Enzi hizo

hahaha kweli enzi hizo! Halafu kulikuwa na sabuni zinaitwa kodrai, komoa hivi bado zipo zilikua sabuni nzuri za kufulia.
 
Yaani usiseme kabisa, kodroy zipo bado mjini ila hiyo YU for Men niliikuta mwaka jana pale Nakumati Nairobi yaani usiseme! Halafu nikakutana na Ambi (Lotion na sabuni yake) Kwa wakina dada wa enzi hizo watasema lolote, kweli viwanda vyetu hoi hata Gardenia na malaika siku hizi sizioni na kama zikitoka utakutakuta jamaa zetu wach... wametia moko, we haya we!!!!?!!!!!!!
 
nani aliwahi vaa chupi ya v.i.p hapa?mara ya kwanza jamaa alikuja toka dar basi siku hiyo tunacheza mpira mkoani huko jamaa kaja mpirani halafu kava bukta kuubwa lina uwazi,basi kakaa juu ya jiwe mguu mmoja huku mmoja hukooo almradi tuone kavaa mchupi wa v.i.p lol.
 
Back
Top Bottom