Nahisi itakuwa kweli. Nasikia waksti mwingine wanafumlngulia pressure ndogo km ushahidi tu! Iweje uwe karibu na barabara, eti usipate maji? Hawa jamaa wamekuwa sugu kabisa!Kwa taarifa yako, maji kimara hayawezi kupatikana. Wauza maji wote wametengeneza mtandao wao na watu wa DAWASCO, ili wakate maji wao waje kutuuzia na magari. Jaribu kufanya utafiti utaelewa na kama kuna mtu anabisha alete
sababu za kukosekana maji sehemu hizo.
Tatizo mnyika na kubenea hawafuatilii suala hilo. Wameshikilia kufuatilia mambo ya maandamano tu. Maendeleo kwenye majimbo hawana mpango nayo.Mwanzo mlisema mwisho wa March, baadaye mkasema May, baadaye July. Yaani imekuwa ni mwendo wa kusogeza tarehe mbele!
Je, shida ni nini? Bomba bado halijamalizika au nini? Ajabu ni kwamba hata zile sehemu tulizokuwa tunapata maji walau mara moja kwa wiki sasa ni miezi inakwenda mitatu hatupati hata tone! Shida ni nini jamani.
Kimara na Mbezi yote, ukiacha baadhi ya watu walio usawa wa si zaidi mita mia tano kutoka Morogoro road maji hayafiki kabisa. Tatizo ni nini? Mbona mwaka jana shida haikuwa kubwa hivi?
Tafadhali sikieni kilio chetu, enyi wahusika, na mtoe taarifa nini kinaendelea!
Inawezekana mkuu. Kuna figisu figisu za kufa mtu.Kwa taarifa yako, maji kimara hayawezi kupatikana. Wauza maji wote wametengeneza mtandao wao na watu wa DAWASCO, ili wakate maji wao waje kutuuzia na magari. Jaribu kufanya utafiti utaelewa na kama kuna mtu anabisha alete sababu za kukosekana maji sehemu hizo.