Epukeni bidhaa za Game Mlimani City!

Wakuu mtawalaumu wafanyabiashara na manufacturers, lakini mkumbuke mfanyabiashara yupo kupata faida tu hata kwa kuuza kinyesi akisema ni biskuti. Jukumu la kwanza kabisa la serikali ni kulinda raia zake. Kulinda raia zake ni pamoja na kuwaepusha na bidhaa feki. Mtu aliye kijijini Mangaka atajuaje kuwa hii dawa ni feki? Serikali ilitakiwa iwe imeisha mlinda huyu mtu ili hiyo dawa feki isimfikie maana yeye hawezi kutofautisha.

TATIZO LA NCHI HII NI KUWA HAKUNA SERIKALI NA KAMA IPO BASI HAIPO KWA MASLAHI YA WANANCHI WAKE WENGI.

By the way kwanini watu wengi wakifika maeneo ya Mlimani City hupenda kuongea kiingereza. Jambo hili nimelibaini muda mrefu na kila mtu niliyemuambia amesema ni ukweli. Je ni ushamba pia unatusumbua?
Ha ha ha,Teh teh teh teh!

Kwa sisi wabongo hii ndio Shopping Mall kubwa toka inchi hii imeumbwa,sasa inakuja na mambo ya kila aina hasa kwa vijana wa makamo (teens) hasa na mambo ya kuiga iga.
Ila ukibahatika siku mmoja ukisafiri nnje ya inchi,jaribu kutembelea Malls za wenzetu alafu wewe angalia watu wa aina gani wanaenda kwenye sehemu hizo alfu sababu utaijua ya kwanini watu hapo wanbadirisha lugha(usisahau wabongo wanakasumba ya kufikiri kingeleza ndio lugha ya walio kwenye neema na kustaarabika )ambacho sio kweli na NI WIZI MTU
 
Hakuna hatua inayoweza kuchukuliwa dhidi yao mpaka tujue duka lile linamilikiwa na nani, Na ni viongozi gani wana mkono humo! Pili lazima tujiulize kuna nini TBS na TFDA. hawa wanachukua hatua lini? na dhidi ya nani?

Ninajiridhisha kuwa kuna double standard nyingi sana katika utendaji wa hawa waheshimiwa.
 
Siku zote waswahili tunajimaliza wenyewe.
Tamaa ya kitu kidogo inatuangamiza wenyewe hapo sasa hao TBS na TFDA kati yao wamesha daka mlungule na jamaa wanatukamata kama kawa alafu wanasahau kuwa madhala tunayo pata yatawaathiri hata wao kwa upande mmoja am mwingine kwa ajili ya tamaa zao na hao makaburu wakisha kugundua hilo unashusha mzigo wa mayai mabovu,nyama zilizo kaa sana South,fish,soda,juice,bavaria zinazo karibia kuisha muda wake huko South wanajua soko lipo bongo tu na watanunua tu ni kupunguza bei kiduchu...hapo sasa uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii twafaa.
Sijui tukimbilie wapi??
Dawa nikuwawajibisha wenye vitengo husika wanao kula mlungula.
 
Ha ha ha,Teh teh teh teh!

Kwa sisi wabongo hii ndio Shopping Mall kubwa toka inchi hii imeumbwa,sasa inakuja na mambo ya kila aina hasa kwa vijana wa makamo (teens) hasa na mambo ya kuiga iga.
Ila ukibahatika siku mmoja ukisafiri nnje ya inchi,jaribu kutembelea Malls za wenzetu alafu wewe angalia watu wa aina gani wanaenda kwenye sehemu hizo alfu sababu utaijua ya kwanini watu hapo wanbadirisha lugha(usisahau wabongo wanakasumba ya kufikiri kingeleza ndio lugha ya walio kwenye neema na kustaarabika )ambacho sio kweli na NI WIZI MTU

Jaribu kufikiria THE BIG PICTURE. Kwasasa kiingereza ni lugha ya biashara na elimu ya juu! Unafikiri itawezekana vipi watu kujua kutumia kiingereza kama watakitumia darasani tu? Kama mlimani city inatoa fursa kwa watu kukiongea , well ni kitu kizuri na sioni sababu ya kupinga.
 
hehehehe
ina maana bado TBS hawajafanya vitu vyao tu?
walipaswa kutupa taarifa walaji maana madhara ni makubwa yatakayotokea kwa uzembe wa bidhaa feki
 
By the way kwanini watu wengi wakifika maeneo ya Mlimani City hupenda kuongea kiingereza. Jambo hili nimelibaini muda mrefu na kila mtu niliyemuambia amesema ni ukweli. Je ni ushamba pia unatusumbua?
Ulimbukeni na ushamba wa kwamba kila aongea kingreza basi kasoma au status fulani kubwa.....nilikuwa naangalia vile vista duu uchwara irene kiwia na nancy sumari kwenye kile mrembo anajitambua sijui.....vinaongea kingereza kibovu wanavunja ile mbaya.....mpaka aibu nikajiuliza kwanini wasiongee kiswazi tu wanachokimudu.....

again wabogo acheni ulimbukeni na mashopin mall
 
Yo Yo

Acha watu watanue bwana,muda mwingine kuna kuangalia tu bidhaa bila kununua ili upate jua vitu gani vipo na ununue.
Kuhusu hao kina dada kuongea inglishi kwa michu,kama wamekosea basi wanajifunza kwa kuongea zaidi japokuwa nilipenda jaydee alivyoongea zaidi ya hao duuz..mahojiano yake yalikuwa mazuri na ya kueleweka na kazi inaonekana.
Pia kwenye hizo shopping malls wengine unapitia kupata AC kidogo na joto la dar si unajua pia kufurahia mjengo na mavitu ya ndani.
 
Invisible,

Hivi kwanini kama kuna matatizo pasifungwe tu kwa muda maka hapo watakopokamilisha uchunguzi?mie huwa nashangaa sana nchi yangu inavyoendeshwa.

Mataka kakosea ,kwanini asifukuzwe kwanza!Shame
hivi hujaacha kushangaa
 
Mini nadhani hata zile cinema mnazongalia pale New World Cinema ni feki yaani za kichina maana duh! :)
 
Hizi bidhaa za game kweli hazina kiwanga na ta gurantee yao hiyo kitu kikirabika kukubadilishia ni shughuli pevu, mimi nimenunua pasi mbili za kunyooshea nguo hazikumaliza hata mwezi zimekufa, na nilizirudisha kwani zilikuwa na gurantee, wakakaa nazo week au na zaidi na baada ya kwenda kuzichukua zimefanya kazi siku mbili tatu na kufa tena.
 
Belinda belinda
unajua sisi tunaoendelea kukua hicho kiswahili chako kinanipa utata mtupu
hehehe

Nilimaanisha jengo, kiswahili nikichotumia kuwa ni mjengo siyo sahihi kabisa ila kinatumika informal.
Pole Msanii..naamini umenipata sasahivi
 
Hizi bidhaa za game kweli hazina kiwanga na ta gurantee yao hiyo kitu kikirabika kukubadilishia ni shughuli pevu, mimi nimenunua pasi mbili za kunyooshea nguo hazikumaliza hata mwezi zimekufa, na nilizirudisha kwani zilikuwa na gurantee, wakakaa nazo week au na zaidi na baada ya kwenda kuzichukua zimefanya kazi siku mbili tatu na kufa tena.

Pasi nzuri ya kunyooshea nguo nunua brand ya Phillips make ya Singapore. Mimi ninayo zaidi ya miaka 5 waya tu ndo umechakaa lakini bado iko bomba kabisa. Hata Kariakoo nunua tu maana hata ya kwangu niliinunulia huko. Ila hakikisha pasi yenyewe siyo box imeandikwa "made in Singapore"
 
Nilikuwa na rafiki yangu mmoja ambaye anaishi South Africa ambaye amekuja kwa xmas.. ni Mtanzania akaniambia hapa tunaibiwa sana ...si Game na Shoprite pekee bali pia Mr. Price na Woolworth. Anasema kuwa bei za Mr. Price ni 4 to 10 times za bei za Mr. Price South Africa. Pia shati linalouzwa Tshs 100,000 Dar Woolworth linauzwa kama Tshs 10,000 tu South Africa. Na kama sikosei hawa ni wawekezaji ambao wanaleta vitu ambavyo vimezalishwa nchi zingine kwa hiyo ile ajira haipo hapa, vile vile wanasamehewa kodi ya mitaji na 'tax holiday' wanapata.

Nafikiri kunahitajika upembuzi yakinifu kuona kama tunahitaji kweli hawa wawekezaji uchwara ambao hawainui sektaningine, wanavuna na kufanya capital flights, potelea mbali hata kama watakuwa wanashirikiana na watanzania..

Lakini tukiangalia pia....wale wa Kariakoo nao wanatuuzia feki tu. Ukiona nguo yang'ara ujue ukiifua mara moja tu kwisha... hakuna njia ya kutoka hapa tulipofikia?

Unachosema kuhusu bei ni ukweli kabisa. Woolworth na mr price ni maduka ya kawaida sana SA. Mr Price ndo balaa yani kuna vitu vinaanzia randi 10, 20, mpaka 100 hivi. ni vichache ambavyo vinafika mia hamsini. lakini ukifika pale mr price mlimani labda cheapest kinaweza kikawa ni randi 200. wanatuibia kishenzi. hakuna kitu special na zile nguo.
 
Kwa bei hizo tunalipia ubovu wa SYSTEMs zetu-Cost of setting business in TZ, Rushwa, ucheleweshaji wa kuingiza mizigo bandarini na airport, etc. hivyo vyote anayetakiwa kulipa ni mlaji wa mwisho. Unless tunayaondo hayo tutaendelea kulipa price za Juu! Despite all that watu bado wananunua kama hawana akili nzuri sijui ni ulimbukeni au ni kukosa alternative?
 
Hata mie nina wasiwasi baadhi ya bidhaa zao ni feki....tulinunua LG microwave ile ndogo pale GAME..hata nusu mwaka haikudumu..ikaacha kufanya kazi.
At the same time nina LG microwave..ilinunuliwa from Australia ..ina miaka karibu 6 sasa na haijatupa shida hata siku moja.
Sio siri, Tanzania kwa kiwango kikubwa imekuwa soko la bidhaa duni
 
Pasi nzuri ya kunyooshea nguo nunua brand ya Phillips make ya Singapore. Mimi ninayo zaidi ya miaka 5 waya tu ndo umechakaa lakini bado iko bomba kabisa. Hata Kariakoo nunua tu maana hata ya kwangu niliinunulia huko. Ila hakikisha pasi yenyewe siyo box imeandikwa "made in Singapore"

Nakuunga mkono ndugu yangu...!! Ila siku hizi hapa hiyo pasi ya Phillips unayosema ina make ya Singapore zinatolewa copy kama kawaida pale China.

Mwaka jana Dec. nilipokuja nyumbani nilipitia Mlimani City kweli kwavile nina mtoto mdogo nikavutiwa kuingia katika hilo duka la Games...Lakini mara baada ya kutazama tu zile bidhaa niligundua moja kwa moja zilizo nyingi ni feki tena hata kwa kutazama tu bila kuishika na kuichunguza unaweza kutambua hilo.

Je tuna kwenda wapi watanzania..Kweli inafika mahala mtu unajiuliza hao mnao waita TBS wapo kweli ? Au wapo kwa maslahi yao binafsi ?

Hivi kwani kila bidhaa mbovu zina ingizwa Tanzania , Nilipo kuwa Dar kwa bahati nzuri au mbaya katika pita pita zangu niligundua bidhaa nyingi sana zilizopo madukani hazina ubora..NOKIA N95 8GB ulaya ilikuwa kati ya dola 590 hadi 892 madukani ,Lakini simu hiyo hiyo hapo Tanzania ilikuwa inauzwa kati ya dola 238.09 hadi dola 368 .

Tujiulize jamani, tuna kwenda wapi na matakataka hayo. Wenzetu wanasafisha mazingira kwa kutumia plastic zilizosalia na kututengenezea matakataka ambayo wanajua fika baada ya muda mfupi tu tunakuja kuyatupia ndani ya nchi yetu.Kwanini Tbs watufanye watanzania ni sehemu ya kutupia Takataka ?

Nashauri kwa ndugu zangu watanzania wenye uwezo wa kutumia internet services , kwani najua kwa sasa ni wengi wetu wenye uwezo huo..Kabla ya kufanya maamuzi ya kwenda kununua bidhaa ambazo ni imported tujaribu kuingia kwenye ma web site na kufanya uchunguzi wa kina wa kile unachotaka kwenda kukinunua ili uweze kujua thamani na uhalisi na ubora wa bidhaa hizo kabla ya kutoa fedha zako nyingi ambazo utakuja kuzijutia mara baada ya bidhaa ile kuharibika.
 
Ulaya wanatumia Euro na ukiacha UK na nchi zilizo nje ya EU. Ukweli ni kwamba Tanzania bei si kipimo cha ubora wa kitu bali ni usanii mtupu. Mtu unaweza uziwa kitu cha shs 100 kwa shs 10,000 hivi hivi usipokuwa makini.

Halafu tuache longo longo ukichukua vitu vyenye ubora wa Ulaya na Marekani ukivifikisha Tanzania basi ujue kama vipo 10 kila mwaka utauza kimoja tena kwa mtu aliyetoka ulaya, wabongo wengi tunataka vitu cheap huo ndiyo utamaduni wetu uliyowekwa na hali mbaya ya kipato na unyonyaji tunaofanyiwa na waajiri na viongozi wetu.

Kuna kipindi makampuni ya kuchimba madini yalipoingia watu walikuwa wanalipwa vizu sana ila viongozi wakawaambia jamaa kuwa mkiwalipa kiasi kikubwa wabongo hawafanyi kazi mpaka hela iishe.

Sasa tukubaliane kuwa matumizi yana direct relationship na kiwango cha kipato cha watu, Kama zaidi ya watu million 13 kipato chao kwa siku ni below shs 1300 (dola moja) usitarajie wafanya biashara walete vitu vyenye ubora wakati wanunuzi hawana uwezo.

Ila kwa duka kama Game ambalo target yake ni watu wenye kipato cha wastani ni aibu kuuza bidhaa kama za wamachinga. Ninapata imani kuwa huenda wamewaajiri wamachinga na watu wasio waaminifu ambao wanaliua duka lao kwa tamaa za kujitajirisha, tena hawa jamaa ni wezi kweli kweli hawaoni haya hata kukwambia chukua kitu utamlipa nje LOL!.
 
Back
Top Bottom