Eric Shigongo katika siasa za kupotosha wasanii

Didia

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
719
258
Leo katika Kipindi cha Tuongee Asubuhi cha Star TV nimemuona Bw. Eric Shingongo akitangaza Tamasha la Wasanii Lenye Kuitwa "TAMASHA LA UZALENGO TANZANIA KWANZA" Katika maelezo yake lengo la tamasha ni kuwaunganisha wasanii kulinda amani ya nchi ambayo inaonekana kuanza kuvurugwa.

Hii ni njia nyingine ambayo wabinafsi wanaodhani wanajenga na huku wakibomoa amani ya Nchi Yetu Tanzania. Bw. Shingongo anapaswa kuelewa kuwa msingi wa Amani katika nchi na hata familia ni Haki. Ndio maana tulipo pata uhuru nguvu kubwa ya Hayati Baba wa Taifa ililenga kujenga Taifa lenye usawa na haki. Hivyo huwezi kuhubiri kujenga amani bila kuhubiri haki kutendeka katika jamii. Hata kama watanzania tungekuwa na chama/dini moja, pasipo haki, Amani haiwezi kudumu.

Natambua kuna wasanii wengi wabinafsi na au viraza ambao hawaoni au kuelewa matatizo yanayoikumba nchi hii na visababishi vyake hasa UFISADI, UBINAFSI WA VIONGOZI, UZEMBE WA SERIKALI KATIKA KUTATUA KERO ZA WANANCHI n.k. Wapo wasanii wengi ambao kwa vile kwa sasa wanapata vijisenti vya kuendea Club na au kuendesha Toyota Corolla wanadhani shida hakuna. Wasanii hawa huenda wasione hali ngumu ya maisha inayowakumba watanzania wenzao. Hawa watamuunga mkono Shingongo kama baadhi yao walivyo badili nyimbo zao na kuweka tungo za kusifia chanzo cha tatizo wakati wa kampeni za uchaguzi.

Hivi unaposema "Tanzania kwanza" ni yapi ambayo unataka yaje baadae? Wananchi, Siasa, Uchumi n.K? Hivi Mzalendo ni yupi? Yule anayesifia wizi na unyang'anyi, Anayekaa kimya bila kuchukua hatua dhidi ya uovu au anayekemea na kuweka maisha yake rehani kwa mstakabali wa Taifa?

WanaJF nisaidieni kwa kila namna kuwaelimisha wasanii wetu watoke gizani. Najua historia ya siasa ya Bw. Shingongo, bila shaka, malengo yake katika tamasha hili. Tusimuache azidi kutumia nafasi yake kupotosha wananchi.
 
Leo katika Kipindi cha Tuongee Asubuhi cha Star TV nimemuona Bw. Eric Shingongo akitangaza Tamasha la Wasanii Lenye Kuitwa "TAMASHA LA UZALENGO TANZANIA KWANZA" Katika maelezo yake lengo la tamasha ni kuwaunganisha wasanii kulinda amani ya nchi ambayo inaonekana kuanza kuvurugwa.
Atutolee uzandiki na uwongo wake hapa amani ya nchi imevurugwa wapi kama ametumwa na CCM aseme hivyo asituletee majungu anatumia ishu ya amani ya nchi kuvurugwa kwa ajili ya kujinufaisha yeye kwa kukusanya wasanii na kuwafanyisha matamasha ili apate hela halafu background anasema eti amani ya nchi inavurugwa what a crap
 
Aligombea jimbo la Buchosa - wilaya ya Sengerema akazidiwa ujanja wa kugawa hela na wenzie wa CCM.
Hii pengine ni strategy ya kumfanya aendelee kuwepo kwenye gem kusubiri 2015.
 
Kachanwa live kwenye hilo tamasha likalo udhuriwa na watoto wengi na masharobaro asiegemee upande mmoja awaseme na hao waliomfanya aandae tamasha kwa mtazamo ni serikali ya ccm ambayo imeleta hasira kwa watu
 
Msukuma mshamba huyo, anatafuta madaraka ndani ya ccm mpya!
 
Huyu shigongo si ndiye aliyekuwa anaandaa mashindano ya mfalme wa rhymes ambayo alikuwa akipanga washindi baadaye wasanii wakastuka, wakamsusia!!
Huyu bwana ni 'mjanja mjanja' mno.
 
"everyone is talking about crimes, but who are the criminals, some people want to go to heaven but none of the them wants to die". Peter Tosh's song Equal rights. Amani inapatikana/kudumishwa pale tu kunapokuwa na Equal rights and justice kwa raia wote wa nchi. Shigongo analeta tantalila tu obviuos its not his mind bali katumwa na ccm apparently baada ya kupewa mihela kuandaa hiyo kitu
 
Watu wengi wanaangamia kwa kukosa maarifa. Maarifa yanatusaidia kupambanua mambo na kuweza kuiona shillingi katika nyuso zaka zote mbili. Maarifa yanatusaidia kufanya maamuzi katika nyanja mbali mbali za maisha baada ya kufanya uchambuzi wa matoeo ya maamuzi yetu kwa siku za baadaye. Shigongo na wenzake wamegundua udhaifu wa wasanii wetu ambao wengi mfumo wa elimu ya nchi yetu umewanyima fursa ya kupata maarifa hivyo wanaamua kuwatumia kwa manufaa yao. Kuna msemo usemao - ukimnyima mtu elimu utamtawala milele.
 
Mwenye macho haambiwi tazama jamani. Shigongo si mtu huru, ameshikiwa mawazo. Kama kweli anaipenda amani, alikuwa wapi wakati wa mauaji ya Arusha? Au as SOON as CDM walipochochea vurugu, mpaka viongozi fulani waseme ndio na yeye aone kuwa amani inavurugwa? Sucker...
 
Sijui kiwango cha ufahamu wala elimu yake. lakini nataka tu kumwambia
amani haitafutwi kwa kuwaliwaza kwa muziki wanaoshindiliwa misumariyenye kutu mwilini bali kwa kuwatendea haki na kuhakikisha hawaendelei kuumizwa. Amani yaa nchi yetu inahatarishwa zaiddi na CCM na serikali yao inayowakumbatia vibaka, mafisadi na walaghai kama Shigongo mwenyewe, wazushi.
 
Kumekuwa na kelele nyingi juu ya kutoweka kwa amani, kila kukicha wimbo ni amani inataka tutoweka, nnachojiuliza ni yupi anayehatarisha amani kati ya wawili hawa: Yule anayemkanyaga mwenzie au yule anayepiga kelele kuwa anakanyagwa? Wakubwa wamekuwa wakijiwekea maisha mazuri kwa kujilipa posho nzuri huku sisi tukiendelea kuumia kwa kupanda kwa maisha kila kukicha, Sukari juu, unga juu, mafuta juu. Tunaambiwa mafuta yamepanda kwasababu dola imepanda na uzalishaji umeshuka, hebu tujiulize zile tani za sukari alizoziona Kandoro kule Mwanza zimefungiwa kwenye maghala zinasubiri nini wakati mtaani hakuna sukari? Je jirani zetu wao wanatoa wapi mafuta?
 
Vijarida vyake vya bei chee vimechangia sana kuongeza zero 2010, mchambuzi flani wa maswala ya jamii ITV alisema wamiliki wa hivi udaku gazeti wametajirika kutokana na watu masikini wasio na uwezo wa kununua magazeti ya bei maridhawa.Akampoint Shigongo kuwa ni mmoja ya mtu aliyenufaika na watoto wa maskini kukimbilia viudaku vyake.
 
ndugu zangu hapa kazi rahisi sana, mimi naona aandae tamasha lake kama kawaida na jamii yote watakaoweza waudhurie. wahudhuriaji wafanye yafuatayo:

1.Shigongo akijitambulisha
akisema mamboooo........................ watu wanajibu peopleeeeeeeeeeeeees
akisema salaam aleikhum................... "
akisema bwana asifiwe........................... "
aema kistumsifu yesu kristo................... "

2.wasanii wakisimaa tu
wakianza tu yo, yo, nyanyua mikono juu niwaimbie......... watu wajibu peopleeeeeeeeeeeeeees
 
Watu wengi wanaangamia kwa kukosa maarifa. Maarifa yanatusaidia kupambanua mambo na kuweza kuiona shillingi katika nyuso zaka zote mbili. Maarifa yanatusaidia kufanya maamuzi katika nyanja mbali mbali za maisha baada ya kufanya uchambuzi wa matoeo ya maamuzi yetu kwa siku za baadaye. Shigongo na wenzake wamegundua udhaifu wa wasanii wetu ambao wengi mfumo wa elimu ya nchi yetu umewanyima fursa ya kupata maarifa hivyo wanaamua kuwatumia kwa manufaa yao. Kuna msemo usemao - ukimnyima mtu elimu utamtawala milele.

Mkuu hapo penye red nimekusoma
 
ni kweli kabisa asilimia 90% ya masharobalo watakaoenda kweye iyo kampeni na sio tamasha basi elimu ndogo au akuna ndio maana wanatumiwa nakubuluzwa wanasahau mama zao na ndugu zao wanavyoishi wa mlo mmoja au miwili tu kisa elfu au laki kazaa tu,wengine walidiliki kujiita watoto wa flani nashangaa badae wanasema tuwape dili masela, inasikitisha kusema uzalendo wakati wezio watoto wao wamesoma vizuri na kupata ajira nzuri na kuwekewa life insuarance,ki ukweli kuna jambo nyuma yao kama wangejadili kwanza matatizo ya mfumko wa bei, ufisadi, ugumu wa maisha na ajira, matatizo ya umeme, dhuruma kwa wanyonge,then uzalendo ufuate wangekua sawa kabisa.nina shaka na hii naita kampeni ya kisiasa tu na ni:hatari: sana
 
Back
Top Bottom