Ephraim Mrema na Ufisadi TANROADS

kwa kweli Tanzania tuna kazi kubwa sana hasa kwenye swala la utawala bora. kila kitu kinachofanyika tz ni politics tuu.

Msesewe,
Uko sahihi kabisa,mfumo wa utumishi si mzuri,"divide and rule" ndiyo mfumo wa viongozi wengi wa hizi taasisi zetu za umma.Wewe kama ni threat kwa cheo cha kiongozi lazima ushughulikiwe,kama si mwanamtando wa bos umeumia.sielewi ni lini Tanzania tutajaribu angalau kuwa na utawala bora.hii inavunja moyo kwa wafanyakazi wengi tu waliyokwenye mashirika au taasisi za umma.
 
Baada ya madai ya Mbunge Mporogomyi bungeni dhidi ya CEO wa TANROAD, sasa TAKUKURU waanza uchunguzi dhidi ya hayo madai. Habari zaidi hapo chini kutoka Tanzania Daima.

Ephraem Mrema achunguzwa

na Mwandishi Wetu

SIKU mbili baada ya Mbunge wa Kasulu Magharibi, Kilontsi Mporogomyi (CCM), kufichua vitendo vya ufisadi wa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Wakala wa Barabarani Tanzania (TANROADS), Ephraem Mrema, mambo mengine yanayohusu ajira yake yameanza kuibuliwa.

Habari za uhakika zilizolifikia Tanzania Daima Jumapili hivi karibuni, zinaeleza kuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), ilianza kuchukua hatua za kumchunguza Mrema siku moja baada ya kutolewa kwa tuhuma dhidi yake, kwa kuhoji watu kadhaa katika vikao vya siri.

Habari zinadai kuwa, kikubwa kinachochunguzwa ni iwapo analipa kodi kama ilivyoelezwa katika ajira yake Wizara ya Miundombinu baada ya Mporogomyi kumtuhumu bungeni, Alhamisi iliyopita.

Habari zaidi zinaeleza kwamba, maofisa wa TAKUKURU wanachunguza madai ya Mrema kuwahi kupendekezwa kuondolewa kazini, lakini baadaye akaendelea na wadhifa huo anaoshutumiwa kuutumia vibaya kwa wafanyakazi na wasaidizi wake wa karibu.

Kwamba TAKUKURU ilianza kazi kwa kuwasiliana na Ofisi ya Kamishna wa Kodi za Ndani (Domestic Revenue Commissioner) ili kujua kama analipa kodi kulingana na mshahara wake na ajira yake katika Wizara ya Miondombinu.

Wakati gazeti hili likiwakosa wasemaji wa TAKUKURU kuzungumzia suala hilo, lilifanikiwa kuzungumza na Kamishna wa Kodi, Johannes Mally, ambaye hakukana wala kukubali kuzungumza na Takururu zaidi ya kutoa ufafanuzi.

Mally, alisema taasisi yake inalifanyia kazi suala hilo ingawa si kwa faida ya kutoa matokeo yake kwa vyombo vya habari.

“Kama jambo hili limeibuka na kuzua maswali, ni jukumu letu kulifuatilia, lakini si kwa ‘public purposes’. Kuna kipengele cha sheria kinachozungumza wazi kwamba hakuna ruhusa ya kuthibitisha malipo kama yanafanyika au la kwa mteja.

“Cha msingi katika marupurupu kama hayo yaliyoelezwa na mbunge huko Dodoma, ni lazima yakatwe kodi stahili,” alisema Mally alipozungumza na Tanzania Daima Jumapili jana.

Gazeti hili liliomba ufafanuzi wa mamlaka hiyo kuhusu kiwango cha fedha anazolipa Mrema kutokana na mshahara na posho zake kwa mwezi, zinazodaiwa kukaribia sh milioni 30 ambapo Mally alieleza kuwa:

“Kuna utaratibu, kisheria ni kwamba jambo hilo ni ‘secret’ (siri) kati ya mteja, mamlaka na mwajiri. Lakini kwa kuwa mtu unayemtaja ni mwajiri wa Wizara ya Miundombinu, bila shaka tutaangalia ‘source’ yake (mwajiri-miundombinu). Kama analipa au la.

“Nadhani mamlaka nayo ina nafasi yake ya kuchunguza, na matokeo hayo hayaruhusiwi kuwekwa wazi. Kama nilivyosema kwamba haya mambo yanafanyika kwa taratibu husika na ni siri,” alisema.

Mrema alishtumiwa bungeni na Mporogomyi kuwa analipwa malipo makubwa tofauti na vigezo vya kazi aliyopewa, kadhalika stahili ya kiwango tofauti na utaalamu alionao.

Kiwango cha malipo ya Mrema kilichoelezwa bungeni na Mporogomyi, kiliibua hisia tofauti miongoni mwa jamii, hususan madai kuwa licha ya Mrema kuwa Mtanzania, ameajiriwa kwa mkataba unaoonyesha kuwa analipwa kama mgeni, na kuligharimu taifa kiasi cha dola za Marekani takribani 24,450 kwa mwezi (karibu sh milioni 30) mbali ya malipo mengine ambayo yametengwa nje ya pato lake rasmi la kila mwezi.

Alipoulizwa, Mrema alieleza kushangazwa na tuhuma zilizotolewa na Mporogomyi bungeni, na kumtaka mwandishi asubiri kupata ukweli kwa sababu anafahamu kuwa ataanza kuchunguzwa wakati wowote.
 
anachunguzwa kwa lipi? labda kwa tuhuma za rushwa ya mizani ya kibaha, hiko ni sawa kabisa. lakini huwezi kuchunguza kuhusu mshahara na marupurupu yake, kwa kuwa hakuyaweka yeye. kasi hii ya kumchunguza huyu ingeenda sambamba na y akuchunguza tangold, na akina masha wanaoropoka kuko mikoani eti imma ilitelekeza jukumu lake kuisajili tangold kwa maslahi ya usalama wa taifa
 
Nilishasema hapo awali........kwa CEO Mrema kuwepo pale tumekwisha, ulizeni kwanini alifukuzwa kazi toka ktk miradi iliyo chini ya Ofisi ya waziri Mkuu, Ulizieni uhusiano wake na Wizara ya Ujenzi ulivyokuwa wakati alipokuwa Konoike.................no wonder ameyafanya hayo aliyoyafanya pale TANROADS................ulizeni pia kule Zanzibar aliondokaje ondokaje................pia sitashangaa kuwa hiyo nafasi aliipata kwa mgongo wa Lowassa + Chenge!!

....In short huyu Mrema ni hafai
 
Indume,

Unaona double standards za Serikali yetu na hasa vyombo vya dola na sheria?

Mrema katuhumiwa kuwa haieleweki alivyopata kazi na mshahara wake ni mkubwa, TAKUKURU inaanza kumchunguza bila kimemo.

Lakini kwenye suala la Richmond ambalo Lowassa na Msabaha walihusika, TAKUKURU ilisema mapema hakuna kosa na hata baada ya Kamati ya Bunge ya Mwakyembe kubainisha kuwa mchakato mzima wa Richmond ulikuwa na walakini mkubwa na kuegemea kuwa na vitendo vya uhalifu na Rushwa, TAKUKURU wamekaa kimya.

Njoo suala la Karamagi na mkataba wa Buzwagi. Mazingira yanaonyesha ama kuna hujuma au rushwa, lakini Karamagi anapeta na TAKUKURU wamekaa mguu pande.

Ingiza Rada, Chenge katuhumiwa, Serikali na TAKUKURU wanasema hawafanyi uchunguzi wa ndani, hawana sababu kwa kuwa Serikali ya Uingereza inaichunguza BAE. Sasa kama afisa mwandamizi wa Serikali yetu inasadikiwa alipokea Rushwa ili nchi iingie mkataba mkenge, kwa nini Serikali yetu isimchukulie huyu mtuhumiwa na badala yake kudai fidia kwa muuzaji na si afisa mwandamizi aliyefanya uzembu au uhujumu?

EPA, Meremeta, Tangold, CIS. Sijasikia Takukuru kuanza uchunguzi mara moja kwenye hili mpaka Slaa alipopiga kelele ingawa tulishaanza kupiga kelele Mwaka mmoja kabla ya siri kufichuka. Ni vipi TAKUKURU ilipuuzia suala zima na kujifanya haina uwezo mpaka kulazimishwa na Bunge huku uhujumu wa hali ya juu unaendelea BOT kwa kisingizio cha Usalama wa Taifa?

ATCL! Tumeingia mkataba bomu, maafisa wa ATCL wamejinunulia magarina kuingia mkataba mmbovu ambao unaigharmu Serikali na Taifa mamilioni ya fedha. Lakini si TAKUKURU au Polisi waliokwenda kwa haraka kuwachunguza kina Mattaka kuhusiana na hili.

Ripoti ya CAG. Utouh katoa ripoti mwaka jana inayoonyesha uzembe uliokithiri ambao una harufu ya ubadhirifu wa karibu Shilingi Trilioni 3! Lakini sijasikia TAKUKURU wakichunguza hasa lile suala la mikataba na manunuzi yanayofanyika bila kufuata taratibu.

Cha maana TAKUKURU walichofanya ni kukamata watu kwa tuhuma za Rushwa ndogo ndogo na za uzandiki kama suala la kina Mollel na Laizer wa Arusha na kugombea nafasi NEC CCM na sasa hili la Mrema wa Tanroads.
 
Rev. Kishoka.
Ni kweli TAKUKURU na serikali yetu wana double standard linapokuja suala la kuwashughulikia wanaovunja miiko ya uongozi. Suala lolote linalomhusu mtu yeyote ambaye kwa njia moja au nyingine ana mahusiano ya karibu na aidha serikali au SISIEMU basi huyo hawezi kutikiswa unless uwe na bifu nao. Mfano mdogo ni ule wa Wabunge wa SISIEMU Arusha, yaani TAKUKURU haieleweki kabisa. Na sioni umuhimu wa hiyo taasisi, haiko madhumuni ya kulinda rights za Mtanzania.
 
Kwani TUKUKURU inatakiwa ichunguze wakati gani?

Tunajua hilo?

Tatizo si wakati gani, tatizo ni class ya watu inaoamua kuwafanyia uchunguzi. Suala la Richmond hawakupenda kulifuatilia, na walipofuatilia walidanganya Bunge na wananchi wote kwa ujumla kwamba ule mkataba ulikuwa sahihi. Huo ni UOZO, na walifanya vile kwa kulinda maslahi ya wakubwa zao. Sasa hapo utaangalia na kuona nini maana ya class ya watu wanaokuwa dealt by TAKUKURU. Siko hapa kumtetea CEO wa TANROAD bali FISADIZ wote wanastahili adhabu yao pia kwa mujibu wa sheria..
 
Hivi hii mishahara mikubwa ya hao wakubwa ikipunguzwa kidogo ili kasma nyingine iende kuongezea mfuko wa ujenzi wa barabara nadhani hata Mungu atatubariki sana
 
Ukiondoa la kupiga simu na kumtishia meneja wake amfukuze mtu kwa lazima,sina shaka na elimu yake.Anastahili kushika cheo hicho.
Mimi nadhani hizo ni siasa za maji machafu tu,watu wanamalizana kinamna.TUACHE MAJUNGU.
 
nilishasema Hapo Awali........kwa Ceo Mrema Kuwepo Pale Tumekwisha, Ulizeni Kwanini Alifukuzwa Kazi Toka Ktk Miradi Iliyo Chini Ya Ofisi Ya Waziri Mkuu, Ulizieni Uhusiano Wake Na Wizara Ya Ujenzi Ulivyokuwa Wakati Alipokuwa Konoike.................no Wonder Ameyafanya Hayo Aliyoyafanya Pale Tanroads................ulizeni Pia Kule Zanzibar Aliondokaje Ondokaje................pia Sitashangaa Kuwa Hiyo Nafasi Aliipata Kwa Mgongo Wa Lowassa + Chenge!!

....in Short Huyu Mrema Ni Hafai

Tuache Majungu, Alikuwa Kwenye Mradi Wa World Bank/ida, Uraba Sector Rehabilitation Project, Matunda Yake Ni Ukarabati Mzuri Wa Urban Municpal Roads, In Mbeya, Iringa, Moshi, Nk Manispaa 8, Mradi Huo Ulisha Isha Na Mkataba Ukawa Umefika Mwisho, Hali Kadhalika Zanzibar Etc

Kama Ni Tuhuma Za Perormance Hazina Ukweli, Ila Kwa Hizo Za Rushwa Siwezi Kumtetea.

Tangu Awali Nimesisitiza Hapa Huyu Mtu Anapigwa Vita Kwa Sababu
Kuwa Ni Wa Kuja Pale Tanroads, Wengi Walidhani Wale Wazoefu Wa Pale Wangepata Ile Nafasi, Bahati Mbaya Haikuwa Vile, Yaliyobaki Ni Vita Badala Ya Kuchapa Kazi
 
Sikonge,

..i will grant you the benefit of doubt ktk haya masuala ya ukabila.

..i will also speculate kwamba ulihemewa tu ulipotoa mfano kwamba Mramba[mchaga] na bajeti ya barabara ni moja ya dhuluma za serikali dhidi ya mikoa ya pembezoni.

..naomba pia nikuelimishe kwamba mradi wa barabara jimboni kwa Mramba ulianza wakati wa John Magufuli. pia mradi ule ulipewa pesa zaidi wakati wa Mramba kwasababu ulikuwa ktk advanced stage ya ujenzi. Mbunge aliyelalamika mradi wake ulikuwa ama ktk design stage au feasibility study, ndiyo maana ukapewa fedha kidogo.

..nilitegemea baada ya posting yangu ungejielimisha zaidi kuhusu miradi hiyo miwili, na pia ungeomba radhi kwa kauli yako.

..nasubiri kwa hamu kuona kama Mbunge Selelii, na wenzake, atamkaba koo Waziri wa sasa miuondo mbinu Dr.Kawambwa, kama alivyofanya kwa Mramba mwaka jana.

..Basil Mramba ana kashfa[kuchapisha noti chafu na kampuni ya kijerumani, misamaha ya kodi...] nyingi tu kama mwanasiasa, lakini hili la kusema amedhulumu barabara za jimboni kwa Lucas Selelii na wenzake, siyo kweli.

..tofauti uliyoitaja kuhusu Kilimanjaro,Mbeya,Arusha, kulinganisha na mikoa ya pembezoni ni suala kihistoria. ule msingi[elimu,miundo mbinu...] uliowekwa na wamisionari na wakoloni ndiyo unaowapa ahueni mikoa hiyo. vinginevyo nchi nzima imeathirika kutokana na uongozi mbaya wa Tanu na baadaye CCM.

..zaidi siamini kama Mchaga,Mhaya,Mnyakyusa ana akili zaidi, au ni mjanja zaidi, au ni mchapakazi zaidi, kuliko Muha, Mnyaturu, Makonde etc etc. tofauti za makabila hayo ni exposure tu.

..naamini kabisa kabisa kwamba Waha,Wanyaturu,...wangepewa historical opportunities walizopewa Wachaga,Wahaya,..basi leo hii Kigoma,Singida,Mtwara, ingekuwa inasifika kwa "maendeleo" na Kilimanjaro,Kagera,..ingekuwa ndiyo mikoa ya pembezoni.

..hakuna hata siku moja nchi nzima[makabila yote,mikoa yote]itakuwa ktk hatua moja ya maendeleo. siku zote kutakuwepo na maeneo yaliyopiga hatua zaidi kulinganisha na mengine. kitu cha kuzingatia ni kujaribu kuzielewa tofauti hizo, na zaidi eneo moja kujifunza toka eneo lingine. mara nyingine maendeleo hupatikana kwa kuiga.

..nashauri kabla ya kuwashutumu Msuya na Mramba, tuwabane kina Samwel Sitta,Rashidi Kawawa,Maokola Majogo,Ben Mkapa,Nalaila Kiula, Anna Abdalah, Jakaya Kikwete,Paul Kimiti,Chrisant Mzindakaya...wajieleze kwanini wameshindwa kuhimiza maendeleo ktk mikoa ya kusini na mingine ya pembezoni.

JokaKuu,
Uliyoyaandika mwanzo naona "bado jujanipata" ila ya chini yote naona kuwa umenielewa. Ila ukichukulia uliyoyaandika wewe hapa chini juu ya mikoa iliyoendelea na ukiangalia juu, unakuja kuelewa ni nini hasa ninamaanisha. Wasiwasi mie ni kuwa "huko kubaki nyuma kwa watu wa Sikonge" na kwenda mbele kwa WACHAGA ni tatizo kubwa. Unasahau kuwa nimesema wazi kabisa "kwangu mimi naliona hili ila WANGAPI HUKU KWETU SIKONGE WANALIONA HILI....?" Kutokana na hali hiyo, watu wa Tabora, Singida, Kigoma nk ni watu rahisi sana kuwa MANIPULATED kutokana na UJINGA wao (si upumbavu). Na huu ujinga na UMASIKINI kama utaachwa, kesho unaweza KULIPUMUA mambo. Jokakuu, kuna dada yangu ambaye alikuwa haifahamu vizuri Tabora. Alipokwenda kusoma huko (na likizo anakwenda kwao DAR au Sikonge) ndipo akaniambia kwa mdomo wake kuwa "Kaka, Tabora kweli MASIKINI..."
Kwa ufupi ili unielewe ni kwamba "Mikoa kama Kilimanjaro, Arusha, Dar na DODOMA..." ni kama SITTING ROOM ya Tanzania. Hii iwe isiwe hata kama watu wakila NYASI (Mramba) lazima iwe mbele. Ila haina maana kule sleeping room na CHOONI mwa Tanzania kusahaulike. Sijui kama umeshafika Sikonge JokaKUU. Jitahidi ufike huko na uone jinsi watu WALIVYOCHOKA. Watu niliosoma nao shule ya msingi sasa wanaonekana kama BABA ZANGU. Tumbaku imewamaliza kabisa. Inatia uchungu sana. Sasa ukiona na maendeleo yote ya WACHAGA/WAHAYA na bado wanazidi kuongezewa, mhhh. Wakati Wachaga/Wahaya wanalilia kuwa na VIATU na sasa wanapewa hadi LEATHER MOCCASIN , huku kwangu Sikonge watu wanalilia MIGUU. Sijui kama sasa umenielewa.

NB: Juu ya Mramba na CEO kuwa WACHAGA, niliitumia tu kama KIOO kuonyesha tatizo hilo la kukosa MIGUU Vs VIATU. CEO wa TANROAD kwa Sikonge ni mtu wa Mwisho ambaye tutamhitaji. Kwetu sisi huyu bwana anatoa VIATU. Sie huku twamsubiri mtu atakeyukuja na kutupa MIGUU kwa kutuonyesha wapi kuipata na kama tutakuwa WAVIVU basi mie ningelipenda hata kwa FIMBO atupeleke huko HOSPITAL kwenye MIGUU. GET ME NOW?? HAKUNA KUHEMEWA HAPA. All in all UCHUNGU WANGU NI KUWA CHOONI KUMESAHAULIKA KWA KILA KITU ZAIDI YA KUJA KUCHUKUA KODI. Na hilo Bunge letu sijui SAID NKUMBA ambalo kila mwaka CCM wanatuletea ...
 
Ukiondoa la kupiga simu na kumtishia meneja wake amfukuze mtu kwa lazima,sina shaka na elimu yake.Anastahili kushika cheo hicho.
Mimi nadhani hizo ni siasa za maji machafu tu,watu wanamalizana kinamna.TUACHE MAJUNGU.

Wee, UMUSHOSHORO.
JE una UHAKIKA na hayo unayoyasema kuwa TUACHE MAJUNGU? Mie sina na ndiyo maana CHICHEMI. Heri ya wanaokuja na kusema HAFAI na kuweka walau point moja kwa nini hafai. Wee OGAH, hebu tueleze zaidi au fafanua zaidi maana wengine ukisema ULIZA, hatuna pa kuuliza. Huku kwetu Sikonge umwuulize nani? Heri ya JESHINI (JKT) walikuwa kulikuwa kuna RADIO MTINI.
Juu ya elimu yake hata mie nimeridhika, ila kuwa CEO je ana uwezo huo? Angelikuwa walau CIVIL ENGINEERING aliyekuwa kwenye UJENZI wa muda mrefu nafikiri ungelisema kuwa anauzoefu. Huko kwenye ujenzi inabidi uwe MENEJA kweli wa Mradi. unaongoza timu ya watu kibao na kuwa incharge wa visehemu vingi sana. Lazima uwe mtu wa kufikiria hata kinachoendelea mjini na mambo ya kisiasa. Tuseme kesho una kazi ya kubeba kifusi na kumbe kesho hiyohiyo wanafunzi wa UDSM wanaandaman barabarani. Kama wewe hujui kweli siku hiyo UTALIWA pamoja na kukodisha maroli ya kubeba hicho KIFUSI. Sasa mtu aliyekuwa anafanya makadirio ya bei, yeye sanasana anahaha na Benki kuu, bei za vifaa, mafuta,kodi nk kwani hivi vinaweza kuharibu mahesabu. Ni mtu anayekuwa na kitimu tuseme cha vijana kama 15. Sasa akija kuwa CEO wa TANROADS, Mhhhhhhh!!!!!!! Huo ni muono wangu tu kwa sifa ambazo hadi leo nimesoma. Ninaweza kuwa WRONG.
 
Tuache Majungu, Alikuwa Kwenye Mradi Wa World Bank/ida, Uraba Sector Rehabilitation Project, Matunda Yake Ni Ukarabati Mzuri Wa Urban Municpal Roads, In Mbeya, Iringa, Moshi, Nk Manispaa 8, Mradi Huo Ulisha Isha Na Mkataba Ukawa Umefika Mwisho, Hali Kadhalika Zanzibar Etc

Kama Ni Tuhuma Za Perormance Hazina Ukweli, Ila Kwa Hizo Za Rushwa Siwezi Kumtetea.

Tangu Awali Nimesisitiza Hapa Huyu Mtu Anapigwa Vita Kwa Sababu
Kuwa Ni Wa Kuja Pale Tanroads, Wengi Walidhani Wale Wazoefu Wa Pale Wangepata Ile Nafasi, Bahati Mbaya Haikuwa Vile, Yaliyobaki Ni Vita Badala Ya Kuchapa Kazi


Hakuna Majungu Mzee..........i just gave the leads.........wanaofuatilia hili suala.....hizo informations zitawasaidia kujua Mrema ni nani...........na ndio maana tuko hapa Mkuu
 
Tuache Majungu, Alikuwa Kwenye Mradi Wa World Bank/ida, Uraba Sector Rehabilitation Project, Matunda Yake Ni Ukarabati Mzuri Wa Urban Municpal Roads, In Mbeya, Iringa, Moshi, Nk Manispaa 8, Mradi Huo Ulisha Isha Na Mkataba Ukawa Umefika Mwisho, Hali Kadhalika Zanzibar Etc

Kama Ni Tuhuma Za Perormance Hazina Ukweli, Ila Kwa Hizo Za Rushwa Siwezi Kumtetea.

Tangu Awali Nimesisitiza Hapa Huyu Mtu Anapigwa Vita Kwa Sababu
Kuwa Ni Wa Kuja Pale Tanroads, Wengi Walidhani Wale Wazoefu Wa Pale Wangepata Ile Nafasi, Bahati Mbaya Haikuwa Vile, Yaliyobaki Ni Vita Badala Ya Kuchapa Kazi

Kwimbi,
Kuna Dr mmoja alikuwa Arusha. Huyu jamaa pamoja na kufanya kazi nchi za nje na kuliliwa huko, aliamua kurudi nyumbani. Jamaa alikuwa HARD WORKER si kawaida. Alianza kupigana na SYSTEM ya hiyo sehemu na jamaa wakatangaza vita na yeye. Walitumia WEAKNESS moja kuwa jamaa hakuwa na uzoefu au elimu katika management. Nasikia alikuwa akilalamika kuwa muda mwingi anautumia KUJIBU maswali wizarani/kwa Rais kuliko kuchapa kazi. Jamaa alikuwa akitumia UZOEFU wake na KUJUANA nje ya nchi na kutafuta MISAADA kwa hiyo sehemu. Mwisho jamaa walimzidi kete na aakchia ngazi. Kuna wengine wanadai kuwa Kikwete kampa muda akasomee UONGOZI and then HE WILL BE BACK. Wengi wanadai kuwa jamaa kukosea hii MBA kwake ilikuwa PIGO KUBWA SANA. vitu vingi alikuwa akifanya kama yuko JAPAN. Jamaa wakawa wanatumia huo UAMINIFU wake kufanya mabaya kwa jina lake. Jamaa hahitaji kukata tamaa.
Ninamfahamu jamaa aitwaye KAAYA wa DAWSCO. Hawa walikuwa Wahandisi waliomaliza INDIA na kuja kutupwa NUWA by the time. Walianza kwa kusota kwenye MADAWATI na kidogokidogo wakaanza kuibadilisha NUWA na kuondoa Wazee wote wa zamani. Sasa hivi wao ukiwabilidha kibao sijui itakuwaje. Huyu jamaa anaweza kuwa na TATIZO hilo. Ila sijui ukweli uko wapi kati ya anayosoma OGAH na wewe. Time will tell. Sijui ukweli hapa uko katikati??
 
shaloom wandugu,

Hayo ya Kilaza Mrema yalishasemwa sana hapa, na jinsi alivyoifanya tanroads mali ya wachagga!

Kwakweli ana maamuzi ya kimangimangi hasa tena wakati mwingine ya kitoto!

Lakini hayo yote ni kwakuwa alipata hiyo chance kwa mgogo wa LOWASSA, akisaidiwa na CHENGE, bila kumsahau kakayake ambaye ni rafiki wa lowasa MREMA WA NGURUDOTO ARUSHA.

Kaanguka Lowassa, Chenge, Sasa zamu yake Mrema!

Here it comes out!
 
..tatizo ni hayo mabilioni anayolipwa na Tanroads.

..angekuwa jeshi la magereza usingesikia Mbunge yeyote akimlalamikia.
 
Tanroads ya wachaga? chadema pia? na tiaraei nako? mwana wakubali wachaga kiboko. Ukabila 2010 utakuwa moto, beware Tanzanians.

Wachagga waache kuomba kazi serikalini na wakiwa qualified wanyimwe ili angalau kuwe na nafasi kwa wengine!

Nimesoma suala hili na hoja zote. Naomba niseme machache.

a. Malipo:
Je taasisi za serikali zina utaratibu gani wanaotakiwa kufuata wanapoamua kumuajiri mtu kutoka nje (mtaalamu) au mwenye sifa ya kitalaamu? Je utaratibu wa malipo umeanishwa vipi na ni kwa kiasi gani taasisi hizo ziko huru kujipangia malipo yao?

Kama hakuna utaratibu wa kuweka mipaka ya malipo (caps) na hivyo kila taasisi iko huru kumuajiri mtu yeyote na kwa malipo yoyote yale. Sasa kama mtu anaweza kunegotiate na akapata anachotaka/anachostahili kwanini yeye ndiyo alaumiwe badala ya wale waliomuajiri?

b. Waajiri
Kama kuna kwa Bw. Mrema liko kwa aliyemuajiri. Kama Mwajiri wake hakujua sifa zake na akakubali kutoa mamilioni ya shilingi kila mwezi basi si kosa la Mrema. Yeye kaomba kazi, kanegotiate mkataba, kaweza kushawishi malipo na pecks nyingine, na serikali imekubali kumlipa. Je TANROADS ina utaratibu gani wa kuajiri CEOs?

c. Mtaalamu
Kama sifa za Mrema kama mtaalamu aliyekubuhu zina ukweli, swali la msingi ni je katika thamani ya fedha tutalipa nini utaalamu huo? Je angekuwa ni mtaalamu mzungu mwenye sifa hizo angelipwa kiasi hicho? Ili tuweze kulinganisha hatuna budi kujiuliza je Mghana aliyekuwepo kabla yake alikuwa analipwa kiasi gani? Kama alikuwa analipwa well below anacholipwa Mrema basi kuna kesi, lakini kama malipo yao yanakaribiana, basi hoja itaulizwa kwanini tukatae kumlipa Mtanzania mwenzetu mwenye utalaamu wa aina hii lakini Mghana tulimlipa?

Kama ni kweli kuwa utaalamu wake ni muhimu sana na anaweza kufanya kazi mahali popote duniani, hatuna budi kujiuliza kule Uingereza wataalamu kama yeye wanalipwaje? Kama anacholipwa UK ni chini sana ya anacholipwa TZ basi hatuna budi kulalamika. Lakini kama ameacha malipo makubwa na kutake paycut kuja kufanya kazi Tanzania kwanini tusiappreciate hicho?

Leo hii kuna wabongo wengi nje ya nchi ambao wamebobea katika maeneo mbalimbali ya utaalamu. Kuna mainjia na madaktari wanaotengeneza karibu dola elfu kumi au zaidi kila mwezi. Wapo wengi wa ngazi za kati ambao mshahara wao tu uko kati ya dola 4 na elfu sita. Ukichanganya na pecks nyingine mtu yuko ahueni.

Sasa huyo anapoamua kurudi kufanya kazi TZ ambako analipwa dola 1500 kwa mwezi au dola 2000 na baada ya kubembeleza anapata hadi kiasi cha dola 3000 kwa mwezi kweli tutaita ni ufisadi. Mtu unapoamua kuondoka nchi hizi za magharibi na kwenda nchi nyingine kuna gharama ya kile kinachoitwa "lifestyle" ambapo wana take into consideration comfortability of your life na hivyo wanaiwekea thamani.

Hoja hapa iwe siyo mtaalamu aliyekubuhu na hastahili malipo hayo. Lakini hatuna budi kuuliza wataalamu wengine wanalipwaje?

Ukabila
Kwa mara nyingine zile chuki dhidi ya wachagga zinaendelea kujitokeza kila jina la Kichagga linapotajwa. Tumefikia mahali wachagga wasiwe viongozi wa idara yoyote ile Tanzania na serikali itoe Memo kuelezea kuwa Wachagga hawastahili kushika nafasi yoyote ya juu, na kama wanashika wahakikishe kuwa akija mchagga "mwenzao" kuomba kazi asipewe nafasi hayo ili kusije kuonekana ukabila.

Na wachagga wote wenye kushika nafasi za juu serikalini wajiuzulu ili kupisha wananchi wa makabila mengine.
 
Tanroads ya wachaga? chadema pia? na tiaraei nako? mwanak wakubali wachaga kiboko. Ukabila 2010 utakuwa moto, beware Tanzanians.

TIARAEI ndiyo wapi? Au ina maana ya Ti Ar Ei? hihiiii Mie nilishachekwa kuwa sisi Watanzania tunaitamka vibaya R. Tunasema ARA badala ya AR... Sijui upi ni ukweli. Wakali wa lugha nijulisheni ili siku nyingine nijitete.
Huu ukabila mama naomba unisaidie. Mie najua tatizo lipo na inabidi liongelewe ila kuna wengine wanadai kuwa hiyo imesababishwa na HISTORIA ya nchi katika devide and rule..... Au mie nina KIHINDIHINDI nini? Maana Kizunguzungu Tanzania hakipo tena na sasa kwa mbali nahisi Kichagakichaga. Just asking.
 
Back
Top Bottom