Establishment of the Islamic court-Mtikila

Status
Not open for further replies.

mstahiki

JF-Expert Member
Jul 14, 2007
308
5
Mtikila petitions against Kadhi court
Faustine Kapama
Daily News; Friday,October 19, 2007 @00:02
Full Salvation Church’s Rev. Christopher Mtikila has petitioned the High Court in Dar es Salaam challenging the move to establish Kadhi Court for Islamic Sharia law in Tanzania.

Rev Mtikila has asked the court to declare unconstitutional the involvement in any way whatsoever of the Ministry of Justice and Constitutional Affairs, Law Reform Commission and the Parliament in issues involving the Kadhi Court.

The High Court, according to the petitioner, should also declare unconstitutional the establishment of the Kadhi Court or separate legal systems for separate or other groups of citizens of the country.

Rev Mtikila, who is also the chairman of the opposition Democratic Party (DP), also said he had decided to seek the court’s intervention so as to protect the constitution and laws of the land against moves seeking to establish the Kadhi Court in extreme violation of the constitution.

The requests comes only a few days after the National Muslim Council of Tanzania (Bakwata) renewed its appeal for the establishment of the Kadhi Court on Tanzania Mainland during the Eid Baraza last Saturday.

Mtikila stated that the Kadhi Court was an instrument of the Islamic religion in the Holy Q’uran. Its establishment, therefore, should not involve the government and parliament as Tanzania was a circular state.

Article 26 (1) of the constitution requires every person, including members of parliament, the president and the judiciary to observe and abide by the constitution, which they swore to defend

According to the petitioner, establishment of the Kadhi Court, a separate legal system for Muslims in the country, tramples the constitution as opposed to Articles 12 and 3, which promugate human equality before the law.
 
Hili swala la kadhi nashindwa hata kuelewa kinachopingwa ama kupendekezwa ni kitu gani hasa. Ningeomba wale wanaofahamu wanisaidie hapa maanake navyofahamu mimi ni kwamba sheria yoyote mpya hupendekezwa ikiwa sheria iliyopo haiwezi kutatua mgogoro fulani...
Je ni swala gani hasa lililosababisha waislaam kuomba mahakama ya kadhi ili kuweza kutatua tatizo hilo?..Je, swala hilo haliwezi kuongezewa kifungu cha sheria zetu kama tulivyoweza kuongeza vipengele vinavyowahusu wanawake, watoto na kadhalika.
 
I'm Muslim, and what i believe Kadhi court will create misunderstanding and confusion. Who will have jurisdiction? Tanzania court or kadhi court on certain cases? I believe this works in the country were the muslim out number the christian like middle east. How will kadhi solve cases where there is two religion involve? How about those people that are born muslim but doesn't practice, are the bound to the kadhi Law's?

I know JK promise Bakwata that Kadhi will resume soon as he get into the office, however this is due to low knowledge about court system. Tanzania i guess use civil law, and Kadhi use sheria law. This two are different law. I know kadhi will deal with mirathi and other things, however for country like Tanzania where there is a lot of combine marriage this will not work.

I know Tanzania court system is a mess, but at this particular time kadhi will cause confusion and misunderstanding between our self.
 
Hili swala la kadhi nashindwa hata kuelewa kinachopingwa ama kupendekezwa ni kitu gani hasa. Ningeomba wale wanaofahamu wanisaidie hapa maanake navyofahamu mimi ni kwamba sheria yoyote mpya hupendekezwa ikiwa sheria iliyopo haiwezi kutatua mgogoro fulani...
Je ni swala gani hasa lililosababisha waislaam kuomba mahakama ya kadhi ili kuweza kutatua tatizo hilo?..Je, swala hilo haliwezi kuongezewa kifungu cha sheria zetu kama tulivyoweza kuongeza vipengele vinavyowahusu wanawake, watoto na kadhalika.

Mkandara, sheria ya ndoa ya mwaka 1970 inawapa tatizo waislamu kama inavyowapa tatizo wakristu (ingawa kwa kiasi kikubwa athari zake kama ingekuwa inatekelezwa ingekuwa kubwa zaidi kwa waislamu). Pili ni kuwa Zanzibar inayo mahakama ya kadhi kwanini hilo liwezekane wakati Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Muungano na hakuna mtu aliyewahi kudai kuwa kuwepo kwa mahakama ya Kadhi Zanzibar ni kinyume na Katiba ya Muungano?

Hivyo, Waislamu wa bara na wenyewe wanataka kuwa na mahakama ya kadhi ambayo itaundwa kwa mujibu wa sheria na kuoanishwa na mahakama ya kawaida (kwa maana ya kwamba rufaa za juu zinaweza kufika Mahakama ya Rufaa ya Tanzania). Niachie hapo kwa sasa.
 
OK, ok, ok, ok, kabla hatujaendelea, mahakama ya kadhi itahusisha hata wale waharifu wasio wafuasi wa dini ya kiislam ?
 
Kwenye masuala yasiyo ya muungano Zanzibar wana haki ya kuweka mambo yao kadri ya sheria ya katiba ya Zanzibar. Kadhi wa Zanzibar hatambuliwi na wala hana nguvu akivuka bahari nakuja bara.

Sisi wa Bara hatuna seikali ya Tanganyika, Serikali ya Tanganyika imo ndani ya serikali ya Muungano kwa hiyo sheria ya Jmauri ya Muungano inatubana.

Tuna matatizo ya sheria nyingi sana Tanzania, tukianza kutunga taratibu nyingine mpya ili kukwepa sheria zile zenye makosa tutafika wapi???

Dawa ya sheria mbovu za kiibilisi ipo tunaendele kuichanganya hapa JF si muda itakuwa ikichemshwa tayari kuwanywesha kombe zima wazee wetu wa SISIEMU, kama wanapenda au hawapendi
 
Mambo matatu ya haraka haraka:

a. Sheria hiyo ya mahakama itawahusu waislamu tu na ni wale tu ambao watataka kutatua masuala yao ya mirathi na ndoa kwa mujibu wa sheria ya kiislamu. HIvyo hata waislamu watakaotaka masuala yao yaamuliwe na sheria za nchi zisizo za kidini basi hawatalazimika kwenda kwa kadhi.

b. Mahakama ya Kadhi haitaangalia mambo mengine isipokuwa hayo mawili tu, Ndoa na Mirathi. Hata hivyo sina uhakika ni nini kitazuia kuongeza masuala mengine madogo madogo kama wizi wa kuku n.k

c. Endapo itaanzishwa kwa sheria ya Bunge mahakama hiyo itatengewa bajeti ya makadhi, ofisi zao, na wanasheria wao kutoka bajeti ya wizara ya Sheria (au Wizara itakayokuwa na dhamana ya Mahakama.

d. Hata hivyo Waislamu hawakatazwi mahali popote kujianzishia mahakama yao wao wenyewe na kuigharimia, lakini hofu yao (at least baadhi yao) ni kuwa pasipo kibali cha Bunge wanaweza kujikuta matatani.
 
Mmmmh ish, Tanzania ni nchi secular so suala hili si hata la kuzungumziwa. Mie kama muislam sioni haja ya mahakama hiyo, kwani miaka nenda rudi tumekuwa tunatatua matatizo yetu ya mirathi na ndoa tena kwenye level ya kifamilia......sasa leo mahakama ya nini? hili ni jaribio la wajanja wachache kuataka kujinufaisha kwa kupitia mgongo wa uislamu na mwisho wake itakuwa ni kuchora mstari mkubwaaa kati ya waislam na wakristo hapo nchini. Kingine ni kuwa sharia nyingi na hasa maimamu uchwara wanaozifuata kwa ukaribu ni dhurumishi kwa wanawake, na nina hisi hilo haswa ndio motive kubwa behind hiyo move. Lakini hakuna haja ya kutoka mishipa ya shingo kwani nina imani kubwa halitafanikiwa....na hata kama likifanikiwa ni waislamu wachache sana pale TZ watakao kuwa wanakwenda ktk mahakama hizo.!!
Hoja ya Mahakama ya kiislamu ishindwe na isifufuke tena...Inshallah!.
 
tukija hapa ndio matatizo ya kuonesha jinsi gani sisi tulikosea kuungana na tanganyika. si nchi ya kuungana nayo. na watachelewa sana kuendelea kwa ubinafsi na choyo cha rohoni.

hivi kenya kuna waislam percentage ngapi chini ya tanganyika wana mahakama zao na serikali inazihudumia hakuna lolote lilotokea, na wala wakristo na dini nyengine hawajapiga kelele.

uganda waislamu wako wangapi mbona hilo sio tatizo kwao, na nchi zengine za afrika mashariki na kati kongo na nnasikia burundi.

cha kuogopwa nini? ati nchi si ya kidini. hivi tanzania kuwa na balozi vertican jee si udini? mie baadhi ya wakati nnachukia sana kuungana na watanganyika maana ni wabinafsi kupita mpaka.
 
I know JK promise Bakwata that Kadhi will resume soon as he get into the office, however this is due to low knowledge about court system. Tanzania i guess use civil law, and Kadhi use sheria law. This two are different law. I know kadhi will deal with mirathi and other things, however for country like Tanzania where there is a lot of combine marriage this will not work.

The guy promised anything that would earn him more votes in regardless of the possibility, feasibility and capacity to realise the promise. He almost promised to bring down the heaven, but he is now failing in almost everything apart from earning invitation for foreign visits. Hili la kadhi mkuu pia lazima limtoe nyongo. Wala halina tofauti na swala la IOC ambalo Mwalimu Nyerere aliongoza kulikataa na likatupiliwa mbali. 2010 itafika hakuna cha kadhi mkuu wala nini, na sijui atawadanganya nini waislamu ikifika hapo. Yetu macho na masikio!
 
Hili suala la kadhi/sharia ninadhani litaleta confusion, sheria tulizonazo zinatushinda ku-inforce halafu tunataka sheria nyingine tena. Tuangalie mfano wa baadhi ya state kule Nigeria ni vurugu tupu.

Ninavyofahamu mimi waoanao kidini wanapotalakiana hufanya hivyo kwa taratibu za kidini na mirathi ni hali kadhalika.

Ninachoona hapa wanaotaka hii sheria wanataka power, prestige and access to resources.

Na huyu Muungwana aliye waahidi waislamu alifanya home work ya kutosha kuhusu hili swala au aliropoka tu kwa uroho wa madaraka? Kwanza sidhani kama hao wafadhili (wanao finance bajeti) wake watakubali...hakika hili litamtokea mapuani.
 
tukija hapa ndio matatizo ya kuonesha jinsi gani sisi tulikosea kuungana na tanganyika. si nchi ya kuungana nayo. na watachelewa sana kuendelea kwa ubinafsi na choyo cha rohoni.

hivi kenya kuna waislam percentage ngapi chini ya tanganyika wana mahakama zao na serikali inazihudumia hakuna lolote lilotokea, na wala wakristo na dini nyengine hawajapiga kelele.

uganda waislamu wako wangapi mbona hilo sio tatizo kwao, na nchi zengine za afrika mashariki na kati kongo na nnasikia burundi.

cha kuogopwa nini? ati nchi si ya kidini. hivi tanzania kuwa na balozi vertican jee si udini? mie baadhi ya wakati nnachukia sana kuungana na watanganyika maana ni wabinafsi kupita mpaka.

Msee,
You can make a good stand up comedian. Yaani mifano ya nchi zooooote hizi duniani wewe umeona Kenya, Uganda, Kongo na Burundi?? Huko Zanzibara mna mahakama za makadhi kwa miaka dahali,maendeleo yepi ambayo mnayo?? Hilo la sirikali kutoa ruzuku ndilo hasa wakina Sheikh Kanzu ibn Nanilii walitakalo, wanataka hiyo ruzuku na ku-justify sharia onevu za mirathi na ndoa......waislam hasa wa Afrika mashariki tuache kuiga upuuzi na kudili na matatizo ya kweli ktk jamii yetu, ambayo si siri kila mtu anayajua na sina haja ya kuyahainisha hapa.!! Ebo, ati mahakama ya kadhi..watu wanataka mahakama ya kadhi au wanataka kupata kazi!!?, maana zile chenji kwenye vibaraghashia hazitoshi kununulia mchuzi wa samaki. Hiyo bajeti ya "kasungura" ambako hakatoshi pia na makadhi humohumo si itakuwa balaa!!!. Haya endeleeni na li-Tanzania lenu maana naona mnazidi kuli-complicate kula kukicha.
Na nyie wa huko visiwani kajiungeni na Kenya maana ni nchi nzuri saaaaaaaaaaaana kwasababu tu wana mahakama za makadhi!!!. Kazi kweli ipo.
 
watu wanachoyo tu, tatizo sio bajeti, tatizo sio pesa. kama kutatua matatizo ni kwa wananchi wote. wawe waislam na wawe wasio waislam. kila raia apewe haki yake.

ss zanzibar tuna mahakama za kadhi dahari na tuna mahakama za secular dahari na nnategemea si mgeni kuelewa historia ya sheria na zanzibar. maswala ya ndoa na mirathi yanaenda vizuri tu. na mtu akijiona yeye hataki kwenda mahakama ya kadhi ruhusa kwenda mahakama nyenginezo. kinachotakiwa ni mahakama ya kadhi kutambuliwa kikatiba ili iwe rahisi kuendana na sheria za nchi pale rufaa inapokatwa kwa mlalamikaji bila ya hivyo mahakama hiyo haitakuwa na pa kusimamia.

kenya, uganda na tanzania ni nchi jirani na zina mazingira ya kufanana sasa kungekuwa na matatizo yangejitokeza huko. kutoa ruzuku kwa mahakama ya kadhi kwa kuwahudumia watanzania pia si tatizo.

tatizo lako ni nini hasa ? pesa au nn? jee hao waislamu hawatoi pesa?

sisi zanzibar tunajua hasa matatizo tulionayo yanatokana na ubinafsi na roho mbaya za wenzetu. tuwe wa kweli mna matatizo sana. mie nnasoa hapa nnaangalia mara kenya hawafai kuungana na ss kwa kuwa wakabila mara uganda hivi mara rwanda vile. utazani nynyi tanganyika mko perfect.

tuachane mambo ya ubinafsi, pahala penye ubinafsi na roho za fiiy hakuna maendeleo.

nnaamini wako watanganyika wenye uelewa na kufahamu kuwa tatizo la tanganyika ubinafsi na choyo.
 
Tatizo si idadi ya Waislamu Tanzania,tatizo ni sheria ndani ya katiba ya Tanzania.

Hizo serikali za Uganda na Kenya sijajua kama katiba za nchi zao zinasema serikali zao hazina dini.

Huko Zanzibar kinadharia serikali ni ya kiislamu, kwa mfano mtu akikutwa anakata Bondo wakati wa Mfungo wa Ramadhani ni Nongwa kweli kweli wakati huku Bara kukazia Swaumu wakati wa mfungo ni kheri tupu.

Ninyi kama mnataka Mahakama ya Kadhi anzisheni tu lakini msiingize udini kwenye katiba yetu tukufu isiyifungamana na dini yeyote duniani.

Kama mnataka pochi ya kuendesha hizo mahakama zenu za kadhi pigeni harambee tutawachangia tu.
 
Mtu wa Pwani I beg your pardon, umesema kwamba Kenya na Uganda wana Kadhi`s court?

Na kwa taarifa yenu wana JF hakuna nchi Africa (with exception of Ghana) yenye sheria nzuri ya ndoa kama Tanzania. Kama jamaa alivyosema hapo juu, we are just likely to bring confusion. Ningewashauri wote wanaotetea kuanzishwa kwa hii mahakama waweke ushabiki na hamaki pembeni wafanye research! wajiulize leo bajeti ya mahakama bongo ni kiasi gani, wajiulize jinsi mahakimu wanavyoamlia kesi chini ya miti huko vijijini nk harafu waniambie serikali itamudu vipi kuhudumia huo utitiri wa mahakama wanazotaka zianzishwe!

Well, watu wana haki zao lakini kwa maoni yangu sheria yetu ya ndoa ina vifungu vingi sana vinavyowatetea waislamu na wala sioni wanapopwaya unless tuu wanaitaka hii mahakama just for the sake wawe na mahakama!

All the best katika harakati zenu!
 
sasa ilikuwaje serikali ikavunja jumuia ya waislam ya afrika mashariki na kuunda bakwata? hapa hamkupiga kelele ila la kadhi linawachoma eeeeeeeeeeeeeeh
 
Watanzania,
Hii kasi ya kubomoa mihimili yetu ya amani na utulivu ni ya nini hasa? Hivi tunaelekea wapi? Niliwahi kusikia kuwa Mahakama ya Kadhi halikuwa liliingizwa kwenye manifesto na wajanja wachache, ilikuwaje? Taifa lipo hatarini na linaelekea kuzimu ndugu zangu.
 
Mambo matatu ya haraka haraka:

a. Sheria hiyo ya mahakama itawahusu waislamu tu na ni wale tu ambao watataka kutatua masuala yao ya mirathi na ndoa kwa mujibu wa sheria ya kiislamu. HIvyo hata waislamu watakaotaka masuala yao yaamuliwe na sheria za nchi zisizo za kidini basi hawatalazimika kwenda kwa kadhi.

b. Mahakama ya Kadhi haitaangalia mambo mengine isipokuwa hayo mawili tu, Ndoa na Mirathi. Hata hivyo sina uhakika ni nini kitazuia kuongeza masuala mengine madogo madogo kama wizi wa kuku n.k

c. Endapo itaanzishwa kwa sheria ya Bunge mahakama hiyo itatengewa bajeti ya makadhi, ofisi zao, na wanasheria wao kutoka bajeti ya wizara ya Sheria (au Wizara itakayokuwa na dhamana ya Mahakama.

d. Hata hivyo Waislamu hawakatazwi mahali popote kujianzishia mahakama yao wao wenyewe na kuigharimia, lakini hofu yao (at least baadhi yao) ni kuwa pasipo kibali cha Bunge wanaweza kujikuta matatani.

A) What if ni ndoa ya mchanganyiko? na itakuwaje kama watu wawili walio katika mfarakano wakikimbilia kwenye mahakama mbili tofauti- kadhi na ya kawaida?

B)Hivi kweli haya mambo mawili tu ya ndoa na mirathi ndiyo yatufanye tuumize vichwa ya kuanzisha hiyo mahakama ya Kadhi? Kwani imeshindikana kuweka taratibu ndani ya mamlaka za kiislamu namna ya ku handle hizo issue mpaka tung'ang'nie mahakama za kadhi?

C)Tunaongeza gharama na "KOMPLIKESHENI" zisizokuwa na msingi

D)Wasiwasi wangu ni kuwa kwa kusema wajigharamie wataweza? Maana kama msikiti mmoja tunashindwa kuuendesha tutawezaje mahakama?

HEBU JAMANI TUWE MAKINI, TUNAZIDI KUJICHIMBIA KABURI WENYEWE
 
Kweli,
Itakuwaje kama watoto katika nyumba wako 6 mzee amefariki watatu wakaenda mahakama ya kadhi na wengine watatu wakaenda mahakama ya serikali.
Au
Mume na mke wote waislam; mume akaenda kushitaki mahakama ya kadhi na mwanamke akagundua kuwa shiria zilizoko huko zitafeva mwanaume naye akaamua kwenda mahakama ya serikali je itakuwaje?
Tanzania inaidadi karibia nusu kwa nusu kat ya wakristo na waislam na utamaduni wao unaendana sawa na mchanganyiko huo, sheria wanatunga kulingana na mchangayiko huo wa nusu kwa nusu.

Ukienda Kenya na Uganda siyo nusu kwa nusu hata tamaduni zao zimebase zaidi ktk ukristo and hence hata sheria zao zinafeva ukristo hivyo walikuwa na haki ya kuanzisha mahakama ya kadhi.

sisi Tz bunge letu ni nusu kwa nusu kati ya wakristo na waislam na ndipo sheria zinapotungwa na hata baraza la mawaziri wanaopendekeza miswada ni nusu kwa nusu hivyo kama kuna sheria haitendei haki kundi fulani hufanya marekebisho ili kundi hilo linufaike.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom