Enzi hizo kuogeshwa

Kweli tumetoka mbali yaani sidhani kama kuna ambaye hajapitia, umenikumbusha mbali sana na siku ukipewa "golden chance" ya kuoga mwenyewe penda usipende utarudishwa tu bafuni maana hutakuwa umeoga vizuri na lazima ukaguliwe na Mama.
 
1236445908635.jpg

child-enjoying-a-bath-at.jpg
 
wangapi waliogeshwa kwa mtindo huu utotoni?mana unaambiwa fumba macho ukifumbua sabuni yake machoni utakoma!!!!!!!! !mana unasuguliwa na dodoki,jiwe au chupi yako na usipokuwa na balanceutakoma mana unasimama na mguummojaa uone hiki nn!!!!!

Da! Nimekumbuka mbali sana, kumbe maisha anayajua mwenyezi mungu pekee!
 
du!!! nimemkumbuka sana mwanangu, halafu yuko mbali na mimi, huwa najisikia raha sana ninapomuogesha, halafu naye anafurahia kuogeshwa na BABA.
 
Hahahaha. Kuna jirani zetu walikuwa wanakula wali kwa nadra. Yaani siku ukiwaona saa kumi wameoga hawatoki kwao ujue kuna mchele aka cheka-na-wana. Sie kwetu tishio lilikuwa utalala chini!
Hizi habari za kuoga utotoni zimewahi kuwanyima wenzenu kula wali msizifanyie mzaha!!!
 
Afu ilikuwa kama makusudi flani. Unaachwa na
hiyo sabuni hadi unakoma. Na hiyo balaance ya mguu ni balaa. Jamani!
wangapi waliogeshwa kwa mtindo huu utotoni?mana unaambiwa fumba macho ukifumbua sabuni yake machoni utakoma!!!!!!!! !mana unasuguliwa na dodoki,jiwe au chupi yako na usipokuwa na balanceutakoma mana unasimama na mguummojaa uone hiki nn!!!!!
 
Nilikua naogeshwa kwa maji baridi na nikilia kuwa maji ni ya baridi mama alikua ananiuliza kwani vumbi nililochezea lilikua la moto?

Nakala kwa mama yeyoo.(Mama mzazi yumo humu jf)

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
issue ilikuwa kuchana nywele aisee. unataka kutoka unadakwa unachanwa nywele hadi kwenye ngozi.
 
Yote tisa, mimi nilikuwa naogopa kuchanwa nywele tu. Mgogoro!. Kabla hazijaisha na kuwa upara, nilikuwa na nywele nyingi nyeusi nene sasa zinakua haraka na kuchana sitaki, kunyolewa naogopa kutaniwa kipara songa ugali!, basi tena.
 
issue ilikuwa kuchana nywele aisee. unataka kutoka unadakwa unachanwa nywele hadi kwenye ngozi.

nimekumbuka dada yangu hadi alkuwa chozi linamtoka.. Mwisho wa siku thje best way mother akawa anapitisha mkasi kwa wote
 
hii imenikumbusha mbali sana.....tulikuwa na housegirl mnoko sana....alikuwa ananisugua miguu na jiwe basi ananikwangua huyo......nilimchukia sana.......

Ndio maana miguu yako hasa huo wa kushoto una makovu, kweli kila kizazi na enzi yake alafu kwenye kusuguliwa lazima watumie dodoki, kama ukiwa mdogo unaogea ndani ya karai la bati (siku hizi ni vifaa vya ujenzi wakati enzi zile tulitumia kuogea)
 
Heri yako uliyekulia "angani"acha wenye uzoefu wa kusuguliwa na mawe tujikumbushe
mwambie mwaya.....kwanza anajishaua tu!!!!!!!!! mi nilikuwa nachukia ukimaliza kuogeshwa mfano ni usiku basi nguo uliyofunikwa wakati unatoka kuoga ndo utakayofungwa wakati unasubiri kula.....ule ubaridi wa nguo ulikuwa unaniudhi hadi nikawa nalazimisha nioshwe mchana ila ndo ukijichafua tu usiku lazima yawepo tena marudio.
 
Kweli tumetoka mbali yaani sidhani kama kuna ambaye hajapitia, umenikumbusha mbali sana na siku ukipewa "golden chance" ya kuoga mwenyewe penda usipende utarudishwa tu bafuni maana hutakuwa umeoga vizuri na lazima ukaguliwe na Mama.

na ilikuwa siku ukipata hiyo chance....huogi, basi unachofanya ni kupiga pasipoti yaan unanawa miguu na mikono hlf na unajimwagia maji kichwani ili ionekane umeoga.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom