England vs Spain under 21 European Championship

Kalumbesa

JF-Expert Member
Nov 24, 2010
1,013
356
Haya wadau wa soka..ligi kuu ulaya zimekwisha lakini fursa ya kushuhudia kandanda safi na maridadi bado ipo..hii game inachezwa leo tarehe 12/06/2011 mishale ya saa tatu na dk 45 saa za tanzania..Itakuwa ni mechi kali hasa ikizingatiwa timu zote mbili zinaundwa na vijana waliochipukia wengi wao wakiwa wameshawika katika ligi kuu za ulaya..Kwa upande wa England wapo vijana hatari kama Daniel Sturridge(Chelsea),Jordan Henderson(Liverpool), Chriss Smalling(Man Utd),Phil Jones(Blackburn and Man U bound),Marc Albrighton(Aston Villa),Jack Rodwell(Everton),Connor Wickham(Ipswich Town) na kwa upande wa Spain kuna vijana hatari kama Bojan Krkic,Thiago Alcantaraz,Jefren Suarez(Barcelona), Juan Manuel Mata(Valencia), Javi Martinez(Athletic Bilbao), Diego Capel ( Sevilla) na Daniel Parejo( Getafe )...

Kwa wale wadau wa soka maridadi..This is a game to watch !!
 
Hivi kama kuna utata hapo kwa Bojan Krkic ni mhispania kweli.?
Kuna dogo wa England anacheza Totenham ( Daniel Rose) yuko nondo ile mbaya. I predict: England 1:3 Spain.
 
Hivi kama kuna utata hapo kwa Bojan Krkic ni mhispania kweli.?
Kuna dogo wa England anacheza Totenham ( Daniel Rose) yuko nondo ile mbaya. I predict: England 1:3 Spain.

Bojan Krkic ni Mhispania unaweza uka google ku confirm...Spain wamejaliwa kuwa na vipaji ndugu..Danel Rose kweli yumo sikumtaja maana sikudhamiria kuwataja wote nimewachukua wachache...Naona umemkumbuka kirahisi nalazimika kuhisi wewe ni gunners fan..Naomba nitofautiane na wewe I predict England 2 - Spain 1..
 
Hivi kama kuna utata hapo kwa Bojan Krkic ni mhispania kweli.?
Kuna dogo wa England anacheza Totenham ( Daniel Rose) yuko nondo ile mbaya. I predict: England 1:3 Spain.
Bojan wazazi wake ni kutoka Serbia but alikuwa anachezea timu ya vijana ya Spain,na Serbia wakawa wanataka wamchukue achezee timu ya wakubwa Spain ikabidi wampe uraia na akachaguliwa timu ya wakubwa ya Spain
 
Danny Welbeck amesawazisha dakika ya 88

Spain 1 England 1
Full time
 
Bojan wazazi wake ni kutoka Serbia but alikuwa anachezea timu ya vijana ya Spain,na Serbia wakawa wanataka wamchukue achezee timu ya wakubwa Spain ikabidi wampe uraia na akachaguliwa timu ya wakubwa ya Spain
Baba yake ni kutoka Serbia na aliwahi kutumika katika kuandaa timu za watoto za Barcelona, amezaliwa Catalonia na mama yake ni Mcatalani na ndo sababu kawa raia wa Spain sababu ya mama yake.
 
Baba yake ni kutoka Serbia na aliwahi kutumika katika kuandaa timu za watoto za Barcelona, amezaliwa Catalonia na mama yake ni Mcatalani na ndo sababu kawa raia wa Spain sababu ya mama yake.

Ya kwa hiyo kiufupi anakuwa ni raia wa Spain by birth,though angeweza kuukana wa Spain akachezea Serbia..ila maisha yote yuko Spain as a result hana sababu ya kuwa M-serbia...Ila Spain wamesheheni vipaji jamani!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom