Enzi Zetu.

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,610
1,809
iringa00.jpg

Hii imetulia naona umekumbusha historia kwa kiasi fulani, EAR (East Africa Railway) hii ni wakati ule Jumuiya yetu ina nguvu, :dance:
 
Nimeikubali pia hiyo ilikuwa miaka ya ngapi?
.. FL1 Hiyo ilikuwa miaka ya 72 mpaka 76 kabla Iddi Amin hajaivuruga Jumuia ya Afrika ya Mashariki. Kiukweli enzi hizo nakumbuka jinsi maisha yalivyokuwa yametulia, amani na upendo. Usafiri kiukweli kabisa ndio wa aina hiyo ni Mwendo wa Layland tu mashine ikiwa inakaribia kijijini kwenu unasikia mlio kuanzia kilomita 5 mnakimbilia stendi. Enzi hizo ukiwa senti 20 wewe kidume maana unatanua mpaka watu wakome kuringa. Sikumbuki kama enzi hizo niliwahi kunywa maji yaliyochemshwa maana hakupakuwa na uchafuzi wa mazingira kama sasa, unatoka shule unakimbilia bombani unakinga mdomo ukitosheka unasonga mbele. Enzi hizo ukitaka kununua sukari kwenye duka la RTC au duka la ushirika la kijiji lazima ununue na jembe tena foleni inaanza saa 11 alfajiri ukiwahi unaweka jiwe kujishikia nafasi. Enzi hizo kituo cha radio ni kimoja tu Radio Tanzania hakuna mambo ya FM sterio. Enzi watangazaji ndio wale akina David Wakati, Suleiman Kumchaya, Stephen Mlatie, Lucas Matipa, Seif Salim Mkamba, Mustafa Nyang'anyi na wengine. Enzi hizo ukijenga nyumba huna haja ya kuweka ma-grill wala nini maana ni amani tupu, Enzi hizo hata kama unatembea usiku ukikutana na mtu ndio kwanza unamkimbilia muongozane hakuna kuogopana sio kama sasa ukiona mtu usiku unajiandaa kwa kujihami maana huna uhakika kama ni mtu mwema. Enzi hizo viatu vilikuwa kutoka kampuni ya bora ukivaa kama ni siku ya sikukuu basi unatembea kwa kuchagua sehemu za kukanyaga ili kiatu kisichafuke, enzi hizo hapakuwa na mgao wa umeme wala maji, enzi hizo hata makonda wa mabasi walikuwa na vimikoba vya kuwekea pesa sio kama sasa konda anakusanya nauli noti anazikunja tu atakavyo, enzi hizo kulikuwa na noti ya shilingi 5 ilikuwa na rangi ya kahawia (brown) na noti ya shilingi 100 yenye picha ya mmasai na rangi nyekundu. Kwa kweli maisha yalikuwa raha mno. Enzi hizo watu wake kwa waume walikuwa wanaaminiana sio kama siku hizi mwanaume hamuamini mwanamke na mwanamke hamuamini mwanaume (eti tumia kinga) nadhani hizo kinga zilikuwa kwa ajili ya kupanga uzazi wa mpango vinginevyo ukipata demu huna shaka we unapiga nyama kwa nyama!!! Kama kuna kikwazo basi Tetracycline (rangi mbili) zilikuwepo kurekebisha matatizo madogo madogo. Enzi hizo gazeti ni Uhuru, Mzalendo na Daily News tu. Matumizi ya lugha yaliheshimika kila sehemu. Enzi hizo mkitangaziwa kuwa mwenge au kiongozi anakuja mnaweza kusubiri kuanzia saa 2 asubuhi mpaka saa 8 mchana hakuna kulalamika, enzi hizo mjini Dar hapa UDA zilikuwa za rangi ya njano na kijani iliyopauka katikati mstari wa kahawia magari aina ya Laylanda BMC inakibwenzi mbele watu walistaarabika mko kituoni mnapanga foleni kuingia kwenye basi.Enzi hizo mitindo ya nywele ni afro kwa sana, wanaume suruali za kitambaa cha klimplini juu inabana halafu chini ni kumwaga tu (buga), shati kwa mtindo wa Ngwabi linabaaa!, akina mama/dada nyewele nao afro au zinachomwa na kitana cha moto then zinakuwa laiiiiini, viatu vya Laizoni kwa sana...Ah! Enziiii hizooooo jamani.:biggrin1::biggrin1:
 
Hivi EAR ndio ilizaa TRC? Manake kuna yale mabasi ya Relwe (nafikiri ilitokana na Tanzania Railway Corporation, ambayo ilikuwa ina mabasi na treni, ninaweza kusahihishwa) yanafanana sana na hilo kwenye picha, ila sikumbuki kuona hiyo nembo ya EAR mbele.
 
Duu hiyo miaka sikuwepo na ndo maana sielewi naomba basi kama utapata picha ya kina mama na Afro hair miaka ile niburudike
 
Hivi EAR ndio ilizaa TRC? Manake kuna yale mabasi ya Relwe (nafikiri ilitokana na Tanzania Railway Corporation, ambayo ilikuwa ina mabasi na treni, ninaweza kusahihishwa) yanafanana sana na hilo kwenye picha, ila sikumbuki kuona hiyo nembo ya EAR mbele.
..Dina, EAR ni kirefu cha East Africa Railways wakati wa iliyokuwa jumuia ya Afrika mashariki. Wakati wa uhai wa jumuia hiyo shughuli nyingi zilifanyika kwa pamoja kati ya Kenya, Tanzania na Uganda. Shughuli kama reli, usafiri wa anga, posta na simu zilikuwa katika EAC (East Africa Community). Mwaka 1977 baada ya Iddi Amin kupindua serikali ya Milton Obote akatangaza Uganda kujitoa katika jumuia hiyo, hivyo automatically jumuia ikafa na wakakubaliana kugawana mali ndio kisa cha Tanzania kupata AICC Arusha, Kenya Kupata KICC (Kenyata International Conference Center) waganda sikumbuki wao walipata nini. Tanzania baadaye ikaamua kutengeneza shirika lake la reli ndio TRC....Nadhani kama sio wendawazimu wa Amini huenda jumuia ingekuwa imekomaa kiasi cha kutosha sasa.
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom