Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,270
- 105,445
Hivi inakuwaje mwanasheria mkuu anashindwa kuona makosa ya waziwazi kama haya? Na kama haoni hili anawezaje kusimamia mikataba ya kibepari kama Barrick na Uranium guys toka Marekani? Kama hao mawaziri wataapishwa kesho ni wazi wakubwa watakuwa wamedharau katiba! Hilo halina ubishi. Na watu wataanza ku-question dhamira ya serikali kwa wananchi wake. Nchi haiwezi kuongozwa na watu ambao hawajala kiapo! Hilo halipo sehemu yoyote duniani. Hakuna! Pili, kuna kitu kingine office ya mwanasheria mkuu ajiridhishe. Nacho ni uraia wa wabunge wote wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania wakiwemo mawaziri na naibu mawaziri. Narudia, office ya mwanasheria mkuu ihakiki na kujiridhisha uraia wa wabunge wote wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania pamoja wakiwemo mawaziri na naibu mawaziri.
Makosa ya waziwazi yako wapi? Unaweza kuyataja tuyajadili?
Umesoma ibara ya 68 ya katiba? Unaelewa mtu anaanza kuwa mbunge wakati gani? unaelewa kuna wabunge wa aina ngapi?
Frankly mimi mtu akiniambia mtu kama Mizengo Pinda au January Makamba hastahili kuingia bungeni na hivyo kuwa katika cabinet nitaona ana argument nzuri zaidi ya hizi fringe fanaticism claims ambazo hazina msingi wa kikatiba.
Kama hizi ndizo opposition anazopata Kikwete mtawapa watu msemo kwamba mnamuandama Kikwete kwa kila afanyacho bila kujali ukweli.
Mie si mtu wa kumtetea Kikwete kwa kawaida lakini katika hili hayuko nje ya katiba wala sheria. labda mseme katiba / sheria inayofanya kuwepo na perception ya "oath of office" katika "oath of allegiance" si nzuri.
Watu wengi wanashindwa kutofautisha, wanafikiri kwamba kile kiapo cha Spika ni "oath of office" wakati ni "oath of allegiance"