Equivalent kilio chetu vipi? Na hii serikali

Yuda

Member
Sep 20, 2011
6
1
Sisi ni wanafunzi wa equivalent je kilio chetu sisi tufanyeje kwani mpaka sasa hata hujui kinachoendelea na mlisema watu wasayansi watapewa mkopo asilimia mia moja je, sisi ambao tuna- equivalent hatutakiwi kupata haki hiyo ya msingi. Wengi wetu tumemaliza d.i.t, mist, arusha tech, karume, na vyuo vyote hivyo vinatoa diploma. Je, hawa watu na wanafunzi wanaondelea na masomo ya diploma hasa wasiendelee kusoma kwa kuhofia kuwa watakuja kuambiwa hawatakiwi kusoma digrii kwani wana equivalent, serikali hii isilete mabadiliko mabadiliko kwenye elimu. Sio wote wanapitia form six wengi wanapita kwa diploma labda waweke ulazima kuwa wanafunzi wapite form six, mbaya zaidi bajeti ya elimu mwaka huu imeongezwa kwa asilimia kubwa ili kusaidia watoto wa wakulima lakini bado inakuwa ngumu kwa kutoa mikopo kwa wanafunzi kwanini serikali hii jamani tunaenda wapi? Na sasa tayari tupo vyuoni nataka tuanze shughuli zetu zile, waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi tunaomba usikilize kilio cha wanafunzi hawa mnaowaita equivalent tafadhari.


Hivi mlifikiria nini hadi mkaanzisha hiki kitu equivalent na bado watu wanaendela kusoma hamdhani mnawakatisha tamaa hawa vijana

tuna-amini serikali hii bila maandamano hamuwezi kwenda sasa subirini tukusanyike wote tuanze kazi
 
Kakaaa!! wenzio tumeshakata tamaa.
Ukipiga HESLB unaambiwa "namba unayopiga kwa sasa haipatikani jaribu tena Mwakani!!"
 
Kakaaa!! wenzio tumeshakata tamaa.
Ukipiga HESLB unaambiwa "namba unayopiga kwa sasa haipatikani jaribu tena Mwakani!!"

kwa wale direct applicants walio kosa,kuna list inaandaliwa tena bt kwa nyi equevalant ndo cjajua bado.
 
Kama vipi someni kwa mishahara yenu. Itasikitisha endapo ninyi mtakopeshwa wakati huo direct wasio na ajira wala mshahara wakisota. Equivalent ukienda NMB BANK utakopeshwa wakati direct hawezi. Acheni kulaumu serikali,jipangeni vizuri mlipe msome.
 
Kama vipi someni kwa mishahara yenu. Itasikitisha endapo ninyi mtakopeshwa wakati huo direct wasio na ajira wala mshahara wakisota. Equivalent ukienda NMB BANK utakopeshwa wakati direct hawezi. Acheni kulaumu serikali,jipangeni vizuri mlipe msome.
unafikiri equivalent wote wana kazi/wameajiriwa????
 
Kama vipi someni kwa mishahara yenu. Itasikitisha endapo ninyi mtakopeshwa wakati huo direct wasio na ajira wala mshahara wakisota. Equivalent ukienda NMB BANK utakopeshwa wakati direct hawezi. Acheni kulaumu serikali,jipangeni vizuri mlipe msome.

Hata hujui unachokisema. Kama na wewe unaingia chuo kikuu na akili hii ni hatari kwa taifa letu.
 
Kuwasaidia wale msiofahamu wanaoingia elimu ya juu kwa equivalent ni hivi;
kuna wanafunzi wanamaliza kidato cha nne na kufaulu mitihani yao. Wakati wengine wakichagua kuendelea na masomo ya kidato cha tano wengine huchagua kujiunga na vyuo mbalimbali mfano DIT, MIST, TCA, KARUME, RWEGARURIRA, NIT na vingine vingi vya cadre hiyo ambavyo hutunuku stashahada. Kama kuna mtu hafahamu hilo basi hata zile fomu zinazojazwa wakati mtu anahitimu masomo ya kidato cha nne wengi huwa hawazisomi na kuzielewa vizuri.

Kwahiyo wale waliojiunga na vyuo hivyo wanapohitimu na kutunukiwa stashahada zao wanakuwa na haki ya kujiunga na masomo ya elimu ya juu sawa na waliomaliza kidato cha sita. Si lazima kupata kazi mara tu baada ya kuhitimu stashahada kama baadhi ya wasioelewa wanavyodhani.

Kama serikali inawanyima mikopo hawa wa equivalent kwa sababu nyepesi na potofu kwamba wana ajira wanatakiwa kujilipia basi wanafanya kosa kubwa sana. Nimepata taarifa kwamba waziri kawambwa ametoa tamko alipokuwa arusha-TCA kwamba kuna baadhi ya wanafunzi wa equivalent watapata mikopo hasa wanaosoma masomo ya sayansi na ualimu. Tunasubiri kuona watapatiwa kiasi gani.
 
asante kaka mwiita kwa taarifa zako za kuwa waziri amesema kuwa wanafunzi wa Equivalent watapata mikopo.Ngoja tusubiri tuone kaka.
 
Nini maana ya equivalent si maana mtu anaprofession fulan tayari na kama mtu una profession ni kwanini asiwe na kazi?

hivi unafikiria kwa spinal cord au kwa masaburi?unajua asilima ngapi ya equivalent wakimaliza diploma huendelea na masomo direct bila kwenda kufanya kazi kwanza?unajua asilimia ngapi wa equivalent wakimaliza diploma ndio wanaenda kufanya kazi na sio kuendelea na masomo? kwa hiyo we unadhani mtu akiwa na profession fulan,tena ya diploma,ni lazima awe na kazi??sidhani kama unawaza mbali kala ya ku comment
 
Back
Top Bottom