Jaguar
JF-Expert Member
- Mar 6, 2011
- 3,438
- 1,026
- Thread starter
- #61
Nakumbuka tulipokuwa form 2 kibaha sec,tuliunda makundi mawili,TERROR SQUAD na MURDER INC.mi nilikuwa TERROR SQUAD,basi mwalimu wa nidhamu mr.kunambi alizinasa habari kuhusu haya makundi.Yeye aliamini MURDER INC ni kundi la wauaji na TERROR SQUAD ni magaidi.Basi aliapa kuwakamata members wa makundi yote na kuyavunjilia mbali.Baada ya upelelezi mkubwa,tulikamatwa wote,kengele ya dharura ikapigwa,watu wote mstarini.Tukapitishwa mbele watu watuone,mwalimu wa nidhamu akahoji malengo ya makundi yetu ni nini,tukajibu ni 'just for fun'.Mwalimu hakujua kuwa yale ni makundi ya music huko marekani,hata hivyo tulipigwa marufuku na huo ndo ukawa mwisho wa makundi yetu.