Wewe mtani wangu Bishanga nasikia ulikuwa selule kule, kwa hiyo kazi yako ilikuwa ni kulinda hanga...kweli?.Kwa tuliobahatika kuhenya JKT enzi hizo,embu tujikumbushe top ten za disco la enzi hizo. Naanza:
Kule kwa chinova,
kule kule,
kule kwa chinoova,
tunasonga na kuzimbabwe,
masika na toye,toyela
toye,toya na kuzimbabwe,
mama na babaeee,tunasonga na kuzimbabwe.
Jamani ongezeni mistari hapa na pia angusheni na ma singo mengine yaliyovuma JKT enzi hizo !
jkt haijali wewe ni mtoto wa mkulima,tajiri,nyerere wala kawawa,wote mlikuwa mnachangnywa kapu moja,na ole wako ijulikane we babako Rais,waziri,katibu mkuu au MD wa shirika la serikali,utashughulikiwa mpaka unyooke.Kuna mtu aliwahi kunipa hadithi kama hii ya kwako kuwa wanachoka mpaka inafika mahali hawatamaniani tena,...inaonekana ilikuwa raha sana lol.
selule mwenyewe! Mi nilikuwa mtunza bustani bana ruvu fire coy,ila kwa wizi wa nyama (kijeshi inaitwa kusogeza) mi ndo nilikuwa mwenyewe,naziibua za moto kwenye gudulia.Siku moja MP akanibamba live,nikafungwa peki bega na mzigo wa nyama,siku nzima nikakimbizwa uwanjani naimba...'mimi mwizi wa nyama'...hahahahaaa jkt bana!Wewe mtani wangu Bishanga nasikia ulikuwa selule kule, kwa hiyo kazi yako ilikuwa ni kulinda hanga...kweli?.
mtani,gudulia lenyewe si mpaka ulifikie?unaikumbuka kwata ya kuelekea kwenye gudulia? Halafu mkisha kula ni moja,moja mbili tatu,moja,yaani maafande wanawarusha eti wanapanga matofali ya jeshi matumboni mwenu!Du hi hi hi...umenikumbusha mambo ya kuwania top layer usawa wa gudulia!.
Kwanini waliiondoa huku kwetu?...Israel na Germany system hii ya vijana kwenda jeshini kwa mujibu wa sheria mpaka leo bado ipo,ina manufaa yake makubwa tu (for those countries which can afford it).
Hehehe! Ila ilikuwa nzuri sana, vijana wanapata ukakamavu kabla ya kwenda chuoni..chezea kambarage nyerere wewe,unamjua unamsikia?
Kama ni hivyo inatakiwa irudishwe...jkt haijali wewe ni mtoto wa mkulima,tajiri,nyerere wala kawawa,wote mlikuwa mnachangnywa kapu moja,na ole wako ijulikane we babako Rais,waziri,katibu mkuu au MD wa shirika la serikali,utashughulikiwa mpaka unyooke.
Jkt was the best leveller of our society.
wee said Kerren,nambie dada experience yako siku ya kwanza afande anakurushia bukta na T shirt kisha anakwambia hilo ndo gauni lako la harusi?JKT.....lilikuwa na faida zake: mojawapo ukakamavu na kujua kuishi mahali popote! It was a good experience.
ngoja tuwaite vingunge wa jukwaa la siasa waje wajibu hii hoja,sisi wengine ni magwiji wa mmu na chit chat.Moja ya vitu nilitamani sana lakini nikavikosa!! But nilipeenda ili nikawe fit zaid na kukaa mkao wa ki-askari zaidi though sio askari. Kitu kilichonisikitisha ni kusema ilifundisha "uraia" na "uzalendo" lakini nikiangalia kwa asilimia kubwa kizazi kilichotuonyesha kukosa uzalenda kwa mali na rasilimali za nchi hii ni kizazi kilichopita JKT, japo pia kizazi kilichokosa JKT nacho kimekuwa ni kizazi cha kulalamika saaaaana bila actions!
Hebu wanikonvisi tena upya kwenda JKT labda nitafikiria
kwa hiyo mkuu ulijifunza na utaalam wa kilimo cha zabibu,mimi jkt nilitika nikiwa bingwa wa gardening,kuchoma mkaa na kufyatua tofali,of course na kufyatua SMG (sikuji kwa nini AK47 hazikuwepo).Nilipenda every moment ya JKT hasa baada ya kuzoea. Hii ilichukua miezi mitatu plus.
Homa ilikuwa inaanza kupanda baada ya kupata form iliyokuambia unaenda kambi gani. Basi hapo utacheki na wenzio ili uone uko na kina nani.
Mi nilipangiwa Msange/Masange Tabora, lakini nikavecha nikaenda Makutupora. Kwata huko kwa kwenda mbele.
Ila nilijiunga na Usanii ( Kikundi cha Sanaa cha Jeshi ) ambako nilikuwa mahiri hadi nikaombewa na AFande incharge wa Dept hiyo nisikatwe bogi.
Marafiki tuliokuwa nao JKT wamekuwa wa kudumu maana mnakuwa mmepitia mambo magumu but mazuri pamoja.
Sijuti kwenda JKT.... kwa kweli.
AKA ...... wa Makutupora... LOL ( n.b: AK = Askari wa Kike) maana tulikuwa na Force Number.
Mpo hapo?
Naongezea.....
ha ha ha ha
siku moja Makutu, ( short form ya Makutupora) mdada mmoja AK .. akawa ana rafiki yake wa kiume. Sasa kumbe walikuwaga wanakutana na may be ku vi do huko katika hanga la wanaume. Kumbuka JKT mahanga yote ( mabweni) ya maaskari wa kike ni Serengeti na yako mbali na wa kiume.
Nadhani wale vijana wenzie na yule mkaka aidha walichoshwa na kula ugali kwa picha ya samaki ( tehe) au walichoshwa kuringishiwa mwenzao anapata wakati wao wanacheza golf usiku; wakamchomea kwa MP Kimaro...
zile time ambazo yule mdada alikuwa anatoroka kwenda kule chini mahanga ya wanaume ( nikifikiria hivi leo with hindsight advantage, nadhani ilikuwa baada ya disko la usiku kombania, alikuwa harejei nasi Serengeti maana pana kaumbali ).
siku hiyo yuko ndani ya neti ya mkaka, MP KIMARO huyu hapa!
mida hiyo saa tisa usiku hivi. yaani usiku mnene.
Valangati na Timbwili lililozuka hapo, usipime. Ukapigwa ukunga kuamsha kikosi .. na wao wahanga wakaambiwa wazunguke kikosi kizima wakiimba kuwa 'sisi Waz....' imagine.
Na nadhani walifungwa pia ( ndio JKT kulikuwa na jela) maana tulipoondoka siku rasmi ya kufunga msimu wetu , 30 June 198... wao walibaki.
mmh !