Enzi hizooo dunia kabla ya kuwa kijiji kimoja.

Jeho

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
5,053
5,503
Niifananishe na nini dunia hii ninayoishi, imefanana na nguo iliyochakaa, iliyojaa viraka kila sehemu.
Hebu angalia leo hii mambo yanayofanyika duniani, mara kuhalalisha ukameruni, wizi wa kimachomacho wa watawala, migomo kila pembe ya dunia. Haya yote ni tofauti na enzi zile.
1.Enzi zile ili binti aolewe ni lazima awe hajachakachuliwa.
2.Enzi zile kiongozi alikuwa anawajibika kwa raia wake lakini leo hii kiongozi anawajibika kwa tumbo lake.
3. Enzi zile uongo haukuwa kama leo. Leo hii mtu kwa kutumia kimdomo cha shetani(simu) anaulizwa swali uko wapi anajibu niko ofisini kumbe yuko gesti na mke/mme wa mtu.
4........................
5........................
Handsome wa mama nawasilisha, waweza ongezea mambo ambayo yalifanyika enzi zako lakini leo hii yanafanywa kwa hali ya tofauti na kipindi kile.
 
..enzi hizo michezo ya watoto kibao...kombolela, kidali poo, kutengeneza magari ya mbao au mabati...lakini siku hizi...kila mtoto anataka computer game acheze vice city...hata kutengeneza gari la kopo tu hawezi...!!
 
4. Enzi zile disko lilikuwa ni disko la ukweli, leo hii huwezi kuita disko wanaita club mwee
5. Ukumbi wa disko sakafu ulikuwa ni wa vumbi, leo hii sakafu zenyewe zimejaa malumalu kibao!
 
..enzi hizo michezo ya watoto kibao...kombolela, kidali poo, kutengeneza magari ya mbao au mabati...lakini siku hizi...kila mtoto anataka computer game acheze vice city...hata kutengeneza gari la kopo tu hawezi...!!

Ndo maana watoto wengi wa leo hata kutembea umbali wa km moja hawezi.
 
...enzi za wali ndondo..sasa..viazi mbatata yai.

...tulionga kanga...sasa...simu.

...tulitafuna maembe toka kwa mti...sasa...mwendo wa juisi.

...

...
 
Enzi hizo "mpita njia" aliweza kutoa adhabu kwa mtoto aliyekosa na mzazi akashukuru kwa mwanae kufunzwa....
 
Enzi hizo "mpita njia" aliweza kutoa adhabu kwa mtoto aliyekosa na mzazi akashukuru kwa mwanae kufunzwa....

Leo hii mpita njia akipiga mtoto aliyekosea anaulizwa kama hana watoto.
 
...enzi za wali ndondo..sasa..viazi mbatata yai.

...tulionga kanga...sasa...simu.

...tulitafuna maembe toka kwa mti...sasa...mwendo wa juisi.

...

...

Tena tulitafuna maembe kwa kutumia meno tu ukijitahidi sana ni visu vilivyotengenezwa kwa kutumia makoa.
 
Back
Top Bottom