.
Nadhani atakuwa ndiye yule aliyeshika nafasi ya pili nyuma ya Banana Zahir Ally 'Zorro' kwenye mashindano fulani ya kuimba waimbaji chipukizi (actually Banana alikuwa ameshakuwa mwanamuziki kamili hivyo ushiriki wake ulitiliwa mashaka).
Aliyechaguliwa (Banana) alienda Afrika ya Kusini kwa hatua iliyofuata ambapo alitolewa.

Nakumbuka Ester aliimba wimbo wa 'I miss you' alioimbiwa Aaliyah baada ya kufariki. Aliupatia vibaya!!
 
Umenikumbusha kitu mkuu. Nilikuwa najaribu ku-recall hiyo sura na speaking style.
Nadhani atakuwa ndiye yule aliyeshika nafasi ya pili nyuma ya Banana Zahir Ally 'Zorro' kwenye mashindano fulani ya kuimba waimbaji chipukizi (actually Banana alikuwa ameshakuwa mwanamuziki kamili hivyo ushiriki wake ulitiliwa mashaka).
Aliyechaguliwa (Banana) alienda Afrika ya Kusini kwa hatua iliyofuata ambapo alitolewa.

Nakumbuka Ester aliimba wimbo wa 'I miss you' alioimbiwa Aaliyah baada ya kufariki. Aliupatia vibaya!!


Sawa kabisa mkuu,hayo mashindano yalikuwa yanaitwa coca cola pop idol! Tena baadae alitoa wimbo kama sikosei unaitwa Sheila! Ghafla alipotea kwenye uringo wa muziki sijui alikwenda ng'ambo?
 
Japokuwa huyo wa bongoflavour simkumbuki vizuri bado sioni mfanano wowote kimaumbile wala Kiupeo kati yao.


Ha ha haaa!Mkuu kwani wa bongoflava wanaonekanaje? Mbona tunaye SUGU na Nassari wote walikuwa wanabongoflava lakini wanawakilisha vizuri tu?
 
Mi naona ni vigum kumlinganinisha Esther Wasirra na Esther Bulaya kwani, watanzania wengi wamemsikia Esther Wasira kwa mara ya kwanza jana.Na hatujui consistency yake itakuwaje,na si rahisi kudraw conclusion yake kwa kumsikia mara moja tu!!Labda tumpe muda,lakin kwa upande mwingine Esther Bulaya tunamfahamu vizuri
*Mkuu mpaka sasa Esther Wassira ameshaongea mara tatu katika matukio matatu tofauti ya kisiasa (Akichukua kadi ya Chadema, Akifafanua mzozo wa Wassira, Kongamano la kumbukumbu la Nyerere).

*Uchache wa kuongea kwenye mambo ya kisiasa angempa Disadvantage na sio advantage.

*Jambo kubwa ni ubora wa unachokiongea(Quality) na wala sio wingi wa ulichokiongea (Quantity) hivyo bado unaweza kuwapima uwezo wao kisiasa(kujenga hoja na kushawishi)
 
*Mkuu mpaka sasa Esther Wassira ameshaongea mara tatu katika matukio matatu tofauti ya kisiasa (Akichukua kadi ya Chadema, Akifafanua mzozo wa Wassira, Kongamano la kumbukumbu la Nyerere)
*Uchache wa kuongea kwenye mambo ya kisiasa angempa Disadvantage na sio advantage.

*Jambo kubwa ni ubora wa unachokiongea(Quality) na

wala sio wingi wa ulichokiongea(Quantity) hivyo bado unaweza kuwapima uwezo wao kisiasa(kujenga hoja na kushawishi)

Unasema ukweli mkuu hakuna kigezo utakachotumia wasira asiwe juu
 
hayo mashindano yalikuwa yanaitwa coca cola pop idol!

Kwa kuweka kumbukumbu sahihi, Coca cola kwa huku afrika mashariki waliendeshaga shindano linaloitwa "COCACOLA POP STAR"
na washindi wake kwa Tz walikuwa "WAKILISHA" ambalo ni kundi lilohusisha Langa, Sarah na Witness.
Ile Pop Idol ya mwaka 2003 ndiyo ilimng'arisha Esther Wasira (ambaye ndiye huyu anayejadiliwa hapa kwa upande mmoja), Terrence na Banana haikuhusika na Coca Cola.
Ni hayo tu Mkuu wangu.
Shukriyah........... Lol!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom