Epusha yafuatayo udumishe uhusiano

Tausi Mzalendo

JF-Expert Member
May 23, 2010
1,471
722
Kupenda na kupendwa raha sana.Raha hii itakuongezea umri wa kuishi, itakufanya uwe mng'avu kwa kutabasamu kila wakati hata ukiwa gizani au peke yako.Ukiwa kwenye uhusiano unaokufanya ujisikie uko juu ya mawingu, ya nini utake kutia doa au walakini ukatishe utamu unaoupata ndani ya roho yako?

Watu wengi waliokua kwenye mahusiano mazuri tena matamu - wapenzi, wenzi wa ndoa etc.wamejikuta wakitia kasoro zisizo za lazima kwenye mahusiano kwa sababu tu ya kutofahamu kwamba mambo wanayoyafanya ndio sumu kali kwa uhusiano. Laiti wangelijua, pengine wasingeyafanya na huenda uhusiano usingeingia doa.
Mifano ya mambo hatarishi:
1.UONGO- Kutokuwa mkweli bila sababu ya msingi.Kwanini unasema uongo hata pale pasipo na lazima? Ukiwa una tabia za uongo kisha mwenzio akajua ujue tayari umeweka ufa. Ufa huu ukijirudiarudia basi ujue kuna siku ukuta utaanguka na kukuacha na hali mbaya. Kati ya kujenga ukuta mzima,itakugharimu sana. Huenda ikakulazimu hata kubomoa kabisa na kukufanya usiweze tena kujenga ulichokua nacho.

2. WIVU - Wivu siyo hulka mbaya hasa kwa penzi changa.Ni kichochea mapenzi tena chenye nguvu kupindukia. Usipoonyesha wivu kwa mpenzi wako ,basi wewe una walakini mkubwa sana.Ila jihadhari sana kuwa na wivu uliopindukia ikiwa uhusiano wenu ulishakomaa na kuelekea kwenye uchumba au ndoa. Wivu baina ya wanandoa ni kitu kibaya maana inaleta dhana ya kutokumwamini mwenzio.Mume au mke anayelia wivu kila mara hukera na hasa kama wivu huo huzua ugomvi kila mara. Wivu wa kuonyesha kila mara ni sumu kali sana inayoweza kuua kabisa uhusiano au mapenzi. Inashauriwa kuwa kama unajisikia wivu kwa mumeo au mkeo basi, mzungumishe kwa upole na mahaba ili mwenzio ajiskie kama kwamba ni ule wivu wa penzi changa.Hapo mwenzio atacheka na hata kukutania na pengine kukuuliza afanyeje ili uwe na amani.Hapo utapata mwanya wa kuchomekea madukuduku yako yote. Ujumbe utafika kama kulikuwa na mambo yasiyokubalika na hii itaweza kunusuru penzi kama lilikua lime legalega.

3. USALITI -Usaliti ni pigo la nguvu katika uhusiano wowote ule. Usaliti ni silaha ya maangamizi. Unaposaliti mtu ambaye amekuwa mwaminifu kwako asili mia 100 ujue siku akigundua itakua ni kama kumwaga rangi nyekundu juu ya shuka la maua maua. Huwezi kudanganya kuwa shuka imeingia dosari.Hata ufue vipi bado kuna waa litabakia.Hata ukiweka bleach bado uharibifu utatokeza kwa maana bleach itaharibu hata yale maua mazuri yaliyopamba shuka lako.Unaweza kupata shuka nyeupee lakini yale mapambo yatakua yamefutika au kubakia kwa mbaliiii.Jiulize ni kwanini watu wakisalitiana ni afadhali kukataa kukiri kuliko kukiri.Ukikiri ni bora kuachana kuliko kubakia kwenye uhusiano maana gubu litakalofuatia hapo ni jehanamu. Wanaume wanasaliti sana wanawake na hata kuamini kuwa wanasamehewa, na wengine hukiri waziwazi. Kinachotokea baada ya usaliti ni kama ifuatavyo:

a) Kusafisha shuka ya maua kwa bleach,
aliyesalitiwa akiombwa msamaha, huumia zaidi kwa sababu ni uthibitisho tosha kuwa imani ilivunjwa na kwamba kosa lilitendwa. Hata hivyo huo siyo mwisho wa mapenzi au uhusiano kama wahusika watakuwa tayari kujisahihisha na kuponyana.Ila "historia" inakuwa imeshawekwa katika maisha ya kimapenzi ya wahusika hao.Kila mara tukio hilo litawajia akilini hata kama wamesameheana.Wako wanaotumia tukio hilo kama silaha na kukumbushia mara kwa mara. Hii ni hatari maana badala ya kujenga basi ni kuzidi kubomoa. Inaweza pia kutokea kwamba baada ya usaliti, penzi likaimarika hasa kama wahusika watajirekebisha na kubadilika kwa ukweli na siyo kwa kinafiki.

b)Kutafuta jinsi ya kujiponya maumivu kwa namna mtu anavyojisikia.
Aliyesalitiwa aweza kubadili upepo na mwelekeo hata kama anabakia ndani ya uhusiano kwa sababu mbalimbali. Wahusika walioamua kuendelea na uhusiano hujikuta wakishindwa kukatiza uhusiano hasa kama ni wanandoa. Mara nyingi hii hufanyika pale mwanaume anapokua ndio msaliti. Kwa mwanamke mara nyingi hisia za kimapenzi kwa mwanaume wake huisha na kinachobakia ni " mazoea" ya kuwa na mwanaume chini ya dari moja. Wanaume hudhania wamesamehewa na kwa vile hawaoni madhara ya moja kwa moja basi huendeleza usaliti waziwazi! Hawajui kuwa wanajiongezea sumu.

c) Kukatiza mahusiano hata kama bado mapenzi yapo. Hii njia huchukuliwa zaidi na wanaume kwa sababu ya ego! Wako wanawake wachache sana huwaacha wanaume kwa sababu ya tendo moja tu la usaliti.Cha kujiuliza : kwanini wanaume huchukua uamuzi huu ilhali wanawake hubakia kwenye uhusiano? Rejea b) hapo juu utajua kwanini wanawake hubakia.Kwa wanaume, ni ile hali ya kujiamini kuwa "yeye ndiye mwanaume bora zaidi ya wengine" na hivyo hawawezi kukubali kuwa na wapinzani!

4. MENGINEYO - UVIVU, UCHOYO, UCHAFU - HIZI NI TABIA MBAYA na hazipendezi japo siyo lazima zikavunja uhusiano moja kwa moja.Huweka doa though. Pata picha mwanamke mchafu kwenye nyumba - atamfanya mwanaume wake atafute pahala pa kupumzikia hata kama atarudi nyumbani baadae. Uchoyo siyo tu kwa mwanamke bali hata kwa mwanaume.Kuna wanaume wachoyo kwelikweli hata kwa watoto wao wenyewe. Kadhalika uvivu.Ndoa au uhusiano siyo nafasi ya kumtegea mwenzio bali ni fursa adimu ya kusaidiana na kutegemeana.
Tuamke turekebeshe mahusiano.Mahusiano mengi hufa "premature death" bila kuwa na ulazima.
 
source ya hiii?

Hivi kila kitu kina source?
Mtu akisema dalili ya mvua ni mawingu au mwanzo wa ngoma ni lele atataja source?
Kwa kifupi hakuna source ya kurejea kwenye kitabu bali ni life experiences za watu.
 
Epuka kushika shika simu yangu kudumishe mahusiano....! Unapogusa unataka nini? Ukikuta yaliyomo then kifuatacho ni nini kama sio ugomvi na kuachana?
Achana na mambo ya ulinzi uwe huru!
 
Kupenda na kupendwa raha sana.
Raha hii itakuongezea umri wa kuishi, itakufanya uwe mng'avu kwa kutabasamu
kila wakati hata ukiwa gizani au peke yako
nipo hapa mimi
Red: Si weye uliokuwa unalilia juzi kati kupgizana kelele na ubavu wakuo?!
 


1.UONGO- Kutokuwa mkweli bila sababu ya msingi.Kwanini unasema uongo hata pale pasipo na lazima? Ukiwa una tabia za uongo kisha mwenzio akajua ujue tayari umeweka ufa.

Mkuu Tausi Mzalendo, kama umenigusa vile, kuna siku nilikuwa safarini nje ya nyumbani, my half mate akanipigia simu asubuhi for normal greetings, lakini simu yangu ilikuwa bussy na kwa bahati nzuri nilikuwa naongea na simu ya ofisi kwa muda mrefu. Baada ya kuachana na ofisi, niliona missed call yake, nikampigia na bila kutarajia nikamwambia nilikuwa naoga !!! sikuwa na nia mbaya na nilisema hilo neno bila kujitambua kwa kuwa simu ya ofisi ilikuwa imenichaganya, yeye akaniuliza ulikuwa unaogaje na simu yako ilikuwa inaonyesha unaongea na simu nyingine !!! Kwa kweli nilijisikia vibaya; na huenda mwenzangu alihisi kuwa nilikuwa naongea na simu mbaya. Hatahivyo, hakuulizia kuhusu kuongea na simu nyingine; na binafsi nafahamu sikuwa na contact mbaya muda ule, ila tatizo ni pale niliposema nilikuwa naoga, badala ya kusema nilikuwa naongea na simu nyingine hata bila ufafanuzi ni simu gani ambayo nina imani hata yeye asingependa kuifahamu, maana anafahamu simu yangu inakuwa bussy na mambo ya ofisi.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom